Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
Nipo na glasi yangu ya shurbati nikiangalia TBC1 wakileta live mambo ya kuzima mwenge kutoka mkwakwani Tanga. Kwa kuwa ninaweza kuwashushia, haya ndiyo yanayojiri hivi sasa.
Mapema, kulikuwa na misa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere ambayo rais alitakiwa kuhudhuria lakini alishindwa kufanya hivyo na kumtuma kapuya kumwakilisha.
Baadaye alipoamka, alikwenda kukagua maonyesho katika mabanda ya vijana.
Hivi punde ameingia Mkwakwani na vijana wametumbuiza halaiki bomba. Walipoimba ule wimbo maarufu-NI WAJIBU TUMSUHUKURU BABA NYERERE, JK alishindwa kuvumilia akaamka kitini na kuanza kucheza sambamba ya midundo ya wimbo.
Hivi sasa kuna burudani za nyimbo za kienyeji, akina mama wa Tanga wanakatika kinoma-naona mmoja anakata viuno na chungu kinachowaka moto kikiwa kichwani Mh! mambo ya tanga hayo!