bahati mbaya
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 578
- 192
Mimi ni mwanamke, nina miaka 36. Tumejaliwa kupata watoto 2 katika ndoa yetu. Kipato cha mme wangu ni cha kawaida maana siyo kwamba anakaa nyumbani naye ni mtafutaji. Kwa lugha nyingine yeye kajiajiri. Mimi ni mwajiriwa wa Serikali ila kipato changu ni cha hali ya chini.
Jambo la kushangaza yeye haudumii familia kwa chakula, mavazi wala Elimu ya watoto. Pamoja na kutonunua chakula bado anapata huduma zote hapa nyumbani bila kujali nani anauhudumia familia yake. Mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa walao anachangia mahitaji ya familia ingawa siyo kwa kukidhi. Miezi sita iliyopita kachukua mkopo ambao sikujua aliutumia kufanya nini maana nimegundua hivyo baada ya kufuatilia sana. Naelemewa na majukumu ya familia.
Je wanaume wote ndivyo mnavyoishi katika familia zenu?