Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tabora amefariki dunia

M-bongo

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
338
71
Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora, Sheikh Mavumbi amefariki Dunia leo asubuhi mjini Tabora na mazishi yanatarajiwa kuwa Kesho mjini Tabora.
 
RIP Sheikh Mavumbi, Mungu atakupastahili yako kulingana na matendo yako duniani!
 
heri wenye moyo safi maana watamuona mungu......
moyo wa sheikh ulikuaje? anajua allah.....
 
R.I.P Sheikh Mavumbi. Kweli merudi mavumbini kama jina linavyosomeka. Mungu akulaze pema.
 
heri wenye moyo safi maana watamuona mungu......
moyo wa sheikh ulikuaje? anajua allah.....
Angekuwa Baba yako mzazi ndiye amekufa ungethubutu kuandika hayo ulio yaandika hapa!?

Kuwa na adabu na kuheshimu wazee wa wenzio.
 
Sheikh mkuu wa mkoa wa Tabora, Sheikh Mavumbi amefariki Dunia leo asubuhi mjini Tabora na mazishi yanatarajiwa kuwa Kesho mjini Tabora.
انّا للہ و انّا الیہ راجعون
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Surely we belong to Allah and to Him shall we return'
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.


Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.
2:157

Wale ambao kwamba yanapo wateremkia machungu ya kuwaumiza wanaamini ya kuwa hakika kheri yote na shari inatokana na mwenyewe Mwenyezi Mungu, na ya kwamba amri yote ni ya Mwenyezi Mungu.

Hao husema: Sisi ni milki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na sisi ni wenye kurejea kwake Yeye.

Sisi hatuna letu jambo lolote. Na Yeye ni mwenye kustahiki kushukuriwa kwa anacho toa, na juu yetu kusubiri wakati wa kujaribiwa, na kwake Yeye ndiyo zipo thawabu na malipo.

Basi hao wenye kusubiri, wenye kumuamini Mwenyezi Mungu, wanapewa bishara njema kuwa watapata maghfira na ihsani ya Mwenyezi Mungu, na wao ndio wenye kuongoka njia ya kheri na uwongozi mwema.

Nachukuwa nafasi hii kuwapa mkono wa rambi rambi na pole nyingi kwa wafiwa, ndugu na jamaa na marafiki wote.

MwenyezuMungu awape subra wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya msiba wa Sheikh Mavumbi.
Amin
 
Mmungu amsamehe makosa yake na amuweke katika daraja ya watu wema peponi nasi Mmungu atuwepushe na moto siku hiyo.
 
Back
Top Bottom