Shirika la ujasusi la Marekani CIA laipaisha Tanzania kwa kueleza madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania pekee

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,272
9,716
Ndugu zangu Watanzania,

Habari njema ni kuwa shirika la ujasusi la Marekani CIA(central intelligence Agency) pamoja na habari zingine kupitia mtandao wake wa INSTAGRAM limeweka picha na muonekano wa madini ya Tanzanite na kueleza kuwa madini hayo yanapatikana mererani tu Tanzania, na likaelezea sifa ya madini hayo ki rangi na namna yanavyoonekana,pia likagusia ukaribu wake kutoka mlima Kilimanjaro mpaka yalipo na kupatikana.

Nini maana ya taarifa hii na umuhimu wake na faida yake kama Taifa na namna Tanzania inavyoweza kuitumia taarifa hiyo kujipaisha kiutalii ,kibiashara na kiuwekezaji?

Kwanza shirika hili kubwa kabisa ulimwenguni na lenye heshima kubwa na linaloheshimika limeiambia na kuipelekea Taarifa Dunia nzima kuwa Madini ya Tanzanite pamoja na mlima Kilimanjaro vinapatikana Tanzania tu na siyo mahali pengine popote wala nchi nyingine yoyote. Hivyo limepeleka ujumbe kwa watalii wote na makampuni yote ya kitalii Duniani kwote yajuwe ukweli huo na yasibabaike kwenda nchi nyingine kutafuta vitu hivyo.

Lakini pia shirika hilo limepeleka ujumbe Duniani kwote kuwa ukiyaona madini ya Tanzanite mahali popote pale Duniani yameingia kinyemela basi ujuwe kuwa yametokea Tanzania kwa njia ya panya na yanapaswa kurejeshwa kwenye ardhi ya Tanzania ili kuinufaisha Tanzania kimapato.lakini pia imepeleka ujumbe kuwa Tanzania ndio yenye kustahili kunufaika kwanza na madini hayo.

Lakini pia shirika hili la kijasusi limetusaidia kuutangazia ulimwengu na Dunia nzima kwa ujumla wake kuwa mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na siyo nchi jirani ,na kwamba watalii kutoka maeneo mbalimbali Duniani wakitaka kuuona na kuufaidi mlima Kilimanjaro basi hawana budi kukata tiketi za kuja moja kwa moja mpaka Tanzania.

Lakini pia limetupatia ulinzi wa kipekee na hati miliki ,kwa kuwa kila mtu akiyaona madini ya Tanzanite mahali popote pale Duniani atajuwa yanapatikana Tanzania na hivyo yametokea huko , lakini pia watalii watajuwa mlima Kilimanjaro upo na kupatikana Tanzania tu.

Watanzania tuna kila sababu ya kulishukuru shirika hili la kijasusi kwa kututangazia mambo hayo muhimu kabisa buree kabisaa.nimeona wameweka na taarifa ya Rais wao wa 41 hayati Bush ambaye alikuwa mkurugenzi wake aliyependwa sana na ambaye ni baba yake mzazi George Bush mtangulizi wa Rais Barack Husseni Obama.

Ni fahari kwetu watanzania na tunastahili kuendelea kudumisha ushirikiano na Marekani katika kuhakikisha kuwa tunapata wawekezaji na watalii katika maeneo mbalimbali.tuendelee kutangaza vivutio vyetu na Taifa letu

habari hiyo ni mwiba mkali na dawa chungu sana kwa majirani zetu ambao wamekuwa msitari wa mbele kupotosha habari na kutumia vivutio vyetu kujitangaza kuwa vinapatikana kwao.

Wizara zinazohusika na mambo haya ni wajibu wenu kuitumia taarifa hiyo kujipigia promo zaid Maana Dunia ya sasa haihitaji kuzubaa kama mgonjwa wa muda mrefu.kuweni shapu kwa kila kitu katika kunyaka fursa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Habari njema ni kuwa shirika la ujasusi la Marekani CIA(central intelligence Agency) pamoja na habari zingine kupitia mtandao wake wa INSTAGRAM limeweka picha na muonekano wa madini ya Tanzanite na kueleza kuwa madini hayo yanapatikana mererani tu Tanzania, na likaelezea sifa ya madini hayo ki rangi na namna yanavyoonekana,pia likagusia ukaribu wake kutoka mlima Kilimanjaro mpaka yalipo na kupatikana.

Nini maana ya taarifa hii na umuhimu wake na faida yake kama Taifa na namna Tanzania inavyoweza kuitumia taarifa hiyo kujipaisha kiutalii ,kibiashara na kiuwekezaji?

Kwanza shirika hili kubwa kabisa ulimwenguni na lenye heshima kubwa na linaloheshimika limeiambia na kuipelekea Taarifa Dunia nzima kuwa Madini ya Tanzanite pamoja na mlima Kilimanjaro vinapatikana Tanzania tu na siyo mahali pengine popote wala nchi nyingine yoyote. Hivyo limepeleka ujumbe kwa watalii wote na makampuni yote ya kitalii Duniani kwote yajuwe ukweli huo na yasibabaike kwenda nchi nyingine kutafuta vitu hivyo.

Lakini pia shirika hilo limepeleka ujumbe Duniani kwote kuwa ukiyaona madini ya Tanzanite mahali popote pale Duniani yameingia kinyemela basi ujuwe kuwa yametokea Tanzania kwa njia ya panya na yanapaswa kurejeshwa kwenye ardhi ya Tanzania ili kuinufaisha Tanzania kimapato.lakini pia imepeleka ujumbe kuwa Tanzania ndio yenye kustahili kunufaika kwanza na madini hayo.

Lakini pia shirika hili la kijasusi limetusaidia kuutangazia ulimwengu na Dunia nzima kwa ujumla wake kuwa mlima Kilimanjaro unapatikana Tanzania na siyo nchi jirani ,na kwamba watalii kutoka maeneo mbalimbali Duniani wakitaka kuuona na kuufaidi mlima Kilimanjaro basi hawana budi kukata tiketi za kuja moja kwa moja mpaka Tanzania.

Lakini pia limetupatia ulinzi wa kipekee na hati miliki ,kwa kuwa kila mtu akiyaona madini ya Tanzanite mahali popote pale Duniani atajuwa yanapatikana Tanzania na hivyo yametokea huko ,laini pia watalii watajuwa mlima Kilimanjaro upo Tanzania tu.

Watanzania tuna kila sababu ya kulishukuru shirika hili la kijasusi kwa kututangazia mambo hayo muhimu kabisa buree kabisaa.nimeona wameweka na taarifa ya Rais wao wa 41 hayati Bush ambaye alikuwa mkurugenzi wake aliyependa ambaye baba yake na George Bush mtangulizi wa Rais Barack Husseni Obama.

Ni fahari kwetu watanzania na tunastahili kuendelea kudumisha ushirikiano na Marekani katika kuhakikisha kuwa tunapata wawekezaji na watalii katika maeneo mbalimbali.tuendelee kutangaza vivutio vyetu na Taifa letu

habari hiyo ni mwiba mkali na dawa chungu sana kwa majirani zetu ambao wamekuwa msitari wa mbele kupotosha bahari na kutumia vivutio vyetu kujitangaza kuwa vinapatikana kwao.

Wizara zinazohusika na mambo haya ni wajibu wenu kuitumia taarifa hiyo kujipigia promo zaid Maana Dunia ya sasa haihitaji kuzubaa kama mgonjwa wa muda mrefu.kuweni shapu kwa kila kitu.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
So what????
 
Kwani Tanzanite (hapo nadhani hint ipo kwenye jina) wewe unadhani inapatikana wapi ?!!!!; Ni sawasawa useme Kwa mwalimu wako au jamaa mtaani amekusifia kwa kukuita kwa jina lako ?!!!

Nadhani ifike wakati kila mtu kwa wakati wake kufanya vitu vyenye tija (unless hii ni part time job au ni hobbie); lakini ungesaidia zaidi kama ungekuwa na constructive criticism kwa hawa walamba asali (as many things are going haywire)
 
Back
Top Bottom