Sheikh Jongo bado ana mengi ya kujifunza

Status
Not open for further replies.
Umejuaje kama kilio cha sheikh Jongo cha kinafiki??? hivi mtu kuonyesha hisia zake ni unafiki?? kauli alizotoa mh. Lukuvi si sahihi alilenga kwenye kuimarisha muungano lakini hakuchagua maneno mazuri hilo nakubaliana na wewe; lakini kwa sheikh Jongo kidogo sitakubaliana na wewe zile ni hisia tu sheikh inaonekana ni mwanaCCM hakufanya lolote baya la kuwaudhi waislamu au muumini wa dini yoyote.
chama..Uislam ni Zaidi ya Siasa..huwezi hata kuufananisha na Tasisi yoyote maana itakua ni Matusi..

Yani Sheikh ulie sababu ya CCM? Huku Uislam ukikashifiwa,Tukanwa Waislam wananyanyaswa..Wanauawa..Yote haya yasimfanye kulia aje kulia kwa Nyerere?

Kwa ufupi amefanya Jambo baya sana..Siyo kawaudhi Waislam tu..Zaidi Kamuudhi Allah..
 
Last edited by a moderator:
Sheikh Jongo amekosea kwa kitendo alichofanya kama ilivyo kwa binadamu yeyote Yule huwa anafanya makosa.
Nauliza ni nguvu ya waislamu pekee iliyotumika kuleta uhuru Tanganyika?
 
Si mafundisho yangu, kwa niliyoyaona na kuyashuhudia. AlhamduliLlahi nipo kabla ya Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, nimeiishi awamu yake, nnajuwa tulipotoka, labda wewe ndiyo umehadithiwa tu.

Niliihama Kariakoo na Tanzania kwa ajili ya Nyerere, na si mimi pekee ni wengi sana kama mimi, for your information.

Habibt utawadanganya hao wa kuhadithiwa hata mimi nimeyaona ndio maana namuunga mkono kwa yote; habibt kumbe ulihama mwenyewe kwa kutaka mimi nilidhani Nyerere alikushikia viboko na kukuhamisha kwa nguvu; lakini mwisho wa yote si umerudi palepale Kariakoo?? sasa ulichodhulumiwa ni kipi??
 
chama..Uislam ni Zaidi ya Siasa..huwezi hata kuufananisha na Tasisi yoyote maana itakua ni Matusi..

Yani Sheikh ulie sababu ya CCM? Huku Uislam ukikashifiwa,Tukanwa Waislam wananyanyaswa..Wanauawa..Yote haya yasimfanye kulia aje kulia kwa Nyerere?

Kwa ufupi amefanya Jambo baya sana..Siyo kawaudhi Waislam tu..Zaidi Kamuudhi Allah..

Uislamu unakataza waumini wake wasiwe wafuasi wa siasa?? katika mafundisho tumekatazwa kuwahukum watu mbona wewe umechukua jukumu la kumhukumu sheikh Jongo pasipo sababu ya msingi??
 
Sheikh Jongo amekosea kwa kitendo alichofanya kama ilivyo kwa binadamu yeyote Yule huwa anafanya makosa.
Nauliza ni nguvu ya waislamu pekee iliyotumika kuleta uhuru Tanganyika?

Uhuru wa Tanganyika uliletwa na watanganyika wenyewe haukuletwa kwa misingi ya kidini!
 
Ni kweli umeletwa na watanganyika wenyewe ila waislam walijitolea zaidi kwa hali na mali.
Kinacho semewa ni kuweka sawa historia iliyo potoshwa na nyerere kuwa kazi yote akiifanya peke yake.
Alikuwapo na akasimamia mradi wa historia potofu.hakupenda watu wengine hasa waislam waingizwe kwenye historia ya kudai uhuru.alipenda sifa sana .
Haya yasinge andikwa kama record zingewekwa sawa ila chuki zake akalazimisha itikadi yake ys zidumu fikra za mwenyekiti mpaka kwenye mambo muhimu ya historia ya nchi.hakujali athari za kusimesha propaganga.
Leo vijana wanapata elimu ya ukweli kili chitokea na wanasema kumbe tumedanganywa ...na wale walozoea kudanganya basi hawakubali ukweli hata kama wanayemkuza hayupo tena..hawa utawakuta wanapayuka ooh unamkashifu nyerere ..na wengine hujiliza liza kinafiki
 
Hakuna aliyejitolea zaidi au pungufu; watanganyika walipigania uhuru kwa umoja wao; Hakuna hata siku moja Nyerere alidai alipigania uhuru peke yake.
 
Habibt utawadanganya hao wa kuhadithiwa hata mimi nimeyaona ndio maana namuunga mkono kwa yote; habibt kumbe ulihama mwenyewe kwa kutaka mimi nilidhani Nyerere alikushikia viboko na kukuhamisha kwa nguvu; lakini mwisho wa yote si umerudi palepale Kariakoo?? sasa ulichodhulumiwa ni kipi??

Kudanganya ni moja katika sifa ambayo si yangu. Huo u "habibt" wako kwangu umetoka wapi na umeanza lini? hunijuwi sikujuwi. Koma.

Juu, hapo ulisema hujaona wala hujasikia wala jongo humjuwi, leo hii uwepo kwa Nyerere na usijuwe kuwa kawatia ndani masheikh, kawadhahalilisha masheikh, kawafukuza masheikh, kawahamisha masheikh, halafu bado yote huyajui? una mdomo wa kuuliza "ulichodhulumiwa ni kipi?"

Ni zaidi ya kiboko kilichoniondoa Tanzania, unafikiri kumfukuza mtu ni lazima umshikie kiboko tu? labda uwe mtumwa. Mimi sina sifa hiyo.

Nilichodhulumiwa ni kidogo sana lakini kwa muungwana ni kikubwa, labda wewe usiye na asili ya uungwana hakiwezi kukudhuru. Idhlal ndicho kilichokuwa dhulma kwangu.

Khaa! leo hii, unauliza "ulichodhulumiwa ni kipi?" unachokisoma hukielewi basi hata picha huoni?
 
Hakuna aliyejitolea zaidi au pungufu; watanganyika walipigania uhuru kwa umoja wao; Hakuna hata siku moja Nyerere alidai alipigania uhuru peke yake.

Tuoneshe historia inayoonesha mchango wa Waislaam katika "kupigania" huo Uhuru, kama usemayo ni kweli.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Uislamu unakataza waumini wake wasiwe wafuasi wa siasa?? katika mafundisho tumekatazwa kuwahukum watu mbona wewe umechukua jukumu la kumhukumu sheikh Jongo pasipo sababu ya msingi??

Ni wapi imekatazwa kumhukumu mtu? na nani aliye mhukumu Jongo? mimi nasema Jongo mnafik, hiyo si hukumu. Hiyo ni tuhuma, unajuwa hukum ya mnafik Kiislaam?
 
  • Thanks
Reactions: prs
Nimeisoma ndugu kilichonikwaza ni kumtukana Mwalimu Nyerere.

Nyerere alikuwa mdhulumati tu!
Na Kiumbe mwenye roho mbaya kuliko Shetani.
Mwizi wa fadhila na Hasidi asie na Hisani!

Roho korosho na mbinafsi mkubwa!
Na huyo jongo mnafiki mkubwa!

Kile kilio choote ni kutetea kile kitumbua chake tu!

Zee zima halina hata haya!
 
Tuoneshe historia inayoonesha mchango wa Waislaam katika "kupigania" huo Uhuru, kama usemayo ni kweli.

Uhuru wa Tanganyika haukupiganiwa kwa misingi ya dini; watanganyika wote bila kujali imani ya dini zao walishiriki; wapo waislamu; wakristo na wapagani; hakukuwa na mchango ambao ulitikana na misingi ya kidini; hizo historia zenu za magumashi tafuteni wa kuwaongopea; babu yangu ni muislamu alishiriki katika za kutafuta uhuru sio kwa misingi ya imani ya kidini bali kwa utanganyika wake ndio maana watu walishirikiana katika harakati zile bila kujali dini zao.
 
Ni wapi imekatazwa kumhukumu mtu? na nani aliye mhukumu Jongo? mimi nasema Jongo mnafik, hiyo si hukumu. Hiyo ni tuhuma, unajuwa hukum ya mnafik Kiislaam?

kwa hiyo wewe ndio umejitwisha mamlaka ya kuhukum?? wewe mwenyewe si mkweli aslaani hivi kumwita mwenzako mnafiki huoni haya??
 
Unafiki katika Uislamu hugawanyika katika sehemu mbili:
1-Nifaaq Amaliy (unafiki wa kivitendo)
2-Nifaaq Iitiqadiy (Unafiki wa kiitikadi)

Unafiki wa kivitendo haumtoi mtu katika Uislamu.
Mfano Muislamu anayemuamini Allah na Mtume wake lakini anafanya mambo yale matatu (riwaya nyingine manne) basi huyu ni mnafiki wa vitendo (Uislamu wake anabakia nao)

Ama mnafiki wa Kiitikadi (Audhubillaah) huyu ni yule ambaye kidhahiri anajionyesha kuwa ni Muislamu lakini kiundani hauamini Uislam.
Huyu ni kafiri zaidi kuliko kafiri anayedhwihirisha ukafiri wake.

Kabla ya kuangalia hukmu ya mnafiki katika Uislamu, je wewe unaamini kuwa Sheikh Jongo ni mnafiki wa kivitendo au wa kiitikadi?

*Binafsi maadamu sijui chochote kuhusu undani wake kuhusu unafiki basi ninamchukulia kuwa ni mnafiki wa kivitendo.
 
Tabaan, kwa alichokionesha pale BMK ni dhahir kuwa Jongo ni mnafik wa kivitendo.
 
kwa hiyo wewe ndio umejitwisha mamlaka ya kuhukum?? wewe mwenyewe si mkweli aslaani hivi kumwita mwenzako mnafiki huoni haya??

Hiyo siyo hukum. Kinachotakiwa aombe toba kwa mola wake kabla hukum haijampitikia.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Uhuru wa Tanganyika haukupiganiwa kwa misingi ya dini; watanganyika wote bila kujali imani ya dini zao walishiriki; wapo waislamu; wakristo na wapagani; hakukuwa na mchango ambao ulitikana na misingi ya kidini; hizo historia zenu za magumashi tafuteni wa kuwaongopea; babu yangu ni muislamu alishiriki katika za kutafuta uhuru sio kwa misingi ya imani ya kidini bali kwa utanganyika wake ndio maana watu walishirikiana katika harakati zile bila kujali dini zao.

Usilolijuwa ni usiku wa kiza. Muislaam chochote anachokipigania, kwanza huwa ni kwa dini yake. Kama anapigania "uhuru" kwa ajili anabanwa katika kuutimiza wajibu wake wa Kiislam basi ujuwe hapo ni moja kwa moja kaupigania Uhuru ili aishi kama Muislam anavyotakiwa kuishi katika Uislam.

Utaupigania uhuru kama uko huru? fikiri!
 
  • Thanks
Reactions: prs
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom