Shinyanga: Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoani Shinyanga unaenda kwa kasi

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,620
3,936
Katika pitapita zangu Mkoa wa Shinyanga nimefika kushuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla mradi unaenda kwa kasi ingawa baada ya kufanya mahojiano na wakazi wa maeneo hayo ya mradi wamesema mradi ulikaa siku nyingi tangu serikali ya awamu ya nne ndiyo hospitali hiyo ilianza kujengwa baadae kutelekezwa.

Kiujumla mradi kwa sasa unakaribia kukamilika na mafundi wapo eneo la mradi wanaendelea na kazi hata hivyo kwa taarifa zilizopo mkuu wa wilaya alitangazia umma kuwa mradi huo utakamilika mwezi July.

Aidha hizi ni baadhi ya picha za majengo ya hospitali hiyo.

20220519_154026.jpg
 
Katika pitapita zangu Mkoa wa Shinyanga nimefika kushuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla mradi unaenda kwa kasi ingawa baada ya kufanya mahojiano na wakazi wa maeneo hayo ya mradi wamesema mradi ulikaa siku nyingi tangu serikali ya awamu ya nne ndiyo hospitali hiyo ilianza kujengwa baadae kutelekezwa...
Ina.maana awamu ya tano ilitelekezwa na Sasa inajengwa kwa Kasi. Wale wa legacy mnakaribishwa kusema na hii ni legacy Sasa sijui inajijenga Kama uyoga
 
Samahani, hivi ile ya chatial ishaishaga?
Ile ishakamilika kwa asilimia kubwa sana na baadhi ya majengo walishaanza kuyatumia imebaki finals na Rais mwenyewe amewaambia ataenda kuifungua Yani kwamba akifungua awe amemalizana nao wasilete kidomodomo
 
Ukiwa mgeni sehemu ebu ulizia wenyeji na kupata taarifa sahihi ndipo ulete jukwaani siyo habari inayoeleaelea. Ujasema ni majengo gani yanajengwa.

Ninachojua ni kuwa Hospitali ya Rufaa ikianza kujengwa mwaka 2014 kwa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) ya ghorofa moja huko Mwawaza Kama nimepatia jina.

Tokea kipindi hicho Hadi Leo hakuna kikichoendelea mpaka Sasa, miaka yote ya utawala wa Hayati Magufuli Kuna ujenzi wa Hosp mbalimbali zimeendelea kwenye mikoa Kama Mara, Simiyu, Geita,Mtwara, Kilimanjaro,Arusha, Mwanza isipokua Shinyanga....
Waombe watu wa Shinyanga radhi kwa kupotosha kuwa ujenzi wa hiyo Hosp inaenda Kasi.
Hiyo siifahamu siwezi jibu kitu ambacho sikifahamu.
 
Katika pitapita zangu Mkoa wa Shinyanga nimefika kushuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla mradi unaenda kwa kasi ingawa baada ya kufanya mahojiano na wakazi wa maeneo hayo ya mradi wamesema mradi ulikaa siku nyingi tangu serikali ya awamu ya nne ndiyo hospitali hiyo ilianza kujengwa baadae kutelekezwa...
Hospitali imeanza kujengwa 2014 mpaka Leo miaka 8 baadaye haijaisha bado unakuja kusifu? Awali ilikuwa inajengwa chini ya serikali ya CUF?

Sent from my M2003J15SC using JamiiForums mobile app
 
Katika pitapita zangu Mkoa wa Shinyanga nimefika kushuhudia mradi mkubwa wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla mradi unaenda kwa kasi ingawa baada ya kufanya mahojiano na wakazi wa maeneo hayo ya mradi wamesema mradi ulikaa siku nyingi tangu serikali ya awamu ya nne ndiyo hospitali hiyo ilianza kujengwa baadae kutelekezwa...
Kwahiyo ulienda mpaka mwawaza au ndio mwana shinyanga mkazi ?
 
Inatakiwa serikali iachane na majengo ya chini kwenye shule na hospitali...hapo unakuwa na kaz ya kuongeza jengo moja moja tu ...
 
Back
Top Bottom