Sheikh Jongo bado ana mengi ya kujifunza

Status
Not open for further replies.
Ndahani,
Naamini unajua nani anatajwa kila wanapoikumbuka Auschwitz.

Vipi na huyo umemtia katika orodha yako?

Kwahiyo Nyerere anafanana na wale watu waliotengeneza Auschwitz? Hii ya leo mbona kali! Kwa mara ya kwanza naisikia toka kwako. Kwa bahati mbaya hata hizi attack kwa Shekhe Jongo ni kwa sababu hataki kufikiri kama unavyofikiria wewe. Kama mtanzania ninayeipenda nchi yangu, siamini kabisa katika udini tunaopenda kuutukuza mana dini yangu ni yangu inakuhusu nini wewe? Kinachinipa faraja ni kwamba kwa ujumla wake, watu wenye fikra hizi za itikadi za kidini wako kiduchu, na wanatapatapa tu. Tulio wengi tunaona mbali kuliko tamaa ambazo Mwenyezi Mungu aliye mwema kamwe hatazipa nafasi....tamaa za baadhi ya watu kutaka kulazimisha kile wanachokiamini kiwe lazima kwa watu wote?
 
Sheikh Kassim alipewa sumu wazi wazi na hata alipopelekwa kwa matibabu uswisi familia iliambiwa hivyo lazima angefariki kwa sumu ile.Kazi ya Augustino Mrema
Lakini yeye alikua anamwaga sumu ndani ya jamii waziwazi tofauti na madai yenu ya kubuniwa.
 
huu uzi umeekaa kihafidhina kuleta chuki kwa baba wa taifa kwa kupanda mbegu ya fitna kwa waislamu wenzako this is true fallacy inayoitwa beg the question.kuna watu kama ninyi mohamedi said wenye mlengo wa kushoto wa kuwaaminisha waaslimu wamenyanyasika na kuonewa kumbe ufalme unaofitinika hautasimama.meza nzima nzima bila kutema,mawazo ya ukakasi kwa jamii ya mazonge kama ninyi mtaishia kulament
Unaonaje ukijibu facts (unazoziita fitna au true fallacy) za mtoa mada kwa facts za uhakika? Je hao anaowataja kwenye mada yake hawajawahi kuwepo? Je hawakushiriki kwenye harakati za uhuru? Je hawakumsaidia Mwalimu kwenye harakati za uhuru? Je hakuna majina mengine ya walioshiriki kwenye harakati za uhuru ambao hawatajwi kwenye historia? Kwa nini majina haya hatukuwahi kuyasikia kwenye simulizi rasmi za harakati za kupigania uhuru zilizokuwa zikifundishwa mashuleni? Just curious!!!
 
Video za kususia kuswali nyuma ya Sheikh Jongo zinazasambazwa kwenye WhatsApp nimeipata moja msemaji katika macho yangu anaonekana kuwa ni yule Daaiyah maarufu anayelingania kupitia Biblia.

Katika hali kama hii toba ya Sheikh Jongo inatakiwa aifanyie hadharani ili kila Muislamu aujue msimamo wake mpya...

Mkuu.

Nimeipata pia, kuna ndugu (ZNZ) wameiwekea na surat al munafiqun halafu wakamalizia na ile hadithi ya mtume (SAW) inayo zungumzia alama za Mnafiki. Hata mtoto mdogo akiangalia na kumuona jinsi sheikh Jongo anavyo bubujikwa na machozi ya kinafiki akasikiliza na aya na hiyo hadithi, akitoka hapo akikutana nae mtaani badala ya kumuita sheikh Jongo atamuita sheikh Mnafiki.

Hii ina mhusu

63_3.png


Inakwenda na hiki kipande cha hadithi

Mtume kipenzi cha Mwenyezi Mungu (SAW) ametufundisha kuwa mnafiki ni mtu mwenye nyuso mbili (ndani yake na nje yake ni tofauti) na alama zake ni tatu. alama tatu kwa mujibu wa Muhammad (SAW):

(1) Akizungumza husema uongo,(2) Akiahidi hatimizi (3) Akiaminiwa hufanya khiyana.

Mtu huanza kwa kusema uongo mmoja kisha akafuatilia kwa kusema mwengine kupita wa kwanza na akaendelea hata mwisho uongo hugeuka kuwa ndio tabia yake au chakula chake na hapo ndipo anapoitwa ‘mwongo'.

Uongo ni tabia mbaya sana hata Mtume wa Mwenyezi Mungu (SAW) aliwahi kusema kuwa; ‘Muislamu hasemi uongo.' Na maana yake ni kuwa; mtu aliyekamilika imani hawezi kusema uongo.

Kwa kumuangalia sheikh Jongo kwa aya na hiyo hadithi utaishilia kusema "....Sheikh Jongo is a hypocracy of the highiest order" kwa kuwa wengi tulikuwa tunamuona kuwa ni sheikh aliyekamilika imani na ambaye anaweza kuisimamia kweli iliyo dhahiri, lakini nani anaweza kuthubutu kusema sheikh Jongo alikuwa analia kiukweli kwa kuwa waasisi wametukanwa?! Nani anaweza kusema kuwa Sheikh Jongo yuko mjengoni kuwakilisha maoni na maono ya taasisi anayotoka?!

Nani anaweza kumuamini akimuona anatokwa na machozi akikutwa na jambo litakalo mfanya machozi yatoke na akasadiki kuwa anatokwa na machozi ya kweli na si machozi ya uwongo kama alivyolia kwa uwongo na ghafla akanyamaza na kuendelea kuchangia na akapigiwa na makofi na vigelegele?!

 
Mungu aliwanusuru hawa,aliwapa upeo wa ziada-hawakuishia madrasatul waliendelea na skuli/vyuo na matunda tunayaona,wanaijua keyboard
we Son of Alaska umemsahau yule mmoja aliyeenda kuomba viza ya Uingereza ubalozini amevaa kanzu na kobazi alikuwa pamoja na mwenzake aliyepiga suti lakini akanyimwa viza yule mwenye suti akapewa yeye shariff, sasa sikuhizi nasikia viza unaipatia Nairobi ya Uingereza, sasa sijajua kama na huko ataenda na Kanzu na Kobazi pia na yeye keyboard ha,pigi chenga sana...

Bila kumsahau yule dada mwingine mwenye uraia wa Canada akija Tanzania anauachia Nairobi halafu anaingia Tanzania kwa sababu Tanzania hawaruhusu uraia wa nchi mbili hiyo ni ya siriwazi au uwazi wa siri na yeye pia keyboard haimpigi chenga...
 
Last edited by a moderator:
Sasa unanipa cheo cha utatu ambacho sikikubali, hicho mmempachika mmoja tu nae atakuja kuwasuta.

Bado hoja zako za Udini zinaendelea...Mimi siwezi na sio mfuasi wa hizo propaganda! mimi ni Mtanganyika na naitaka Tanganyika..
 
Haiwezekani!
Angekuwa mmanyema, jamaa asingemwandika vibaya hapa, angeminya tu.

Asante kaka ilikuwa ni swali la uchokozi tu, Jongo ni jina la Kindengereko na palikuwa na uhasama sana miaka ya nyumba kati ya Wamanyema/Wazulu na hao Wandengereko/ Wamatumbi
 
we Son of Alaska umemsahau yule mmoja aliyeenda kuomba viza ya Uingereza ubalozini amevaa kanzu na kobazi alikuwa pamoja na mwenzake aliyepiga suti lakini akanyimwa viza yule mwenye suti akapewa yeye shariff, sasa sikuhizi nasikia viza unaipatia Nairobi ya Uingereza, sasa sijajua kama na huko ataenda na Kanzu na Kobazi pia na yeye keyboard ha,pigi chenga sana...

Bila kumsahau yule dada mwingine mwenye uraia wa Canada akija Tanzania anauachia Nairobi halafu anaingia Tanzania kwa sababu Tanzania hawaruhusu uraia wa nchi mbili hiyo ni ya siriwazi au uwazi wa siri na yeye pia keyboard haimpigi chenga...
HUYU alienda VIZA ubalozini akiwa kavaa kobazi simkumbuki lakini nahisi ni@Ritz, huyu hana substance,ni mtupu,yeye ufuta upepo unavuma wapi basi uelekea hukohuko irrespective of the consqences
 
HUYU alienda VIZA ubalozini akiwa kavaa kobazi simkumbuki lakini nahisi ni@Ritz, huyu hana substance,ni mtupu,yeye ufuta upepo unavuma wapi basi uelekea hukohuko irrespective of the consqences
upo sawa kabisa wala hujakosea mkuu Son of Alaska huyo si mwingine bali ni shariff Ritz
 
Last edited by a moderator:
Kumbe hujaona hata kilio chake cha kinafik pale bungeni? sasa ndugu yangu si utazame kwanza mkanda wake ujionee mwenyewe? kumbe unabishana kitu hata hujakiona?

Kuhusu CCM, wala usiwe na shaka, mimi mmojawapo ni mwanachama hai wa CCM. Ila kumbuka uanachama wangu wa CCM haunizuwii nikiliona baya au lisilopendezesha kutoka kwa mwana CCM mwingine basi nilifumbie macho kwa kuwa eti mimi ni CCM. Hiyo kwangu na kwa wengi haiendi.

Ndiyo maana sikupendezewa hata William Lukuvi alipokwenda kutugawa kidini pale Kanisani na nimefungua nyuzi humuhumu JF kwa hilo.

Umejuaje kama kilio cha sheikh Jongo cha kinafiki??? hivi mtu kuonyesha hisia zake ni unafiki?? kauli alizotoa mh. Lukuvi si sahihi alilenga kwenye kuimarisha muungano lakini hakuchagua maneno mazuri hilo nakubaliana na wewe; lakini kwa sheikh Jongo kidogo sitakubaliana na wewe zile ni hisia tu sheikh inaonekana ni mwanaCCM hakufanya lolote baya la kuwaudhi waislamu au muumini wa dini yoyote.
 
acha kuhukumu watu huo pekee ni unafiki! kamanda Mohamedi Mtoi jiangalie kwenye halafu urudi jamvini uone kama na wewe utasalimika kwenye unafiki
 
Last edited by a moderator:
Hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!!!!!!!!!

CattleRustler,
Hakika utamu unakolea...
Kwa maana uongo umetoweka na kweli imedhihiri:

Gazeti la An-nuur linalotoka kila siku ya Ijumaa
ukurasa wa mbele limeandika kwa wino ulikoza
kibwagizo hiki:

''Sheikh Jongo ajifunze hawana shukrani hawa

Labda uritadi kama ilivyosema Qur'an

Asome kutoka kwa Suleiman Takadir.''

WAZEE+WA+TANU.jpg
Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine Hawapo)


  1. [*=center]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=center]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=center]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=center]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=center]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=center]Julius Nyerere (Minaki Sekondari)
    [*=center]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=center]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=center]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=center]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=center]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=center]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=center]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=center]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=center]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=center]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=center]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=center]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=center]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo)
​
Wazee hawa walifukuzwa TANU mithili ya mbwa na wao ka ustaarabu wa watu wa pwani hawakufanya tabu walijirudia majumbani mwao na na hawakutia mguu tena pale ofisi ya TANU Mtaa wa Lumumba. Mmoja baada ya mwingine walikufa na si Nyerere wala TANU ilikuwa na habarinao. Walikuwa sawa na ganda la muwa au mgomba baada ya ndizi kukatwa.

Nakuwekea hapa chini kisa chao:

''Tarehe 11 Machi, 1963, Kamati Kuu ya TANU iliyokutana Dar es Salaam ilipiga kura kuvunja kamati ya wajumbe kumi na moja ya Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti wake Idd Tulio. Wazee walikusanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na wakasomewa uamuzi wa Kamati Kuu ya kulivunja Baraza la Wazee. Taarifa ilisema wazee hao ni kero kwa sababu ''dini na siasa vilikuwa vitu viwili tofauti na hawa wazee walikuwa wanachanganya dini na siasa.'' Hiki kilikuwa chombo cha ushauri ambacho wajumbe wake wote walikuwa Waislam; chombo kilichokuwa ndani ya TANU ambacho kilimuunga mkono Nyerere na TANU tangu siku za mwanzo kabisa, kwanza chini ya uongozi wa Sheikh Suleiman Takadir na kisha chini ya Idd Tulio baada ya kufukuzwa kwa Sheikh Takadir kutoka TANU. Wakati haya yote yakitendeka Kanisa ambalo wakati wa kudai uhuru lilijiweka mbali na halikutoa msaada wowote sasa likawa linanyemelea kujiingiza katika siasa likiwa na agenda yake: kuwaweka viongozi Wakristo katika nafasi za uongozi na kuutoa nje ya uongozi Waislam ambao Kanisa liliwaona hawana elimu. Jumuiya za Kiislam kama Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na EAMWS zilikuwa sasa zinapigwa vita na serikali ya Nyerere kama vyombo ambavyo havikuwa na umuhimu wowote katika Tanganyika mpya. Katika kumuhakikishia utiifu wao juu yake, Waislam walijitahidi mwisho wa uwezo wao kuziweka taasisi zao kando na chuki za kidini dhidi ya Wakristo. Juhudi hizi hazikuthaminiwa. Serikali ilifanya juhudi za siri kuhakikisha kuwa jumuiya zote za Waislam zinapigwa marufuku.Huu ndiyo ukawa mwanzo wa kampeni za kufuta historia ya Uislam katika TANU na mwisho wa Waislam kuwa na sauti katika siasa baada ya uhuru kupatikana. Baada ya kupatikana kwa uhuru, ile nguvu ya Waislam iliyotumika kupambana na Waingereza kuleta uhuru, ikaonekana haina maana yoyote na haifai kitu tena. Kuvunjwa kwa Baraza la Wazee ndiyo ilikuwa kishiko cha mwisho cha Waislam katika TANU. Baada ya hapo Kanisa lililokuwa pembeni wakati wa kudai uhuru sasa likajitokeza waziwazi kuwapiga vita Waislam katika TANU.''
 
Umejuaje kama kilio cha sheikh Jongo cha kinafiki??? hivi mtu kuonyesha hisia zake ni unafiki?? kauli alizotoa mh. Lukuvi si sahihi alilenga kwenye kuimarisha muungano lakini hakuchagua maneno mazuri hilo nakubaliana na wewe; lakini kwa sheikh Jongo kidogo sitakubaliana na wewe zile ni hisia tu sheikh inaonekana ni mwanaCCM hakufanya lolote baya la kuwaudhi waislamu au muumini wa dini yoyote.

Khaa, kumlilia khaini aliyeupiga vita Uislaam, aliyewafunga, kuwahamisha na kuwanyamazisha ismu ya Masheikh wakati wake, leo unasema siyo unafik? Amma kwa hakika, mwenye macho haambiwi tazama mwenye masikio haambiwi sikia.

Hivi historia uliyopewa hapo juu umeisoma haswa? na umeelewa kilichoandikwa? unachokipinga ni nini haswa?
 
Khaa, kumlilia khaini alyeupiga vita Uislaam, aliyewafunga, kuwahamisha na kuwanyamzisha ismu ya Masheikh wakati wake, leo unasema siyo unafik? Amma kwa hakika, mwenye macho haambiwi tazama mwenye masikio haambiwi sikia.

Hivi historia uliyopewa hapo juu umeisoma haswa? na umeelewa kilichoandikwa? unachokipinga ni nini haswa?

huo ni mtazamo wako kutokana na mafundisho yako; wapo waislamu wengi sana tunamheshimu Nyerere; kama kweli Nyerere alihamisha watu mbona unazeekea Kariakoo na Dar kwa ujumla??
 
huo ni mtazamo wako kutokana na mafundisho yako; wapo waislamu wengi sana tunamheshimu Nyerere; kama kweli Nyerere alihamisha watu mbona unazeekea Kariakoo na Dar kwa ujumla??

Si mafundisho yangu, kwa niliyoyaona na kuyashuhudia. AlhamduliLlahi nipo kabla ya Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika, nimeiishi awamu yake, nnajuwa tulipotoka, labda wewe ndiyo umehadithiwa tu.

Niliihama Kariakoo na Tanzania kwa ajili ya Nyerere, na si mimi pekee ni wengi sana kama mimi, for your information.
 
  • Thanks
Reactions: prs
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom