jonas amos
JF-Expert Member
- Jul 4, 2016
- 3,621
- 4,401
Salamu wapendwa wana jf
Naomba kuweka wazi kabisa katika hili sipo kwa maslai ya ccm chama tawala au ukawa/chadema kwa wapinzani naomba nisimame kama mtanzania
Siku chache baada ya Mh. Rais wa JAmhuri ya muungano Tanzania Dr. John pombe Magufuli kukataza michango ya aina yoyote ile katika shule zote za serikali. Ikumbukwe tu baada ya kauli hiyo ambayo kisheria tamko la Rais ni sheria na inayofuta ni utekelezaji tu
Baada ya kauli hiyo wadau na wananchi mbalimbali walizungumza wengi wao wakionesha wazi kutokufurahishwa na hilo.
Sasa hapa naomba nielekee kama kichwa cha habari kinavyojieleza
Kutokana na katazo hilo shule mbali mbali za serikali za bweni zimeanza kuwaondoa wanafunzi wake
Ikiwemo mkoa wa katavi
Naomba niistaje kwa majina shule hizo kwa sasa
Wanafunzi wametakiwa kurudi nyumbani mapema iwezekanavyo huku kikao cha wazazi na bodi ya shule vikisubiliwa. Hali hii inatokana na wingi wa wanafunzi hao na shule ikijikuta haina uwezo wa kuwahudumia wanafunzi hak kwa chakula na baadhi ya shule ambazo zilikuwa zikiharakisha ujenzi wa mabweni zikijikuta kusitisha kwa muda huku wakisubir miongozo Kutoka kwa waajiri wao ya mkurugenzi wa halmashauri
Ikumbukwe maeneo ya vijijini wanafunzi wengi wanatoka mbali na mashule ya secondary kwani unakuta kata nzima sekondari ni zaidi ya tatu zinategemea sekondari moja. Aidha kwa wazazi waliowengi wamepokea hili kwa masikitiko makubwa na baadhi niliojaribu kuongea nao bado hawajajua nini wafanye kunusuru elimu kwa vijana wao hasa kulingana na gharama na changamoto za usafiri
Inawezekana kabisa watafiti au washauri wa mh Rais walifanyia Dar pekee ambapo wanafunzi wengi wanatokea nyumbani kwani usafiri wa uhakika unapatikana na pengine kwa gharama nafuu kuliko
Huku kwetu kwanza niseme hakuna ruti za daladala bei ya chini ya usafir ambayo nitatoa hapa mchanganuo wake ni sh. 2000 kwa safari ya kwenda tu hakuna nafasi za wanafunzi kwani safari hizo hufanywa na mabasi makubwa ya mikoani
Mzazi moja
"Nauli ya kutoka nyumban hadi stendi kwa bodaboda ni sh3000
Stand kwenda shule ililo ni sh. 2000
Hivyo kwa asubuhi tu itakuwa ni sh. 5000 manake kwa siku atatumia sh 10000
Uwezo huo mzazi anase sina mie ni bora nilipe chakula na mlizi ambapo huwa ni gunia moja na sh. 5000 thaman ya gunia ni elfu 30000 hivyo ni afadhar alipe hata laki moja kwa mwaka kuliko kulipa tsh. 260, 000/=kwa mwezi
Lakini pia kwa watoto wa kike itakuwa ni Changamoto nyingine kubwa mno hasa kutoka vijana wa kiume wasio wastaarabu hasa bodaboda usishangae baada ya miezi kadhaa wanafunz wakashindwa kumaliza shule kwa sababu za mimba
Ikumbukwe malengo ya kujenga mabweni ilikuwa ni kumpatia mazingira mazuri mwanafunzi ikiwemo muda wa kujisomea kwa uturivu awapo shuleni
Hivyo kama watoto hao watatokea nyumba kuna uwezekano mkubwa ufaulu ukashuka kwa kasi kama ya uchumi
Kwa mikoa kama dar wataathirika nao manake wanafunzi sina uhakika kama watapewa vitambulisho wa shule ili wakapandie kwenye mabasi kwa gharama ya tsh. 200
Manake makonda mmmmmmm nao hawana dogo
Hii ni kwa sekondari tu msingi
Watashindwa kufanya majaribio ya kutosha kwa madarasa ya mtihani hasa darasa la 7
Mh. Naomba ungeruhusu ila kuwe na ukomo selikali bado haina uwezo wa kumuhudumia mwanafunzi hadi kukidhi mahitaji
Bado mzazi anajua uchungu na umuhimu wa elimu ila kwa wenye pesa watoto wao watasoma fedha na baobab sasa kwa wazazi wengi hiku kwetu uwezo huo hakuna ndo mana watoto wanarundikana darasa moja tena wengine wakikaa chini
Mawazir fanyeni kazi ya kushaur kama ilivyokatiba yetu
Najua watoto wa viongozi wengi hawapo shule za kata
Natafta namna ya kwenda ikulu
Sorry nina mwandiko mbaya lakini najua naweza kueleweka wazo langu
Tuseme ni nini sisi
Naomba kuwasilisha
Mods naomba msifute na naomba msiunganishe na uzi mwingine tafadhar wakuu