Sheikh Ponda ajeruhiwa vibaya baada ya kupigwa Risasi mjini Morogoro

Status
Not open for further replies.
Naona povu limekutoka kuona imetajwa Chadema alichosema HUSSEIN ni ukweli mtupu.
Waliompiga risasi Shekhe Ponda wako chini ya chama gani na wanafanya kwa maagizo ya nani..,We Ritz u're a silent killer,unaua waislam wenzako kiunafki...
WEKA MBALI CCM NA JAMII..
 
Weka ushahidi ni chama cha wakristo au povu linakutoka tu,kuna waislam humu hawana chama na hawamkubali Ponda na harakati zake,hapo alipo anawabagua waislam wenye msimamo wastani sembuse wakristu,we kufa na ufinyu wa akili yako ila chadema ni mali ya Watanzania wenye iman na wasio na imani..,uzuri hata Askofu au Padri akiboronga anapewa kubwa tu ili ajue kazi yake ni nini,we kufa na Ponda ndio mungu wako..,nasema Polis walipaswa kumkamata ila sio kumpiga risasi na pia haya yote kayatafuta mwenyewe,hicho anachokitafuta ni kazi ya shetani na sio Mungu...

Huo ujinga wenu tumeshauzoea. Hivi ulitaka Ponda akamatwe kwa lipi? Mimi sio kuwa naunga mkono kila harakati ya Ponda. Ila naumia kwakuwa ni muislamu/binadamu mwenzangu. Iweje mwenzako ameumia huku unatangaza bora angeuliwa,mara unasema unaenda baa kula kitimoto?.
 
Tbccm wanasema hakuna tukio kama hilo ni uzushi kweli iko siku tutaivamia hichokituo na kukichoma moto hakina faida yoyote kwa watanzania..

labda ujikusanye ww na akili yako finyu ndo mchome moto. Sasa ulitaka waripoti taarifa ya kutengeneza? Mm nmewaambia toka jana nilikuwa kwenye eneo la tukio shehe ponda hajapigwa risasi ila ilipigwa bom la machoz kuwatawanya wafuas wake waliotaka kuleta vurugu, yeye alitoroshwa na baadh ya wafuas wake
 
Waumini wakikristo walioko JF wangekua na huu mtizamo, ingesaidia sana kupunguza tatizo la chuki za kidini.

Mimi ni Mkristo na ninaunga mkono waislam waachwe wajiongoze wenyewe, kwanini waundiwe chombo cha kuratibu maswala yao ya dini? CCM itoe mkono wake BAKWATA, huu si mgogoro wa waislam na wakristo ni mgogoro uliondani ya waislam na wao ndo wenye suluhu ya huu mgogoro. Kumuwinda ponda namkumuua kunaondoa heshima ya nchi hii hasa baada ya Kikwete kumtaka Kagame azungumze na Waasi wake, ni Bora Kikwete akaingilia mgogoro huu kwa mazungumzo badala ya kutumia vyombo vya dola kumuwinda Ponda.
 
Habari hii ni kweli au ni uzushi? Kama ni kweli I think for the first tym nitakuwa against Mwema


Ndugu kama siku zote ulikuwa unamuunga mkono kwa matukio yote ya polisi kuua na kupiga wananchi basi wewe una matatizo makubwa sana. Yaani wewe umemuona Ponda tu? Vipi kuhusu kifo cha Mwangosi, vifo na vipigo vya wafuasi wa CHADEMA Arusha, na mengine mengi ambayo polisi wamefanya? Vipi kuhusu amri ya mkuu wa serikali kuwa wakorofi wapigwe tu na polisi wewe hukuisikia!! Na je nayo uliiunga mkono pia? Je ulidhani amri ile ingeishia kwa wafuasi na wanachama wa CHADEMA na wapinzani wengine tu? Kwa mtazamo wangu Mwema na maaskari wake hawana tatizo lolote wanatekeleza kwa uaminifu maagizo ya waliomteua na wanaomsimamia kazi zake za kila siku.
 
Hongera kwa kauli ya bwana Mtatiro na si ya CUF

Mimi napata shida kwenye hii hoja. Kwamba kauli hii ni ya Mtatilo na si ya CUF! Hivi kweli kwa akili ya kawaida unawezaje kutofautisha Mtatilo na CUF?

Mpangilio wa maneno uliomo umekaa kichama, umekaa ki-CUF. Na kwa kweli tungeshangaa kama Waliberali wasingechangia na kutoa msimamo huu. Tumewasikia Wana CUF.
 
kwa huyu sheikh ponda ni mrundi .. katika list ya wakimbizi haramu naye arudi kwao sasa.. asituvunjie amani na kutuharibia dini zetu.. sisi wote ni watanzania na sio waponda.
 
1098211_490799674348104_1279780635_n.jpg
 
Huyu ponda akiachiwa atakuja kuua wengi zaidi nashindwa kuelewa kwani askari wetu wanakosa weledi wa kulenga shabaha mbona kule arusha waliweza, huyo askari alikua doja kule ccp moshi.
 
Mkuu Ritz sheikh Ponda yupo against ccm, soma maneno yake ktk mhadhara wa jana morogoro, source: Mwananchi
"Katika kongamano lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege, Sheikh Ponda alisema kuwa matatizo ya kunyanyaswa na kuteswa kwa Waislam yamekuwa yakichangiwa na Serikali iliyoko madarakani na kuwataka Waislamu kuhakikisha kuwa katika Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 wanachagua Serikali mpya yenye kujali haki sawa."
Ritz soma hapo juu...,hahahaaaaa ni maneno ya Shekhee Ponda..
Viva chadema..
 
Waislam nawaomba muwe na moyo wa busra katika kipindi kigumu kama hiki,,.......nawaomba sana tafadhali,,...kamwe msipoteze mda wenu kubishana na wala nguruwe wenye fikra finyu wasio fikiri
 
Kama sheick Ponda ni gaidi,kumtetea inaleta mashaka.

unahitaji elimu ya miaka 2 kuelewa nini maana ya ugaidi na ndio maana kila kesi inayoitwa ya ugaidi kwa Tanzania imekuwa ikifutwa,bado elimu ya neno na kipi ni ugaidi inahitajika kwa watanzania
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom