Shule zaripotiwa kugomea uchunguzi wa matukio ya ulawiti

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Wilaya ya Moshi Vijini, Ramadhan Mahanyu amesema amesema baadhi ya shule zimekuwa zikigomea kutoa ushirikiano kwa na timu za ukaguzi zilizotumwa na mamlaka za juu.

Katibu Mahanyu ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao cha walimu wakuu wa shule za bweni wilayani humo, ambapo ameipongeza Shule za Scolastika na Aniwarite katika halmashauri ya wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kwa kutoa ushirikiano kwa wakaguzi wanaoendelea kufanya tathimini ya mmomonyoko wa maadili hasa katika shule za bweni.

Amesema shule kuwagomea wakaguzi kufanya ukaguzi katika shule na kuzungumza na wanafunzi, ni jambo ambalo linatoa tafsiri mbaya kwa mamlaka kuwa huenda kuna jambo haliko sawa ambalo linalofichwa.

"Shule za Scolastika na Aniwarite zinatoa ushirikiano kila wakati tunapohitaji kufuatilia jambo, liwe la ukaguzi au uchunguzi na viongozi wao wanaturuhusu kukagua hadi mabwenini ili tujiridhishe na huduma zinazotolewa. Niombe shule nyingine nazo zifanye hivyo kwani tunahitaji kujenga na kuboresha,"amesema.

Katika kikao hicho ambacho kiliitishwa na Halmashauri ya Moshi mahususi kwa ajili ya kutathimini mwenendo wa kuporomoka kwa maadili yanayohusiana na uhamasishaji wa vitendo vya ulawiti shuleni, katibu Mahanyu amesema ni wakati wa walimu kushirikiana kwa karibu na wadau wa elimu na serikali ili kuboresha maadili na taaluma shuleni.

Aidha Katibu huyo amewata wakuu na wamiliki wa shule hasa za bweni kuanza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara mabwenini ili kubaini nyendo za wanafunzi wanapokuwa bweni ikiwa ni pamoja na wazazi kuwa nguzo muhimu kati ya walimu na serikali huku akisisitiza umuhimu wa wazazi kupunguza ulevi na tabia nyingine zinazowafanya kukosa muda wa kutoa malezi katika familia zao.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi Moris Makoi ameagiza wakuu wa shule kufanya kazi bega kwa bega na serikali katika kutokomeza tabia zinazoashiria kukiuka maadili ya kitanzani.

Serikali kuptia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetuma timu ya wataalamu kuchunguza mienendo ya wanafunzi huku ikijielekeza kubaini kama kuna hamasa ya kufunfishana vitendo vya ulawiti katika baadhi ya shule hasa za bweni.

MWANANCHI
 
hivi siku hiizi tume za uchunguzi zimekuwa nyingi sana hivi hawa usalama wa taifa wanafanya kazi gani eti au yapo kwenye ugaidi tu kama kuna ulawiti mashuleni tumeni usalama wa taifa wafanye kazi kwa siri na walete taarifa
 
Kuna watoto wameshalawitiwa huko, ndio maana shule zinagoma kutoa ushirikiano...polisi waingilie kati hapo.
 
Wazazi muanze kupima "kipenyo" cha anal za watoto wenu wanaporudi likizo mujue kama wameshaanza kamchezo ka "sopeka sopeka".
 
Mpaka nchi igundue suala la ushoga ni kubwa itakuwa too late.

Bado mtaendelea kuwalaumu mabeberu.
 
Back
Top Bottom