Sheria inasemaje kiongozi wa juu akiwa mahututi? Je, familia inaweza kumzuia nyumbani?

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,204
10,951
Suali hilo limenijia baada ya mkuu wa majeshi mstaafu, Captain Mabeyo aweke wazi hali ilivyokuwa kabla na baada ya kifo cha raisi wa awamu ya 5, John Pombe Magufuli.

Sehemu iliyonipa hisia ni pale ambapo Serikali kupitia vyombo vya usalama viliona visitangaze kifo chake kabla ya familia yake kupelekewa taarifa hiyo ya huzuni.

Sehemu ya pili ni pale kiongozi anapoumwa sana kiasi ya familia kukata tamaa au kuwa na mashaka ya matibabu yake.

Je, wanaweza kumzuia mtu wao asiende kwenye matibabu?
 
Imagine mke sijui yupo wapi huko mume anauguzwa Mzena. Na pengine hata yeye aliambiwa mumeo ni mzima anachapa kazi.
 
Unamkosea sana heshima mabeyo kumuita captain

Welfare ya mtu kama rais ipo chini ya vyombo vya usalama... Familia hawana say yoyote linapokuja swala zima la kuamua kuhusu afya ya rais...
 
Suali hilo limenijia baada ya mkuu wa majeshi mstaafu, Captain Mabeyo aweke wazi hali ilivyokuwa kabla na baada ya kifo cha raisi wa awamu ya 5, John Pombe Magufuli.

Sehemu iliyonipa hisia ni pale ambapo Serikali kupitia vyombo vya usalama viliona visitangaze kifo chake kabla ya familia yake kupelekewa taarifa hiyo ya huzuni.

Sehemu ya pili ni pale kiongozi anapoumwa sana kiasi ya familia kukata tamaa au kuwa na mashaka ya matibabu yake.

Je, wanaweza kumzuia mtu wao asiende kwenye matibabu?
a sick person belongs to the healing God of the afflicted and medical doctors and not otherwise....

labda kama ni washirika wa ushirikina na uchawi
 
Back
Top Bottom