Shirika la Wakimbizi Duniani lapingana na Tanzania, lasema Burundi si salama kwa wakimbizi kurudi

Mkuu, biashara ya wakimbizi ni biashara kubwa sana duniani.
Wakati wakimbizi wa Burundi wanaingia Kigoma (Kibondo) kwa mara ya pili, ndo niliona hii biashara ilivyo. Ntakupa mfano kidogo.
Ili kufungua kambi, mashirika huwa yanagana/kupeana majukumu kulingana na uwezo wa na rasilimali zilizopo katika shirika husika. Sasa, kuna mashirika (Danish Refugee Council - DRC, Norwegian Refugee Council - NRC, Medicine Sans Fronteers - MSF, na International Red-Cross Society). yalikuwa yanagombania kuendesha sekta ya afya. UNHCR wakatoa condition kuwa shirika linalotaka kuchukua jukumu la kutoa huduma hiyo, basi waoneshe uwezo. Hauwezi amini, kuna shirika moja kati ya hayo, walitua ndege ya mizigo ikiwa na tani 400 za dawa na vifaa tiba.
Kwa sasa mgawanyo wa shughuli zao uko hivi:
NRC - Afya
DRC - camp management na elimu
GtZ - logistics and trucks/car maintanance
Oxfarm - housing and environment
Japan - supply ya magari. hapa imagine kila shirika linaweza kupata magari 15 - 20
Shida iko wapi apo mkuu?
 
Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR linaziomba serikali za Tanzania na Burundi kutowarudisha kwa lazima wakimbizi wa Burundi waliohifadhiwa Tanzania, linaripoti shirika la AP.

Katika taarifa yake, shirika hilo linaeleza licha ya kwamba usalama umeimarishwa Burundi tangu kuzuka ghasia kufuatia uchaguzi mkuu mnamo 2015 " hali hairuhusu kushinikiza wakimbizi warudi Burundi".

"Tunatoa wito kwa uwajibikaji wa serikali ya Tanzania na Burundi kutii majukumu ya kimataifa na kuhakikisha kwamba wakimbizi wowote wanaorudi, ni kwa hiari kwa mujibu wa makubaliano ya pande tatu yaliosainiwa Machi 2018." AP limeinukuu taarifa hiyo ya UNHCR.

"UNHCR linaomba mataifa kuhakikisha kwamba hakuna mkimbizi anarudishwa Burundi kwa kushurutishwa na kwamba hatua zinachukuliwa kuifanya hali kuwa bora zaidi Burundi kuweza kuwapokea wakimbizi wanoarudi, ikiwemo kujenga imani na miradi kwa wanaoamua kurudi nyumbani."

Serikali ya Tanzania imeeleza kwamba imefikia makubaliano na Burundi kuwarudisha wakimbizi makwao, na kusema kuwa hali ya kiusalama katika taifa hilo sasa imeimarika.

Kwa muda mrefu serikali ya Burundi imesisistiza kwamba taifa hilo li salama kwa raia wote wa Burundi kurudi nyumbani.

Kwa nini Tanzania inawakataa wakimbizi wa Burundi?
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola ametangaza kuwa wakimbizi 2,000 watarudishwa Burundi kufikia October mosi.

''Azimio la msingi lilikuwa kila wiki wakimbizi lazima wakimbizi elfu mbili wawe wanarejeshwa nchini Burundi lakini tulipokutana na Mamlaka ya Burundi tuligundua kuwa UNHCR ndio wamekuwa wakikwepa jukumu hilo likisema Burundi haina uwezo wakuwapokea wakimbizi 2000 kwa wiki'' Waziri Lugola aliiambia BBC katika mahojiano ya kipekee.

Aliongeza kuwa serikali ya Burundi kupitia waziri wao wa mambo ya nje Pascal Barandagie waliwasilisha ombi lao kwa Tanzania kuelezea kutoridhishwa kwao na utekelezajiwa makubaliano waliofikia hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili na shirilka la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Bw. Lugola anadai kuwa shirika hilo la wakimbizi lina ajenda ya siri kwasababu linaleta kisingizio ambacho sio cha kweli.

Mbali na maelezo iliyopata kutoka wizara ya Mambo ya nje ya Burundi kwamba nchi hiyo ni salama wazirri Lugola anasema kuwa imeridhisha kuwa wakimbizi hao watakuwa salama wakirudi makwao kwa sababu tangu mwaka 2015 hakuna hata mkimbizi mmoja aliyeingia nchini humo kutoka Burundi kwa kuhofia usalama.

Mvutano kati ya shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa mataifa na serikali ya Tanzania kuhusu suala la kuwaregesha makwao wakimbizi wa Burundi umekuwa ukiendelea kwa miaka kadhaa sasa.

Mwezi Agosti mwaka mwaka 2017, Serikali ya Tanzania ililipatia shirika la UNHCR siku saba kuanza kuwarudisha wakimbizi wa Burundi ambao wanataka kurudi kwao kwa hiari, ama sivyo serikali ifanye zoezi hilo yenyewe.

Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Lugola alisema mtu atakaye sema burudi si salama atakutana na mkono/nguvu ya rais. Sasa sijui hili atalichukuliaje.
 
Mimi nimewah kuongea Na wakimbiz wenyewe, wanadai hivi. Burund hamba vita ila vita IPO kwa MTU Na MTU, wale hawana undugu kumbuka, ulikuwa umejenga mfano ukakimbia vita, then ukarudishwa Nyumba labda Na mengine ubakuta wanamiliki wngine imagine utafanya nin?bado vita vipo sana tu. But mambo hayatangazwi, Na naturecya most ya warund vijana waliopo makambini ni walikuwa askari Wa. Kundi la waasi, so wanatambulishika ukifika tu unakufa. Mfano multi alionfoka within 5 days akakatwa mapanga
 
Mimi nimewah kuongea Na wakimbiz wenyewe, wanadai hivi. Burund hamba vita ila vita IPO kwa MTU Na MTU, wale hawana undugu kumbuka, ulikuwa umejenga mfano ukakimbia vita, then ukarudishwa Nyumba labda Na mengine ubakuta wanamiliki wngine imagine utafanya nin?bado vita vipo sana tu. But mambo hayatangazwi, Na naturecya most ya warund vijana waliopo makambini ni walikuwa askari Wa. Kundi la waasi, so wanatambulishika ukifika tu unakufa. Mfano multi alionfoka within 5 days akakatwa mapanga
Kisheria mkimbizi akiwa kwenye hali hiyo inabidi apelekwe nchi ya tatu... mbona un hawawapeleki ?? .. unajua kazi ya shirika la IOM ?? Hiyo ndio moja ya kazi zake .. usiwe unaongea usivyojua..


Halafu warundi bado hawajawa na hadhi ya kuwa wakimbizi " Refugees" bali ni " Slam Seekers".. Sijui kama unajua kutofaitisha hayo maneno mawili.
 
Kisheria mkimbizi akiwa kwenye hali hiyo inabidi apelekwe nchi ya tatu... mbona un hawawapeleki ?? .. unajua kazi ya shirika la IOM ?? Hiyo ndio moja ya kazi zake .. usiwe unaongea usivyojua..


Halafu warundi bado hawajawa na hadhi ya kuwa wakimbizi " Refugees" bali ni " Slam Seekers".. Sijui kama unajua kutofaitisha hayo maneno mawili.
Sheria IPI unayozungumzia?
 
Sheria IPI unayozungumzia?
Sheria ya Tanzania ya mkimbizi ya mwaka 1998.


Screenshot_2019-08-30-07-03-15.jpg
 
UN ipo kimkakati mishahara minono pia mazingira ta kula bats safari business class dunia nzima
 
Asante sana kwa nakala hii. Una ile Tripartite agreement ya March 2018 ya kati ya serikali za Burundi, Tanzania na UNHCR? Voluntary repatriation ndio core ya makubaliano hayo lakin ndo vile tena hapo Jerusalemu
Mkuu Zote hizo ninazo , nikukumbushe kawaulize watu wazima wakimbizi wa Rwanda walirudishwa vipi na mkapa kutoka kambi ya Ngara, kagera. Watu walitembezwa kwa miguu kutokea ngara mpaka Mpakani rusumo..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom