Shindano la mchoro wa siku ya Dudumizi (Dudumizi Day)

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
115
dudumizi-day-website-design-tanzania.jpg

Katika kuhakikisha tunapata muda wa kuwa pamoja na wana Dudumizi, timu nzima ya Dudumizi Technologies LTD inatarajia kuandaa siku ya Dudumizi, yaani Dudumizi Day. Siku hii itakuwa ni wakati pekee wa wana Dudumizi kujuana na jamii, pia wanajamii kujua kazi mbalimbali zinazofanywa na Dudumizi.
Katika kuelekea siku hii, tunatarajia kuandaa vifaa vitakavyotumika siku hiyo, hivyo, kwakuwa Dudumizi inahudumia wana jamii, na kwakuwa wana jamii ndiyo wanaoijua vyema Dudumizi. Tunapenda kupata mawazo yao, ni jinsi gani Dudumizi day itaonekana.
Kwenye kulitambua hilo, tumeandaa mashindano ya kudesign mchoro (artwork) itakayotumika kwenye siku ya Dudumizi, mshindi atachaguliwa na wanajamii wenyewe na kujinyakulia 50,000Tsh pamoja na Wireless Router Mercury MW 302R Mpya and Genuine kabisa.


Jinsi ya Kushiriki:
1. Penda (like) kurasa yetu ya Facebook
2. Tuma mchoro wako na maelekezo kwenye kurasa ya Facebook ya Dudumizi, Timu ya Dudumizi itachagua michoro 3 yenye Interaction kubwa (Comments, Likes & Share)
3. Michoro hii mitatu itapigiwa kura na Fans w Dudumizi, na atakayepata interaction kubwa, ndiye mshindi
4. Mshindi atapatikana na kukabidhiwa zawadi yake.

MUDA: Muda wa mwisho wa kutuma michoro (arworks) ni Ijumaa, April 10,2015
KUMBUKA: Zoezi hili ni kwa ajili ya fans wa Dudumizi tu kwenye hatua zote.

Dudumizi Technologies LTD
Web: www.dudumizi.com
Address: 3rd floor, Shamo Park House, Goig, Mbezi Beach
 
Fafanua kidogo. huo mchoro wenyewe uwe na theme ipi??????
 
Back
Top Bottom