Sheria inasemaje kuhusu hili?

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Jul 27, 2008
3,173
481
Naomba kwa wale wana JF wenzangu wenye ueledi na mambo ya sheria za kazi wanijuze hili.
Kuna mfanyakazi wa serikali tena ni mkurugenzi wa halmashauri! Yeye ana kesi ya mahakamani. Hii kesi bado inaendelea. Je sheria inasemaje mtumishi anapokuwa na kesi mahakamani wakati tuhuma zinazomkabili ni za ofisi hiyohiyo anayoifanyia kazi?
Sijui kama nimeweka sawa ila wenye kuweza kusaidia hili watujuze!
 
Mkurugenzi halmashauri Moshi kizimbani kwa uhujumu uchumi
Wednesday, 25 January 2012 23:10
Daniel Mjema, Moshi
TAASISI ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imewaburuza kortini vigogo wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini (MDC), wakikabiliwa na makosa mawili ya uhujumu uchumi.
Vigogo hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Mariam Lusewa ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Annah Mwahalende na Kaimu Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu, Sadik Mrisho.
Kwa kawaida kesi za uhujumu uchumi husikilizwa na Mahakama Kuu ya Tanzania, isipokuwa, zinaweza kusikilizwa na mahakama ya hakimu mkazi kama Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) atatoa idhini.
Katika kesi hiyo, tayari DPP alishatoa idhini hiyo Desemba 16, mwaka jana ili tuhuma zinazowakabili vigogo hao ambazo ni kinyume cha kifungu namba 12(3) sura ya 200 ya sheria ya uhujumu uchumi kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, isikilizwe na mahakama hiyo.
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Susan Peter, alidai mahakamani hapo juzi kuwa, makosa yanayowakabili watumishi hao wa umma, waliyatenda kwa pamoja kati ya Desemba 2006 na Machi mwaka jana.
Katika shtaka la kwanza, Susan anayesaidiana na Maghela Ndimbo, alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa hao kwa uzembe wa makusudi walishindwa kumchukulia hatua za nidhamu Mhudumu wa Afya wa Zahanati ya Lole aliyetajwa kuwa ni Frank Lyimo.
Waendesha mashtaka hao walidai, licha ya mtumishi huyo kutokuwapo kituo chake cha kazi kuanzia Aprili,2006 hadi Novemba, 2008, washtakiwa hawakumchukulia hatua za nidhamu.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kati ya Desemba, 2008 na Machi, mwaka jana washtakiwa hao walishindwa kutimiza majukumu yao kwa busara na kuisababishia Halmashauri ya Moshi kupata hasara ya Sh2.75 milioni.
Washtakiwa wote walikana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana kwa sharti ya kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja ambaye ni mtumishi wa Serikali mwenye kitambulisho.

Washtakiwa hao walitimiza sharti hilo na kesi hiyo iliahirishwa hadi Februari 28, mwaka huu itakapotajwa tena.



Hii ndiyo ilisukuma kuuliza hayo
 
Hebu iweke sawa kidogo.Unamaanisha anaendelea na kazi katika ofisi hiyohiyo wakati kesi yake inaendelea mahakamani sio?
 
kwa mijibu wa sheria anatakiwa kuwa nje ya ofisi hadi hapo kesi yake itakapoamuliwa. Anakuwa nje ya ofisi huku AKILIPWA FULL salary siyo nusu mashahara kama zamani.
 
kwa mijibu wa sheria anatakiwa kuwa nje ya ofisi hadi hapo kesi yake itakapoamuliwa. Anakuwa nje ya ofisi huku AKILIPWA FULL salary siyo nusu mashahara kama zamani.

Sawa kabisa, anasimamishwa ili asiendelee kuwa ktk mazingira ya kazi ambapo uwepo wake unaweza kupelekea kuaribu ushahidi.
 
kwa mijibu wa sheria anatakiwa kuwa nje ya ofisi hadi hapo kesi yake itakapoamuliwa. Anakuwa nje ya ofisi huku AKILIPWA FULL salary siyo nusu mashahara kama zamani.

Kama ndivyo huyu mama mkurugenzi nilimkuta jana akiwa na gari la serekali. Nilimkuta maeneo ya shule ya Sekondari Umbwe ambaka alikuwa anahudhuria kikao cha bodi ya shule akiwa kama mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi. Je viongozi wake hawajui hilo? Kama wanajua ni wazembe kutekeleza taratibu na sheria za nchi? Je nao wanaohusika na ajira ya huyu mama hawaoni wanastahili kuwajibishwa kwa kutumia vibaya madaraka ya ofisi zao?
 
Back
Top Bottom