Shule za Serikali na Seminari za Kikristo zapeta Kidato cha Sita: !

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,270
SHULE za Sekondari za Serikali zimeng’ara katika matokeo ya Kidato cha sita mwaka 2011 baada ya wanafunzi wake saba kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi kumi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ni wavulana.Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako aliwataja wanafunzi kuwa ni Muhagachi Chacha (Kibaha), Samwel Katwale, George Felix (Mzumbe), Amiri Abdalah, Comman Nduru na Kudra Baruti (Feza Boys), Aron Gerson, Shaban Omary na Francis Josephat (Tabora Boys), George Assenga (Majengo).

Dk Ndalichako pia aliwataja wasichana kumi waliofanya vizuri zaidi katika mtihani huo na shule zao kwenye mabano kuwa ni Doreen Kabuche (Benjamin Mkapa), Rahabu Mang’amba (Kilakala), Mary Mosi (Kifungilo Girls), Nuru Kipato (Marian Girls), Zainabu Hassan (Al-Muntazil Islamic), Catherine Temu (Ashira).
Wengine ni, Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matovola (Kilakala) na Suzana Makoi (Tarakea).

Alitaja shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 30 kuwa ni, Marian Girls, Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St Mary’s Mazinde, Ilboru, Tabora Boys, St Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga Seminari.

"Shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 30 ni Uru Seminary, St James Seminary, Maua Seminary, Same Seminary, Dungunyi Seminary, DCT Jubilee, Parane, St Joseph- Kilocha Seminary, Mlama na Masama Girls,"alisema.
 
Hii imekaa kidini zaidi. Waislamu wengi wenye uwezo hawaendi kwenye Seminary za waislamu kutokana na sababu mbalimbali wengi wako kwenye hizi za wakristo wengi tuu
 
Watu badala ya kujaribu kujenga mshikamano katika jamii yetu, kila kukicha baadhi yenu mnakaa kutafuta visingizio vya kuigawa. Nashindwa kuelewa watu wenye kasumba ya namna hii wanaojiita au kujiona ni wasomi. Kama Mwalimu alivyosema dhambi ya ubaguzi haina mwisho.

Jaribuni kutumia uhuru wenu wa maoni vizuri kwa kuonyesha ukomavu wa fikra.
 
Jamani mbona hamsemi 'A' na 'B' walizo pata kwenye masomo ya kiisilam? mi nadhani walikonsetrate zaidi upande wa masomo ya kidini ndo sabubu wakachemsha masomo mengine na kufaulu zaidi yale waliyosoma vizuri.:frusty::frusty::frusty::smile-big:
 
Jamani mimi hili naona linaturudisha nyuma tunajadili udini mimi mkristo sioni sababu ya hoja hii kujadiliwa mkimaliza la udini mtaanza,wachaga wana akili kuliko Wandengereko kweli hapa tujisahihishe
 
Hii vipi?

Zainabu Hassan (Al-Muntazil Islamic)

Al-muntazir Islamic seminary!!.. ipo maeneo ya upanga surrender bridge ... wanaupinzani na Feza boys katika kuibiana walimu! O-leval wanatoa cabridge certificate ile mitihani ya UK. A-leval ndio wanafanya NECTA.

Katika ile ligue ya upanga katika Shaaban robert, Mzizima, Tambaza , Jangwani ... naona sasa wao ndio wapo juu zaidi before it wasnt like that!... nilisoma hapo O-leval kabla ya kwenda Mzumbe Advanced. Ni islamic seminary but ni mixed wanachukuwa watu wa dini nyingine pia. As long ukiwa ndani ya shule unafata sheria zao.

Al Muntazir Schools :: Homepage
 
Hata Feza Boys & Girls imekaa kiislamu sana tu.

nakumbuka walitaka iwe islamic seminary... kapuya akawaambia waifanye Boys Only, ili kuingia kwenye ramni kipindi kile waliwachukuwa wanafunzi waislamu toka shule za serikali na kuwapa mtihani wa fanye waliopasi.. waliwasomesha bure... imekaa kiislamu zaidi lakini wanachukuwa dini zote. wana walimu wazuri.. ila bei yake mjasiria mali hawezi kuimudu
 
natoa pongezi za dhati kwa shule za SERIKALI NA ZA SEMINANARI..... sasa na SHULE ZA CHAMA CHA MAPINDUZI zifuate mfano huo
 
SHULE za Sekondari za Serikali zimeng’ara katika matokeo ya Kidato cha sita mwaka 2011 baada ya wanafunzi wake saba kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora kitaifa.Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa jana jijini Dar es Salaam, wanafunzi kumi waliofanya vizuri zaidi kitaifa ni wavulana.Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako aliwataja wanafunzi kuwa ni Muhagachi Chacha (Kibaha), Samwel Katwale, George Felix (Mzumbe), Amiri Abdalah, Comman Nduru na Kudra Baruti (Feza Boys), Aron Gerson, Shaban Omary na Francis Josephat (Tabora Boys), George Assenga (Majengo).

Dk Ndalichako pia aliwataja wasichana kumi waliofanya vizuri zaidi katika mtihani huo na shule zao kwenye mabano kuwa ni Doreen Kabuche (Benjamin Mkapa), Rahabu Mang’amba (Kilakala), Mary Mosi (Kifungilo Girls), Nuru Kipato (Marian Girls), Zainabu Hassan (Al-Muntazil Islamic), Catherine Temu (Ashira).
Wengine ni, Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matovola (Kilakala) na Suzana Makoi (Tarakea).

Alitaja shule kumi bora katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 30 kuwa ni, Marian Girls, Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St Mary’s Mazinde, Ilboru, Tabora Boys, St Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga Seminari.

"Shule kumi bora zenye watahiniwa chini ya 30 ni Uru Seminary, St James Seminary, Maua Seminary, Same Seminary, Dungunyi Seminary, DCT Jubilee, Parane, St Joseph- Kilocha Seminary, Mlama na Masama Girls,"alisema.

Mimi nimefurahi kuona wamo pia wanafunzi wa kiislam waliofanya vizuri, hili ni somo kwa baadhi ya waislamu wanaodhani kuwa kuna upendeleo katika usahihishaji n.k. Ieleweke wazi kuwa bidii bidii na msingi mzuri kwa mtu yeyote ni uhakika wa kufanya vizuri kwenye uwanja wa taaluma.
 
Back
Top Bottom