Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
- Thread starter
- #21
Ta Ruta,
Binafsi nilishasema kuwa JK na serikali yake hawana nia njema kwenye suala la katiba mpya. Toka mwanzo, Waziri Kombani na AG walikuwa wanajikanyaga kwani hawakujua kitu gani wananchi wanataka. Hata JK mwenyewe hakujua pia na alikiri hayo mbele ya vingozi wa CHADEMA.
Hata Wabunge walipoptisha mswada wa hii sheria kwa mara ya kwanza, nilionga na baadhi yao na kuwaeleza kuwa wangetumia busara kidogo kujielimisha ni kitu gani hasa wananchi wanahitaji. Badala yake, viongozi wetu wameendekeza ushabiki.
Kwa hapa tulipofika, tunahitaji akina Mtikila kuchukua hatua ili kutuepusha na huu usanii ambao unaweza kutuletea matatizo makubwa huko mbele ya safari.
mtikila ni sawa lakini nasi tuanze kujenga utamaduni wa kukataa kuburuzwa na hawa mafisadi........