Mzanaki
Member
- Feb 25, 2011
- 20
- 11
Kifo cha mchawi huyu mashuhuri wa serikali kinaonyesha kuwashtua watu wengi ambao kwa njia moja au nyingine walimtegemea mchawi huyu katika masuala mbalimbali ya kimaisha na kisiasa.CCM na mwenyekiti wake Kikwete ni baadhi ya watu walioinjoi kwa kiasi kikubwa utaalam wa mchawi huyu mashuhuri.Mchawi huyu alitumika kupindisha mwelekea wa siasa kwa kutabiri ushindi kwa CCM na yeyote aliyemtaka ili kukatisha tamaa juhudi za upinzani katika kuitoa serikali madarakani.Mmoja wa watu ambao tayari wameshakiri kushtushwa na kifo cha mchawi huyu ni Kikwete ambaye kwa kiasi kikubwa alifaidi utabiri na ulinzi kutoka kwa mzee huyu.
Sheikh Yahya ndiye aliyetishia Watanzania wengine kupambana na Kikwete katika ugombea wa urais kwa kusema mtu atakayejaribu kufanya hivyo atakufa.Sheikh Yahya ndiye aliyetabiri ushindi kwa Kikwete ambao pamoja na kwamba ulipatikana kwa uchakachuzi wa kura tayari wananchi walishaaminishwa kuwa Kikwete atashinda.Sheikh Yahya ndiye aliyemhakikishia ulinzi Kikwete wakati akianguka hovyo majukwaani kwa kusema hakuna kitakachomgusa kwani ameshamtumia walinzi wa kutosha.
Utabiri wa Sheikh Yahya katika siasa hauwezi kutofautishwa na tafiti pandikizi za REDET katika kuibeba CCM katika chaguzi za kitaifa.Katika mtazamo huu ni dhahiri kwamba Kikwete na CCM kwa ujumla wamepoteza mchawi muhimu katika kupindisha mwelekeo wa siasa za Tanzania.