Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Hivi unafananisha JF na Bunge?
Nimecheka!
Hivi unafananisha JF na Bunge?
JAMANI NI VYEMA TUKAELEWA KUWA CHADEMA SASA NI CHAMA KIKUBWA, SI SAWA NA TLP, NRD, UDP, JAHAZI ASILI, NLD nk. Mnapokuwa ktk chama kikubwa ni lazima mtofautiane ktk mambo mengi mengine ni madogomadogo na mengine ni ya msingi. Mfano CCM ni chama kikubwa na sasa wanatofautiana sana ktk njia ya kutumia kuwashughulikia MAFISADI maana ktk watoa maamuzi MAFISADI pia wamo. Si vyema kusema SHIBUDA Afukuzwe, apewe ONYO au ATENGWE na CHAMA. CDM watakuwa hawajengi bali wanabomoa maana haitapata kutokea DUNIANI wote tukaamini na kuongea lugha moja ktk HOJA itakayokuwa mbele yetu. Hivyo kuvumiliana na kuchukuliana ni jambo la msingi ktk kujenga CHAMA CHA KIDEMOKRASIA kama ilivyo CDM.
Tukumbuke kosa lilishafanywa na VIONGOZI wa CDM kwa kuwapokea wakina PROF. KAHIGI, SHIBUDA, WENJE, NYIMBO na wengine wengi Bila kuwafanyia VETTING kama kweli hawa watu wanaamini ktk Demokrasia na Ideology za CDM au wanajiunga ili wapate nafasi ya Kugombea UBUNGE, najua muda ulikuwa hautoshi kwa VETTING kufanyika hivyo viongozi walikuwa na uamuzi wa aina tatu, moja wawapokee na kuwapitisha kugombea au wawapokee na wasiwapitishe kugombea ubunge au wasiwapokee kabisa. SASA viongozi wa CDM waliona ni BUSARA kuwapokea na kuwapitisha kugombea UBUNGE wapo walioshinda ndio hao wakina KAHIGI,WENJE na SHIBUDA na wapo walioshindwa kama mzee NYIMBO. SASA si sahihi kutumia hasira ktk kushughulikia matatizo yanayosababushwa na wageni hawa ndani ya CDM. Maana Viongozi wa CDM wakati wanafanya uamuzi wa kuwapokea na kuwapitisha wawe wagombea ubunge kupitia CDM iliwapasa watambue kuwa mbeleni kuna matatizo kama haya yanaweza kujitokeza, sasa yamejitokeza dawa si kutimuana dawa ni kuyakabili na kuyatatua kwa busara na mbinu za kisasa za usuluhishi wa mogogoro.
Tukumbuke SHIBUDA na wenzake walisha zoea ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI WA CCM, na siku zote walisha zoea kuwaogopa na kuwatii viongozi wenye nguvu ya kiserikali(dola) na kichama. Viongozi wa CDM hawana nguvu za DOLA hivyo kwa SHIBUDA kuwahofia ni ngimu. Pia tukumbuke SHIBUDA anaungomvi na Mbunge mwenzie wa CDM mh. WENJE na aliwapelekea viongozi wa CDM mgogoro huo wautatue lakini wameupotezea sasa SHIBUDA anaamini yeye anachukuliwa kama mtoto wa kambo CDM. Hivyo kauli nyingine zinatokana na Hasira alizonazo.
PIA wana CDM kumbukeni kauli za SITTA na MWAKYEMBE pia zinawaudhi viongozi wa CCM lakini wanazipotezea na kuandaa mkakati wa kichama kuwashughulikia, (naomba nieleweke sio kwamba nawaunga mkono, bali muelewe kwa wana siasa MASLAHI ( wachumia tumbo) kwao chama kwanza nchi na wananchi baadae) sasa CDM isiingie ktk mtego huo ktk kushughulikia suala la SHIBUDA ni lazima MASLAHI ya TAIFA yawekwe mbele na ya CHAMA yafuate baadae.
Kumbukeni SHIBUDA kwa zaidi ya miaka 40 yeye anaimba wimbo wa CCM hivyo inawezekana hajajijua kuwa sasa yupo CDM na wimbo wa CDM ni peoples power bila kujali nguvu za DOLA za kiongozi. AMINI nawaambia SHIBUDA itafika mahala atabaini CCM si nyumbani tena hivyo hatokuwa na jinsi bali kutii uongozi na chama cha CDM
Huyu ni pandikizi la CCM kule CHADEMA, CHADEMA kama hawakuwa makini anaweza kabisa kukivuruga chama halafu akatangaza kurudi kwenye chama cha mafisadi.