Shirikisho la mpira Africa (CAF) limeizawadia Simba sc tuzo ya Mashabiki Bora katika michuano ya African football league

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,727
AFRIKA KUSINI: SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewazawadia mashabiki wa timu ya Simba tuzo ya mashabiki bora wa michuano ya AFL.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Muhene 'Try Again' nchini Afrika Kusini kushudia fainali ya AFL.

Baada ya kupokea tuzo hiyo kiongozi huyo ametuma salamu za pongezi kwa wanasimba.

"Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu." Amesema kiongozi huyo.

MAONI YANGU: Mashabiki hawajaiangusha timu Bali timu inawaangusha mashabiki.

======

Mashindano ya AFL yalianza 20,10,2023 ikiwa ni mashindano mapya kabisa yaliyohusisha timu 8, ambapo Simba sports club ya Tanzania, ilipewa fursa ya kuwa mwenyeji wa sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo na kupigwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly, ambapo kwa mechi mbili walitoka suluhu ya 2-2( Soma zaidi)na 1-1(Soma zaidi )na goli la ugenini kuwaondoa Simba kwa hatua ya awali ya robo fainali.

Mashindano hayo kwa msimu huu yamefikia tamati leo 12, 11,2023 kwa kuzikutanisha timu 2 zilizofanikiwa kufika fainali za Widad casablanka na Mamelodi Sandawons ambapo Mamelod ameibuka mshindi na kubeba ubungwa kwa mara ya kwanza. (Soma zaidi)

Katika tuzo zilitolewa na Simba imepata tuzo ya mashabiki bora baada ya kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa AFL kweye uwaja wa Benjamii Mkapa.

1699809068405.jpeg

Screenshot 2023-11-12 at 19-33-03 Home _ X.png

AFRIKA KUSINI: SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewazawadia mashabiki wa timu ya Simba tuzo ya mashabiki bora wa michuano ya AFL.
-
Tuzo hiyo imepokelewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Salim Muhene 'Try Again' nchini Afrika Kusini kushudia fainali ya AFL.
-
Baada ya kupokea tuzo hiyo kiongozi huyo ametuma salamu za pongezi kwa wanasimba.
-
"Tuzo hii ni kwa kila shabiki wa Simba. Kuja kwenu uwanjani kushangilia timu yenu kumeiwezesha timu yetu kushinda Tuzo ya Mashabiki Bora wa AFL. Pongezi nyingi kwenu." Amesema kiongozi huyo.

MAONI YANGU: Mashabiki hawajaiangusha timu Bali timu inawaangusha mashabiki.
Naunga mkono hoja

Timu imefeli sana
 
#AFRIKAKUSINI: MASHABIKI WA SIMBA WAPATA TUZO YA MASHABIKI BORA #AFL   

Klabu ya @SimbaSCTanzania imefanikiwa kupata tuzo ya kuwa na mashabiki bora katika mashindano ya African Football League (#AFL   ) na Tuzo hiyo imechukuliwa na Mwenyekiti wa Bodi, Salim Muhene (Try Again).

20231112_192346.jpg
======
Mashindano ya AFL yalianza 20,10,2023 ikiwa ni mashindano mapya kabisa yaliyohusisha timu 8, ambapo Simba sports club ya Tanzania, ilipewa fursa ya kuwa mwenyeji wa sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo na kupigwa mechi ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly, ambapo kwa mechi mbili walitoka suluhu ya 2-2( Soma zaidi)na 1-1(Soma zaidi )na goli la ugenini kuwaondoa Simba kwa hatua ya awali ya robo fainali.

Mashindano hayo kwa msimu huu yamefikia tamati leo 12, 11,2023 kwa kuzikutanisha timu 2 zilizofanikiwa kufika fainali za Widad casablanka na Mamelodi Sandawons ambapo Mamelod ameibuka mshindi na kubeba ubungwa kwa mara ya kwanza. (Soma zaidi)

Katika tuzo zilitolewa na Simba imepata tuzo ya mashabiki bora baada ya kujitokeza kwa wingi siku ya ufunguzi wa AFL kweye uwaja wa Benjamii Mkapa.

Screenshot 2023-11-12 at 19-33-03 Home _ X.png

Attachments

  • 1699808865786.jpeg
    1699808865786.jpeg
    136.8 KB · Views: 6
Safi sana simba fans, ujumbe umefika kwa wengine kuwa tanzania sio ya mchezo mchezo katika shangwe uwanjani.
 
Back
Top Bottom