Shibuda ashangiliwa na wabunge wa CCM

mbunge shibuda akiendeleza kile kinachoitwa vijembe,mipasho ya bunge la sasa huku akitumia misamiati ya kiswahili cha pwani kumponda kiongozi wa chadema na wanachadema alishangiliwa sana na wabunge wa ccm hadi mwisho bunge kugeuka ushabiki na kuimba ccm ccm ccm.na alifika mbali zaidi na eti kuwaomba pole wananchi wa zanzibar eti kwa waliyoyapata ya kutengwa kutokana na maamuzi waliyofanya,akuwa wazi zaidi ila alimaanisha cdm kutoishirikisha cuf kutokana na kuunda serikali.
Ilinisikitisha sana huu unafiki na uzandiki mbona kama wanampenda walimchinjia baharini kwenye nec,shibuda amesahau au katumwa? Maana sikuona kachangia hoja yeyote kuhusu hotuba ya rais zaidi ya kumponda(majungu) kiongozi wa cdm.leo pale bungeni kama unataka usifiwe wewe iponde cdm unawezwa ukabebwa
cdm msikate tamaa ila kuweni waangalifu kupokea makada mitumba toka ccm ni bora mkawekeza nguvu zenu kwa vijana wapya ambao hawaijui ccm achaneni na mitumba ya ccm mlenge wagombea vijana na muutangaze mwaka 2015 kuwa wa vijana 70% ya wagombea wenu wawe vijana wasomi

nawasilisha


he must go out.
 
Akifukuzwa chamani si mbunge tena, soma hapo chini.

"Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Na Salim Said

OFISI ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi, inamtambua aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Fred Mpendazoe kuwa bado ni mbunge wa jimbo la Kishapu kupitia Chama hicho hadi hapo itakapopata taarifa rasmi kutoka CCM.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ge-mpendazoe-bado-ni-mbunge-wa-kishapu-3.html


Haya kalagabaho........................
 
tuna mmwangalia mienendo yake kwanza hope atakuja jutia kauli zake hizi

Mtamwangalia hadi mwisho..hakuna mtu anaweza kumfukuza mtu chadema hasa akiwa mbunge..

That will mean cut off..in ruzuku kwenda kwenye chama..mchaga gani atafanya biashara kichaa kama hiyo ..hakuna
 
huyo ndio angalau anawasaidia kujiweka sawa


maana hao wengine wanaambiwa ukweli wajirekebishe
 
CUF walimfukuza Naila Jidawi uanachama Msekwa akasema ni mbunge halali nadhani hata Chiku Abwao aliwahi kufukuzwa NCCR kama sikosei lakini akaendelea kula kuku pale Dodoma. Mzee mipango hii huwa inasukwa ikasukika.

Sheria za uchaguzi haziruhusu wagombea huru kugombea katika nafasi ya Urais au Ubunge, hivyo kama Mbunge akifukuzwa toka chama chake Mbunge huyo anatakiwa kupoteza Ubunge wake kinyume na hivyo ndiyo zile sheria za undumila kuwili kwamba Mbunge anaweza kuendelea kuwa mbunge huru hata kama atafukuzwa na chama chake lakini wakati huo huo wabunge watarajiwa huru hawaruhusiwi kugombea Ubunge.

 
Ccm walikiona hiki ki-parasite Shubuda wakakikata kwenye mti wao na chadema fanyeni hima kumtosha ndani ya dustbeng haraka iwezekanavyo.
Asikabidhiwe dhamana yoyote ndani ya chama.
.
 
wakuu kilichotokea jana nina hamu kuona hatua za haraka sana zikichukuliwa maana ule uchafu ulikuwa wazi mno sijui cdm watahitaji ushahidi gani na nafikiri wamejifunza namna kufanya after issue ya zitto.nimeongea na wadau wengi wote wanasubiri kuona nn cdm watafanya.binafsi nafikiri cdm wakubali walipotea kwa shibuda na wamfukuze HARAKA.nasubiri tamko lao kwa hamu nione ukomavu wao.
 
Wakuu nimeongea na Shibuda amekataa kata kata hajawahi kutamka upuuzi mnaoandika tafadhali Elimukwanza tuombe radhi CHADEMA na mheshimiwa Shibuda bwa ha ha ha ha ha.
 
Ikielezwa kuwa CDM ni wataalamu wa kukurupuka, wanachama wake wanataka kumtoa mtu roho.

Mmemkaribisha haraka Shibuda kwenye chama bila ya kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo wake.

Tumewazoea viongozi wenu, hasa Dr na mkulu wa kambi ya upinzani.... wanakurupuka kwa kwenda mbele.

CDM days are numbered!
 
Shibuda ukiendelea na msimamo huo utashangiliwa sana na CCM kama alivyo shangiliwa mtoto wa Mzee Zuberi lakini mtaji wako kisiasa unaliwa kwa kasi............Wanasiasa wenye akili sasa hivi wana simama upande wawa nanchi, kila alifanyalo lazima liwe na maslahi ya wananchi maana ndiko uliko mtaji wao.Nyie leteni mchezo mkidhani CDM ni kimbilio la wakosefu mkadhani mtadumu kwenye siasa........
 
Mbunge shibuda akiendeleza kile kinachoitwa Vijembe,mipasho ya bunge la sasa huku akitumia misamiati ya kiswahili cha pwani kumponda kiongozi wa CHADEMA na wanachadema alishangiliwa sana na wabunge wa CCM hadi mwisho bunge kugeuka ushabiki na kuimba CCM CCM CCM.Na alifika mbali zaidi na eti kuwaomba pole wananchi wa zanzibar eti kwa waliyoyapata ya kutengwa kutokana na maamuzi waliyofanya,akuwa wazi zaidi ila alimaanisha CDM kutoishirikisha CUF kutokana na kuunda serikali.
Ilinisikitisha sana huu unafiki na uzandiki mbona kama wanampenda walimchinjia baharini kwenye NEC,Shibuda amesahau au katumwa? maana sikuona kachangia hoja yeyote kuhusu Hotuba ya Rais zaidi ya kumponda(majungu) kiongozi wa CDM.leo pale bungeni kama unataka usifiwe wewe iponde CDM unawezwa ukabebwa
CDM msikate tamaa ila kuweni waangalifu kupokea makada mitumba toka CCM ni bora mkawekeza nguvu zenu kwa vijana wapya ambao hawaijui CCM achaneni na Mitumba ya CCM mlenge wagombea vijana na muutangaze mwaka 2015 kuwa wa vijana 70% ya wagombea wenu wawe vijana wasomi

Nawasilisha

Shibuda ni CCM damdam,aliingia CDM ili kuisambaratisha.Kama wasipomfukuza atawaliza!
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu ITV wametoa clip kidogo za mazungumzo ya Cheyo na Shibuda bungeni jana. Inaonekana hawa wazee wamewachoka vijana walio kwenye hiyo kambi yao, na kwamba wanampenda JK sana
 
Shibuda ni kada wa ccm pia ni afisa usalama wa tangu enzi zile za kukomboa nchi za kusini mwa afrika hivyo u ca imagine ameumwa makusudi na mie naamini cdm walilijua hili ila sikuelewa kwa ninii walimchukua...
Na hiki ndich kilichofanya ccm kukaa muda mrefu namna hii madarakani kwani sekta muhimu zote usalama wa taifa jeshi na mengineyo yalikuwa yanaingowa na miongozo ya chama hata sasa ndo maana utaona wakuuu wengi wa mikoa wilaya n]na hata wakurugenzi wengi ni wanajeshi au usalama wa taifa .....
 
Kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku huu ITV wametoa clip kidogo za mazungumzo ya Cheyo na Shibuda bungeni jana. Inaonekana hawa wazee wamewachoka vijana walio kwenye hiyo kambi yao, na kwamba wanampenda JK sana
Du You Tube ya Michuzi iliyowekwa na M. Shosi imenifurahisha sana kwani zinaondoa ubishi mm ningeomba atakayenasa za Shibuda na Cheyo atuwekee hapa ubishi uishe. Mm nimeingia mpaka http://www.starTV.Tanzania hamna hotuba hiyo labda TBC
Ukweli Shibuda amekandia vijana kukurupukia siasa na migomo na ameisifu hotuba ya Rais kadai kulikuwa hakuna haja ya kuiacha kuisikiliza.
Mwenye clip hiyo naomba atuwekee
 
Wakuu nimeongea na Shibuda amekataa kata kata hajawahi kutamka upuuzi mnaoandika tafadhali Elimukwanza tuombe radhi CHADEMA na mheshimiwa Shibuda bwa ha ha ha ha ha.

Itakuwa jambo la busara itafutwe clip yake tumsikie wenyewe.....
 
Sheria za uchaguzi haziruhusu wagombea huru kugombea katika nafasi ya Urais au Ubunge, hivyo kama Mbunge akifukuzwa toka chama chake Mbunge huyo anatakiwa kupoteza Ubunge wake kinyume na hivyo ndiyo zile sheria za undumila kuwili kwamba Mbunge anaweza kuendelea kuwa mbunge huru hata kama atafukuzwa na chama chake lakini wakati huo huo wabunge watarajiwa huru hawaruhusiwi kugombea Ubunge.


Hizo ndio sheria zetu kwa upande mwingine naziunga mkono maana gharama za kuitish uchaguzi mpya ni mzigo kwa walipakodi!
 
Back
Top Bottom