Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

Jamani mimi napenda kupingina na nyinyi wote,lkn nadhani mawazo yetu wote ni kwa ajiri ya kupata timu iliyo bora hata kama tutakua tukipingina hapa.

Cha kwanza nadhani kama wapenzi wa michezo lazima tuwe na subira hatuwezi kupata timu nzuri katika kipindi kichache kama tunavyotaka sisi.Hii ni kutokana na wachezaji wenyewe na hulka zao.
Wachezaji wengi wa kitanzania wanalewa sifa mapema sana,na wengi ni waongo waongo hawafatilii mafundisho na miiko ya mpira wenyewe.
Hapa tunaweza kumlaumu huyu kocha ila tatizo lipo kwa nguvu kazi yenyewe,nasema hivi sio kwa sababu nimesikia kwa mtu furani au ndivyo ninavyo dhani la hasha...,nasema kutokana mimi niko karibu na wengi ya ha wa wachezaji wetu.
Kocha anaweza kufundisha kwa uwezo wake wote lakini mafundisho yakawa hayazingatiwi na hawa wachezaji ikawa work done sawa na zero.
Kuna mchezaji mfano ya hao waongo waongo niliosema hapo juu,alicheza simba kwanza kwa majaribio akashindwa kufanya lolote kwenye mechi hizo ambapo matokeo yake akusajiriwa na Simba,akaendelea kucheza timu yake ya mtaani lkn dreams zake zilikua kucheza timiu ya Taifa na kweli akaja kucheza kweli timu hiyo tu kwasababu ya USANI... USANI...(kama rais wetu anavyo sema,ukitaka kupata uongozi unafanya fanya tu....) basi Ndg.yule Mchezaji akaja cheza National Time kama International Player kutoka huko alikotoka hata miezi sita hana na hiyo timu aliyo kua akicheza huko bara ulaya.Kaja lichofanya ni madudu tu,jana kakosa bao la wazi yeye na Lango tu.
Wengine kesho mechi mpaka saa tisa wana lewa na wanawake tu habari hawapati alafu hao ndio wanaopigiwa debe na magazeti nawalio wengi wasio jua system za maisha yao,wengi ya hao wanasema mpira ndio maisha yao lkn hawafati ile miko ya mchezo wenyewe.
Ukiwa na wachezaji wa aina hii watano tu kwenye kikosi basi hapo hamna kitu na tunaweza kufukuza kila kocha hata akija MOrinho nini Maximo.Ina husu kwanza hawa wachezaji wenyewe wajue wajibu wao(kitu ambacho watz hatuna)
Kuna mengi tu hapa ya kueleza kutokana na hii hari,na ili tupate maendeleo ya ukweli lazima tuwe wakweli kwa hatu ambazo timu imeziweka na lazima tuweze kuziweka wazi kama sifa ya Kocha.
Mfano mimi nimeona mpira wote wa jana na mengine iliyopita ukiondoa mechi mbili za mwanzo,timu kiwango kimeongezeka sana kuliko kipindi chochote cha mpira wa Tanzania kuanzia mwaka 1995.
Tulikua na makocha wazawa mfano wa Mziray yule wa Chuo kikuu,hakufanya lolote ukiniuliza mimi ambaye toka alipo pewa yanga Miaka ya nyuma nilkuwepo karibu kabisa mpaka kwenye vyuma vya wachezaji,kocha mzawa msomi na mshirikina wa hari ya juu.sipendi kusema mengi ila hii ni mifana michache sisi kama wapenda miche zo tunaweza kujadiri kutokea hapa
 
Tatizo ni lile lile tuliokuwa nalo toka siku za nyuma..hatuna timu ya Taifa ya Kudumu! kuna mantiki gani kuwapeleka wachezaji Brazil na Ulaya then unakuja kuwatema almost nusu yao...kwa hiyo kila mara tutaendelea kuwa na timu mpya ya taifa ambayo hata kama wachezaji ni wazuri kiasi gani si rahisi kufanza vyema given muda wanaokaa kambini ni mfupi
 
Tatizo ni lile lile tuliokuwa nalo toka siku za nyuma..hatuna timu ya Taifa ya Kudumu! kuna mantiki gani kuwapeleka wachezaji Brazil na Ulaya then unakuja kuwatema almost nusu yao...kwa hiyo kila mara tutaendelea kuwa na timu mpya ya taifa ambayo hata kama wachezaji ni wazuri kiasi gani si rahisi kufanza vyema given muda wanaokaa kambini ni mfupi

Mkuu mimi nadhani tuko pamoja,
Nini Mantiki ya hayo matendo ya kocha kkupeleka wachezaji brazilan ulaya na kuwaacha karibu nusu!
Ok,sitaki kumswemea kocha ila nadhani kwa mujibu ya nilicho sema hapo juu,"wengi ya hawa wachezaji hasa hawa wenye majina hawafati mafundisho na miiko ya mchezo wenyewe"
Sasa kocha anapo kuja kubaini yale yalionyuma ya matendo ya hawa wachezaji ona ona ni ubora kubakia na wachezaji wachache tena wasi na majina na wadogo kwani wana muda mwingi wa kucheza na kiumri mambo makubwa makubwa hawaja yaanza.
Lakini tusisahau kwamba hawa wachezaji wadogo Hii ndio ushiriki wao wa kwanza watakapo tua tena dimbani hawatakuwa wageni tena na matunda tuta yaona
 
Kila meneja lazima atoe results. Kocha lazima atoe results. Sasa Masimo kashindwa hayo. Kwa hiyo hakuna mswalia mtume. Aanze. Tatizo liko palepale. Tanzania hatuna utamaduni wa kuwajibika hivyo Masimo ataendelea kutumbua mpaka dakika ya mwisho. Ni nani atathubutu kumwambia afunge virago? No one. Team imeshindwa hivyo Koch AANZE.

Ingawa hicho ni kidonda. Tutafukuza Inzi Mpaka tuchoke! Mkakati ni wa wizara na wadau waote husika kupanda mbegu. timu za vijana,huwezi kuunda timu kutegemea vipaji tu. You need kuwatambua mapema na kuwaendeleza. Na sio Masimo tu hata hao viongozi wa FAT nao waanze.
 
Kila meneja lazima atoe results. Kocha lazima atoe results. Sasa Masimo kashindwa hayo. Kwa hiyo hakuna mswalia mtume. Aanze. Tatizo liko palepale. Tanzania hatuna utamaduni wa kuwajibika hivyo Masimo ataendelea kutumbua mpaka dakika ya mwisho. Ni nani atathubutu kumwambia afunge virago? No one. Team imeshindwa hivyo Koch AANZE.

Ingawa hicho ni kidonda. Tutafukuza Inzi Mpaka tuchoke! Mkakati ni wa wizara na wadau waote husika kupanda mbegu. timu za vijana,huwezi kuunda timu kutegemea vipaji tu. You need kuwatambua mapema na kuwaendeleza. Na sio Masimo tu hata hao viongozi wa FAT nao waanze.

Mkuu,
Kuna jamaa alisha wahi kuniambia,
"when somebody is mad,resoaning power drops"
Sasa Mkuu wewe na wapenzi kama sio Watanzania wengi wana asira na kocha na kufungwa kwa jana.
Sasa inabidi tutulize mzuka ili tujue wapi tumeangukia
 
Sio mzuka. Analipwa ili achague team nzuri, aifundishe mbinu za kisasa na tema ishinde. mtihani ni kushinda, ingekuwa ni mtihani wa kuandika kwenda form one basi ina maana kafeli. Je tangu awe kocha ameshiriki mashindano mangapi na ameshinda viokombe vingapi au hata tu kuwa runerup. Huoni haya majamaa ya Ukweni huku, kocha hashindishi team anaanza. Hiyo itsaidia whoever want the job awe makini sio kuokpta madafu yetu na kuanza. Sry labda ahalipwi madafu no Dollar nafikiri. Tukituliza mzuka tutakuwa na huruma na tutaanza kusikliza hadithi ndefu za alinacha.
 
Salaam, unajua mimi nikia nakua nilikuwa naambiwa kwamba soka ni magoli na kombe sio daraja... ukiwa daraja l 2 unapiga magoli na unapata kikombe then unaweza panda daraja.. sasa sisi Bongo bwana kwa kweli swala la magoli na vikombe Kilimanjaro Stars kidogo limekuwa gumu... Sawa FIFA inasema Soka la bongo limepanda kwa mara ya kwanza "Crap"; mimi kama mshabiki wa kawaida hilo ni sawa na kusema GDP ya bongo imepanda na wakati umaskini unaongozeka... Upo hapo!!?? haya mambo ya kuangalia mahesabu ya vitabuni halafu ku judge na kukubali kwamba kuna mafanikio wakati facts on ground zinaonyesha ukweli tofauti mimi sikubaliani nayo kabisa... Angalia club level, Yanga walikuwa na Micho na sasa ni Kondick (nadhani nimepatia majina) lakini kwenye ligi muongozaji nani, sio Yanga baba ake... Watani wetu pale Msimbazi wao ni Makocha raia lakini Wallahi jamaa wametufanya vibonde daima (past 2 years plus ni kasheshe mbaya na ndicho kipindi cha wadhungu hicho wajemeni).... sasa wengi watasema mbona Naigeria ipo powa na wazungu, Kameruni etc... sasa jiulize haya:
1. Lugha - una uhakika kiwango cha kuelewana nchi kama Naijeria na makocha wa kidhungu ni sawa na Bongo?? Kumbuka Maxima hata ung'eng'e shida - sign language mwanangu!!!
2. Kujua aina ya mpira wa vijana wetu... Kuna watu kama Kaseja (Mtani wa jadi lakini kijana anapiga jamani) hawapangiw, eti wafupi - Wallahi jamaa hajui ndio figure zetu Bongo hizo (mbona Thomas Hassler wa Germany alikuwa wa kutumaininwa sana tena nyuma sasa na ni kafupi kajamaa vibaya mno!!)
3. Kama angekuwa ni kocha mzalendo ("Mkwasa yupo cheki mafanikio Twiga pale - pokea Tano Bro Boni", Mzee Kibadeni, Julio.... wapo wengi) akapewa mchuzi wa maana unafikiri hataweza fanya maajabu?? Wewe angalia kocha yoyote mzalendo alikuwa anlipwa kiasi gani kufundisha Taifa Staaz, fananisha na micho - hapo point ni maslahi kaka!!
4. Ng'ombe hanenepi siku ya mnada... soka sio kwenye umri wa miaka 25 (Taifa wengi) soka ni utotoni.. Ndio tuna Tinocco (mepatia ee!?!?!?) lakini swali yeye na hao anda 17 wanaelewana lugha??

Ka hiyo to me Soka la Bongo limeshakuwa kama mashirika ya Umma, tuyabinafsishe (and not to Mzawa bali Mdhungu) hata kama jamaa hafanyi kitu lakini sifa tunazo kwamba tuna kocha/onwer mdhungu... Fifa kama walivyo World Bank watatupandisha level lakini bottom line mpira ni uleule wa kupigwa bao bila vikombe!!!!!!

Maximo aende zake tumpe mzalendo same pochi tuone kama Sauzi hatukutia timu babaake!!!!!
 
Sio mzuka. Analipwa ili achague team nzuri, aifundishe mbinu za kisasa na tema ishinde. mtihani ni kushinda, ingekuwa ni mtihani wa kuandika kwenda form one basi ina maana kafeli. Je tangu awe kocha ameshiriki mashindano mangapi na ameshinda viokombe vingapi au hata tu kuwa runerup. Huoni haya majamaa ya Ukweni huku, kocha hashindishi team anaanza. Hiyo itsaidia whoever want the job awe makini sio kuokpta madafu yetu na kuanza. Sry labda ahalipwi madafu no Dollar nafikiri. Tukituliza mzuka tutakuwa na huruma na tutaanza kusikliza hadithi ndefu za alinacha.


Duu...
Hii kazi kweli kweli.

Maarifa!

Ni kweli huko kwa wanaujua mpira kikweli kweli,kocha akivurunda ana anza,ila.. wasi wasi wangu sie huko hatuja fika huko hatuwe suck the coachers kama wafanyavyo just for the seek of firing them.
Wenzetu wana wachezaji proffesionals wanaojua wajibu wao na mpira na miiko yake wanaifata.sasa embu niamabie yule Bonaban anafata miiko kama sio mibangi,mipombe na mademu kucha kuchwa!?
Mie nasema facts kwa mtazamo wangu hatuna wawajibikaji kwenye nyanja zote tusiwalaumu makocha bure we huoni hata kubutua mipira sikuhizi wameacha kama umeona mechi ya jana DAKIKA 45 za kipindi cha pili tuko golini kwao tuna wahemea ila umaliziaji mbovu kwa kocha hawezi kuja kukusaidia kufunga.
Hivi unakumbuka wakati ule tulipokua na wachezaji kweli kweli akina Hamisi Thobias Gaga (GAGARINHO),Athumani China,Issa Athuman,Zamoyoni Mogera,Makumbi Juma kuwataja wachache tu hawa na wafahamu vizuri na walifata miiko ya uchezaji
 
SM, tunakubali hayo lakini ukumbuke kuwa kocha wa wakati ule ailelewa kipaji cha kila mchezaji na kumuacha ajitutumue awezavyo na yeye kazi yake ilikuwa kuwafanya waweze cheza kama timu au nimekosea??????? Sasa unajua timu kubwa za ulaya kama mfano unavyosema ni kwamba wao wanachezea klabu kubwa na kule ni mpira karibu sawa au more than timu ya taifa... sisi hapa Maximo ametoka Brazil - kule mpira ni carpet; sisi Bongo mambo yetu ni piga then kata mbuga - au nimekosea? Sasa hapo Maximo anaona sio soka inabidi awafundishe different soka kama la homu... Mbona WaJerumani wanacheza soka lao la wote mbele/wote nyuma na wanatesa tuuu??? Sasa jiulize timu ngapi kubwa za Taifa wana kocha wa Brazil?? Unajua why?? Mpira wa Brazil ni tofauti na timu karibu zote nje ya Americas!!
 
Mkuu Morani,
Mie nadhani tutafika tu hata kama mmekuwa wagumu kukubari makosa ni ya wachezaji wetu.
Alafu embu niambieni hivi hii ishu ya pochi la Maximo kuwa kubwa mmelipata wapi naona kila mtu toka kombe lkimeaanza ni kuungumza juu ya pochi hilo.
Mie mwenzenu naona hizo zote ni propaganda tu za hao makocha wote wa kienyeji (wazawa).
Haman hata mmoja kati ya hao ulio wataja ambaye haja pewa hiyo timu na wote wamefanya nini..? MADUDU matupu ukiomndoa Mziray ambaye ndio aliaanzisha hili sakata la kocha Maximo aliutoa CASTLE CUp kule mwanza sijui taifa sikuymbuki vizuri hapa,Lakini nakuaambia hanma kocha anaye amini Ushirikina kwenye soka kama Mziray,sijui na huu upo huko ulaya na kwenye vitabu?\\Kuhusu Mpira wa brazil kuwa tofauti na wengine duniani siwezi kusema sana,ila imani yangu ni kwamba ukiweza kufunga lazima ujue na kuburudisha maana after all mpira ni burudani.
Mechi ile tuliyo toa draw na burundi watoto walicheza samba sio ya kitoto tulishangilia mpaka dakika ya mwisho sasa sijui mnataka nini?
 
He should be given time, he can not make a good team in this short time.
Lets give him time
 
Wana JF, hebu tuangalie tulikotoka. Sasa hv tunaona serikali imewekeza nguvu kwenye michezo na tumeona tuna hata kauwanja ka kujivunia baada ya papaa Mkapa kufanza mambo. Huyu kocha nafikiri tatizo si yeye bali ni wafundishwaji ambao uwezo wao wa kufikiri ni mdogo. Kuna mambo ambayo si ya kocha. Kama kufikiria kwamba nimpigie mchezaji mwenzangu au adui. Utakuta mchezaji, mtu mzima kabisa mwenye ndevu, anampa adui pasi, wazi wazi. Sasa hapa kuna kumlaumu kocha..?? Ni kocha gani atafundisha kutoa pasi kwa adui..?? kama yupo, nafikiri TFF ingekuwa imeshamwajibisha au tungejua kuwa amepewa rushwa nene na timu pinzani. Pia, jiulize ni wangapi wanajua kiingereza kwenye timu ya taifa. Wewe mchezaji mmoja au wawili wapewe instructions then wao ndio wawape wenzao au kocha atumie vitendo kama bubu fulani, hapo unategemea nini kama sio miscommunication..?? Mi nafikiri hawa wachezaji waanze kupelekwa shule, wakajue hata 1+1 ili kuongeza reasoning yao wanapokuwa uwanjani (manake inaelekea akili zao zimejaa starehe na tamaa ya umaarufu), pia wapelekwe english course wajue namna ya ku-communicate.

Mkumbuke huyu jamaa alikuja na kukuta soka la bongo limejaa majungu na fitina, sasa kitendo cha yeye pia kutosikiliza majungu, msimpelekeshe. Tujiulize, kama jana tungepigwa 6-0, si ndio tungempakia hata kwenye meli ya mizigo arudi kwao..?? Hizo 2-1 ni matokeo ya kawaida kabisa. Tena tumejitahidi as tumebp goli la wapinzani (I mean timu pinzani, sio vyama vya upinzani ktk siasa).

Hapo,vipi, hapo ...............??.........sawa....!!!!!!
 
samahanini lakini ningependa nifahamishwe kama kuna mtu anafahamu mshahara na marupurupu ya huyu kocha!!na analipwa kupitia fungu gani as nijuavyo mie ni kuwa Raisi mwenyewe alisema atakua anamlipa so ki ukweli kweli yatakiwa raisi atoe kwenye mfuko wake mwenyewe which i cant bliv is what is being done sasa naomba nijulishwe mamilioni hayo yanatoka kwenye mfuko ganiii?
 
kwa wale wanaosema aendelee kubaki as apewe muda zaidi hivi mwajua kuwa if we wont make it kuwa angalau best washindi wa pili katika haya makundi ya 2010 ambapo tumo na cameroon we gonna stay out of football mpaka kugombania mataifa ya afrika 2012??kwa hiyo tukae tungoje tuu mpaka that tym???
if yeye ndo anahangaika na kutengeneza timu ya vijana wadogo alee vipaji kwa now which ndicho aliichofanya kwenye challenge cup then huyo mwenzake mwingine sijui Tinnoco alikuja nae kula pesa zetu kwa kazi gani??cz most of the tym wako pamoja hata sauzi kupanga ratiba walikua woote!yasemekana kwenye bonus za taifa stars iliposhinda tinnoco alipata fweza nyingi kuliko hata bushiri kocha msaidizi wa maximo mzalendo!sasa na hawa nao waanze A kupelekwa brazil.na kwingineko alafu wacheze mechi 2 3 watimuliwe tena nusu!!??lets b serious wajimini
 
samahanini lakini ningependa nifahamishwe kama kuna mtu anafahamu mshahara na marupurupu ya huyu kocha!!na analipwa kupitia fungu gani as nijuavyo mie ni kuwa Raisi mwenyewe alisema atakua anamlipa so ki ukweli kweli yatakiwa raisi atoe kwenye mfuko wake mwenyewe which i cant bliv is what is being done sasa naomba nijulishwe mamilioni hayo yanatoka kwenye mfuko ganiii?

Mshahara na marupurupu ya huyo kocha nadhani sio muhimu kwa sasa kwa sababu siamini kuwa makocha wazalendo walikuwa wanashindwa kwa sababu ya mshahara. Unataka kuniambia ndugu zetu wakina Kayuni, Mziray, Mkwasa, kibadeni nk wakipewa posho anayopewa Maximo tutaimba kidedea wakati wote. Nadhani utaratibu mzima uliharibiwa na serikali tokea walipofuta michezo mashuleni, angalia mafanikio yaliyokuwepo miaka ya mwisho ya sabini kutokana na Umishunta,Umiseta etc. Hivi kweli inaingia akilini kwamba watoto hawatengewi mafungu kwa ajili ya michezo badala yake wazee ambao hata magoti hayakunjiki wanakwenda kucheza?(in the name of SHIMIWI.) Nionavyo mimi nadhani lile fungu la shimiwi lingepelekwa mashuleni kujenga vijana halafu tuanze kutoa lawama kwa MAXIMO nina imani posho yake si kubwa sana ukilinganisha na zile zinazotupwa kwenye SHIMIWI.
 
Mshangaaji, hapo umenena... Kwa kumalizia ni kwamba kwa vile msingi umeshakatwa huyo Maximo kuwepo kwake ni kujaribu kuwakunja samaki tayari wameshakauka - ambapo ni viwili wabaki walivyo au uwavunje, PERIOD...

Kwa mantiki hiyo kuliko kumlipa Maximo (whatever he get as an individual) kwa nini pesa hizo zisiwekezwe kwenye mashule mfano kununua mipira, ku "Train" na kuajiri walimu wa michezo, kurudisha kipindi zamani tulikuwa tunaita "PE" sidhani kipo hiki kule shule za msingi.... Then tuweke mikakati ya kwamba miaka 10 ijayo lazima tuwe mahali flani....

Kinachontia uchungu ni kwamba Muungwana alituahidi kwamba lazima tutakwenda Ghana, na sasa Ghana ni hadithi.... (hii niite short-sightedness au??)
 
sawa sio kubwa ni kiasi gani???ukumbuke huyo ni kocha wa kimataifa so kwa asilimia kubwa anacheza na tu milioni kadhaaa on top of that lazma pa kulala n other stuffs analipiwa wewe usemae sio kubwa hebu jiulize ni watanzania wangapi wanaweza benefit with that??kwa nini zisiwekezwe hizo kwenye kujenga vituo vya kukuza vipaji??which is the most important thing??
 
n ABT MTALII Kahidi kuwa safari ya ghana lazma iwepo sijawahi hata msikia aki comment on it after ku luz!!!as ni mojawapo ya ahadi zake nyingii alizotoa ambazo hazitimizwi!ahadi ni deni atii
 
Nafikiri huyo Maximo angekubali kusikiliza ushauri wa wengine wakati anapochagua wachezaji na sio kusikiliza majungu
 
Back
Top Bottom