Shule nyingi za serikali hazina vyoo!!!

Kifaranga

Senior Member
Jan 6, 2011
144
31
Jamani kwa utafiti wangu niliofanya kwa haraka haraka na kwa kusikia toka kwa wadau mbalimbali ni kwamba vyoo vingi vya shule za serikali vimejaa, vinanuka na hakuna wa kusimamia na kurekebisha hali hiyo. Mfano dhahiri ni Tosamaganga iliyopo Iringa. Inakuwaje vyoo vimejaa na hakuna wa kurekebisha hali hiyo???? Damn it .... Siasa zimezidi bongo!!!!
 
sa si bora hko hta kuna vyoo shule nyingi za kata zina matundu manne hadu nane tu ya vyoo wakiambiwa kujenga halmashauri zinasema hazina hela, yani mazingira ktk shule za kata sio kabisa yaani hawa watoto wanafeli kwa mengi
 
Nini! Tosomaganga!!!!! Jamani, hata shimo la choo tunataka serikali ije ikachimbe!

Mimi nakumbuka wakati nasoma, walimu walikuwa waki-mobilise ku-empty pitlatrines, na kupeleka shambani kwa ajili ya bustani ya kabeji. Basi kama imebidi wanafunzi na walimu wao hawawezi kuondoa uchafu huo ili vyuo viweze kuendelea kutumika, kweli Shule inashindwa ku-mobilise fund raising ili wapate fedha kidogo ya kulipia magari ya kunyonya uchafu....HAO WALIMU WA TOSOMAGANGA WANAPASWA WAPIGWE VIBOKO KWA KUTOWAJIBIKA, NIMEKASIRIKA SANA
 
Kuna mkuu wa wilaya fulani Bukoba huko aliwachapa viboko walimu watu wakashadadia eti amekosea, hawa walimu wa kata na tosamaganga si wale wale wa kupigwa bakora?

Nafikiri tuwe fikira pevu, hata choo chako cha nyumbani utasema government ikusaidie? Uvivu wa watanzani ni kero kubwa sanaaaaa! watu hatuna fikra zaidi ya kuwazia ujinga.

Acha wafu wawazike wafu wenzao, siku mlipuko wa kipindupindu umekuja watajua cha kufanya at that time.
 
siku hizi tangia sekondari ziwe chini ya halmashauri huwezi fanya ujenzi wa jengo bila ruhusa ya halmashauri na kibali cha mhandisi, kuhusu fund raisings na michango bodi ya shule lazima ibariki na wazazi wakubali kuchanga, suala la wanafunzi ku empty pitlatrines kwa sasa ni gumu kwanza wao hawawezi kukubali na pili wazazi nyie wenyewe mnachangia mkisikia mtoto kaambiwa akazibue choo mnakuja juu na matusi huku mkisema mmelipa ada mtoto wenu apate huduma sasa unapowalaumu walimu unakosea saana, mfumo wa hizi shule zetu za sekondari umebadilika wakati ule zikiwa chini ya katibu mkuu wakuu wa shule walikuwa na maamuzi ya vitu ka hivyo sasa siasa imeingia saana hadi madiwani eti nao wanahoji competence ya mwalimu kweli hii ni sahihi. Kutokana na mwingiliano huu walimu pia nao wanabaki ka watazamaji tu, au na wao utakuta wanalalamika, ikiwa mkuu wa nchi anashangaa na kulalamika watu wa kada ya chini ka walimu wafanyaje???? Blame the system banaaa
 
Kuna mkuu wa wilaya fulani Bukoba huko aliwachapa viboko walimu watu wakashadadia eti amekosea, hawa walimu wa kata na tosamaganga si wale wale wa kupigwa bakora?Nafikiri tuwe fikira pevu, hata choo chako cha nyumbani utasema government ikusaidie? Uvivu wa watanzani ni kero kubwa sanaaaaa! watu hatuna fikra zaidi ya kuwazia ujinga.Acha wafu wawazike wafu wenzao, siku mlipuko wa kipindupindu umekuja watajua cha kufanya at that time.
Sasa mwalimu tu akurupuke na wanafunzi wake achimbe choo bila idhini ya halmashauri aone utasikia hapa ktk ramani tulitaka tujenge sijui maabara sijui nini? Na huwezi inua jengo bila kuruhusiwa na wakubwa mitoto menyewe ina kiburi inachopewa na mizazi yao, sasa mwalimu kwa nini apate pressure kuhangaika kwanza kwa mshahara gani anaolipwa eboooo!!!???
 
Back
Top Bottom