Shost! Nani kakwambia Bwana anawekwa hapo?

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Salaams!

Wapendwa, mmewahi kusikia majigambo ya mashost juu ya kuwateka kiakili/kimapenzi bwana zao wakionesha kiganja na kudai wamewaka hapo kumaanisha jamaa zao hawana ujanja na hawafurukuti?

Nimekuwa nachekeshwa sana na kauli za aina hii maana nijuavyo mimi mwanaume kumkubalia mambo mengi partner wake si lazima itokane na kupagawishwa saana kimapenzi au kiujeuri na mwandani huyo. Wakati mwingine jamaa anakuwa anamwonea huruma kutokana na pengine hali yake duni kimaisha, marketability (hauziki/havutii), historical background nk. lakini kabla ya kuchunguza vijimambo hivi demu hudhania yeye ni special saaaaana na kwamba ndiyo maana anapewa kila anachokitaka.

Mashost tujuzeni kaka zenu, nani huwarubuni nyie kiasi cha kuamini mmewaweka bwana zenu viganjani na hawafurukuti? Siku ukigundua mdogo wako tumbo moja ana mimba ya mshikaji utafuta vipi kauli?
 
Kwa nini? Mbona kiumri naelekea 50yrs Inawezekana sijawahi kuwa na mpenzi kwa maana unayokusudia lakini nimewahi kupendana na akina dada kadhaa kabla katika maisha yangu. Kwa sasa nimestaafu na kutulia sehemu moja. I had 1mdada niliyemtosa baada ya kumsikia akidai ameniweka kiganjani wakati lengo langu ilikuwa kumpunguzi machungu ya Boyfriend aliyekuwa naye kabla yangu kwani alikuwa anasononeka na kwa kujua bado anamfeel sana jamaa yake nikawa najitahidi kumjali kwa kila namna ili asijihisi makapi.

Imeelekea wewe bado ni mdogo na hujawahi kuwa na mpenzi.
 
Wacha kashfa wewe, mbona wewe alikuvutia mpaka ukamfuata? Sasa unasema ulimuonea huruma, jamani wanaume, hata siku moja mapenzi hayahitaji huruma, huruma ipo kivyake hukooooooooooo na mapenzi yapo kivyake. Uwezi kuwa na mtu haujampenda/kuvutiwa nae, halafu huseme upo nae tu kwa sababu unamwonea huruma kivipi.
 
Unaniudhi, kwa maana ingine hata wewe huuziki, la sivyo usingekaa na mtu asiye uzika. Acha dharau zako.
 
mijanaume ya aina yako ndo inatakiwa igeuzwe nyoka kabisa nini kuwekwa kiganjani
 
Duh! Wewe ni baba huruma hadi uwe na mpenzi kisa unamuonea huruma. Utaonea wangapi huruma kwa mwendo huo.
 
Kwa nini? Mbona kiumri naelekea 50yrs Inawezekana sijawahi kuwa na mpenzi kwa maana unayokusudia lakini nimewahi kupendana na akina dada kadhaa kabla katika maisha yangu. Kwa sasa nimestaafu na kutulia sehemu moja. I had 1mdada niliyemtosa baada ya kumsikia akidai ameniweka kiganjani wakati lengo langu ilikuwa kumpunguzi machungu ya Boyfriend aliyekuwa naye kabla yangu kwani alikuwa anasononeka na kwa kujua bado anamfeel sana jamaa yake nikawa najitahidi kumjali kwa kila namna ili asijihisi makapi.

Sidhani kama ulikwenda kwa huyo mdada kihuruma, lengo lako lilikuwa moja labda la kujiridhisha mwenyewe na siyo kuwa na uhusiano wa kudumu.

Si unaona umempata mmoja ambaye umempenda na yeye ndiye huyo aliyekuweka kiganjani hata kama hajisifu mbele ya watu. Kwa maana kwamba ulichukuwa hatua ya kwenda naye kanisani/msikitini mukafunga ndoa, na huwa munajadiliana kwa mambo tafauti.
 
The analists umenikumbusha hiyo mie pia huwa nachukia mtu akisema amemuweka kiganjani mpenzi wake hayo mengine ya kumuonea huruma coz hauziki sina hakika nayo kabisa
 
Safina my dear,
Point yangu hapo si kuanzisha uhusiano bali ile care (kujaliwa/kuthaminiwa/kudekezwa/kupewa kila atakacho nk.) wakiwa ndani ya uhusiano tayari. Please rudia kuisoma topic. Sikusudii bwana kumtongoza bibi kwa kumwonea huruma isipokuwa ile kumjali zaidi wakati tayari wapo pamoja kimahusiano.

Wacha kashfa wewe, mbona wewe alikuvutia mpaka ukamfuata? Sasa unasema ulimuonea huruma, jamani wanaume, hata siku moja mapenzi hayahitaji huruma, huruma ipo kivyake hukooooooooooo na mapenzi yapo kivyake. Uwezi kuwa na mtu haujampenda/kuvutiwa nae, halafu huseme upo nae tu kwa sababu unamwonea huruma kivipi.
 
Shantel, zungumza na wakaka wakwambie ni kwa nini wanakuwa na wanawake nje ya uhusiano wao rasmi lakini bado wanakuwa wapole na wanyenyekevu sana wanaporejea kwenye uhusiano wao rasmi (ndoa au partnership). Utakutana na sababu kibao na huruma ni mojawapo. Wanataka hawa wanaodhulumiwa wajisikie wanapendwa sana kuwaepusha na machungu. Nakwambia wanawake wanaamini vitu kibao sana juu ya wanaume lakini kwa uchunguzi wangu nimegundua hawajawachunguza kiasi cha kutosha na ndiyo maana mmoja atadai kamweka kiganjani wakati mshikaji anaruka pengine na shoga yake wa karibu kabisa.
Mtu aliyewekwa kiganjani anaweza vipi kumwibia mwenye kiganja penzi lake tena chini ya pua yake?

The analists umenikumbusha hiyo mie pia huwa nachukia mtu akisema amemuweka kiganjani mpenzi wake hayo mengine ya kumuonea huruma coz hauziki sina hakika nayo kabisa
 
Ni kweli inawezekana hata mimi siuziki ndiyo maana hutasikia nasema nimemweka mtu kiganjani mwangu. Kwa nini watu hawataki kufanya uchunguzi kujua kama nisemayo yapo au la? Angalia mfano huu; Nimetamani kupass time na mdada pasipo kujua kaolewa, ana mchuma au la. Inaweza kutokea akakubali lakini akadai yeye ana jamaa yake. Mie namwambia sisi watu wazima hakuna hofu. Akinogewa na mambo yangu ataniuliza kama nampenda kweli au namchezea tu. Endapo nitakuwa nahitaji mambo yake bado nitamwambia nampenda. Wengi wanapoambiwa hivi hujikuta wanapenda na huenda hata wakavuruga uhusiano wao wa awali. Ikitokea akavunja uhusiano wake wa awali na kukwambia "unajua nimwemwacha X kwa sababu ya kukupenda wewe?.....Ukiniacha ntakufa kwa mawazo.....nakuona kama umezaliwa kwa ajili yangu......"nk. Katika mazingira kama haya unaweza kumkuta mshikaji anajifanya kujali kweli wakati yeye mwenyewe anatamani kumkimbia demu kwa kuhofia tabia. Kwa ufupi nakuomba uchunguze.

Unaniudhi, kwa maana ingine hata wewe huuziki, la sivyo usingekaa na mtu asiye uzika. Acha dharau zako.
 
mijanaume ya aina yako ndo inatakiwa igeuzwe nyoka kabisa nini kuwekwa kiganjani
Una balaa wewe, si bora awe chura maana hatang'ata. Hapo tu ashakung'ata akiwa nyoka si atakuua kabisa? Halafu awe nyoka na siku hizi si umesikia nyoka wanavua magamba? yaani nyoka akivua gamba ina maana sumu inakuwa kali kuliko ile ya awali.
 
Halafu huo usemi ingekuwa sisi ungesikia "Unatudhalilisha kijinsia" Hata bungeni ungefika
 
Back
Top Bottom