ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Ni dhairi kuwa hakuna binadamu ambaye uzaliwa na mali, hali kadhali, umauti unapomfika inakuwa ndio siku yake ya mwisho ya kumiliki mali alizozichuma hapa duniani. Kwa hali halisi, inaonekana kuwa matatizo yanayohusiana na mirathi yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku hasa kutokana mambo yafuatayo:
1. Pale Mume na Mke wanapoachana/ kutengana hata kama hawakuwa na ndoa (wameishi kama hawara) wakiwa tayari wamechuma mali na wana watoto.
2. Pale marehemu anapokufa akiwa ameacha mali nyingi
3. Pale marehemu anapokufa akiwa ameacha watoto wengi
4. Pale marehemu anapokuwa ameamua kurithisha mali zake kwa mtu/taasisi nje ya familia yake.
5. Pale marehemu anapokufa akiwa katika mahusiano yaliyotetereka (mgogoro wa ndoa)
6. Pale Mume mwenye wake zaidi ya mmoja wenye watoto anapofariki akiwa katika nyumba ya mmoja ya hao wake zake.
7. Pale familia ya upande ndugu wa Mume au Mke wanapokuwa masikini na kuishi kwa utegemezi.
8. Pale marehemu anapokuwa ameacha watoto wengi ambao wanaishi na familia zao katika nyumba za wazazi (wameoa/kuolewa na kuzaa wakiwa bado wanaishi katika nyumba ya wazazi wao).
Kwa vifo vinavyotokea katika mazingira kama haya, hata kama marehemu atakuwa ameacha wosia, bado kunakuwa na mvutano mkubwa sana wa familia kuhusu uhalaili wa huo wosis na urithi wa mali za marehemu.
Wapo wale ambao wanadiriki hata kuharibu/kudanganya juu ya wosia wa marehemu ilimradi wawemo kwenye orodha ya urithi na pia wapo wale ambao wapo tayari kutoa mtu roho ili waweze kuendelea kukalia mali za marehemu.
Zipo pia familia ambazo zimesambaratika kabisa kutokana na mambo ya mirathi na kuona kuwa Waume/Wake/baba/mama, au ndugu zao hakuwa na maana yeyote kwao hapa duniani kwa kushindwa kuwatambua katika urithi, hivyo kutowaenzi katika lolote lile mara baada ya kifo......
Tufanyeje sasa: tusiwe na mali, tusioe/kuolewa, tusizae, au tutafune mali zetu zoote kabla umauti haujatufika??