Shahidi: Zitto alikataa kuandika maelezo polisi kuhusu watu anaodai waliuawa na Jeshi la Polisi kwenye operesheni mkoani Kigoma

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Mithili ya Kigogo!!

Ndugu Zitto Kabwe alipotakiwa kutoa maelezo ya Ushahidi wa uwepo wa mauaji ya watu yaliyofanywa huko Kigoma alishindwa au kugoma.

Ikumbukwe huu ulikuwa ni mmojawapo wa uzushi wa karne kutoka kwa 'kigogo' huyu wa na Ayatolla wa ACT a.k.a Chama cha kuuma na kupuliza.

CC : Mwanasheria Mwandishi Pascal Mayalla

SOURCE: MAGAZETI YA JANA

=======

MKUU wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, Albert Kitundu (49) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) alikataa kuandika maelezo polisi kuhusu watu anaodai waliuawa na Jeshi la Polisi kwenye operesheni mkoani Kigoma.

Aidha, alidai katika upelelezi walioufanya wakati huo akiwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Kinondoni, alibaini kuwa kilichosemwa na Zitto hakikuwa na ukweli kwani watu waliofariki si 100 kama ilivyodaiwa, bali ni wanne wakiwamo askari polisi wawili.

Mrakibu wa Polisi, Kitundu alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati akitoa ushahidi. Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga, shahidi huyo alidai Zitto alikamatwa na maofisa wa jeshi hilo baada ya kutoa maneno ya uchochezi na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay na kumuhoji kawaida.

Alidai alimuuliza nafasi yake katika chama cha ACT Wazalendo, historia ya maisha yake ikiwamo elimu ambayo aliyaeleza kwa kirefu. Kitundu alidai alipomuuliza kuhusu tuhuma alizozitoa kwa jeshi hilo, alikiri kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi kuhusu watu 100 aliodai wameuawa. “Baada ya kueleza hayo nilimwambia Zitto nataka kumuhoji kama mtuhumiwa ili maelezo yake yaweze kutumika kama kielelezo mahakamani.

Nilimpa haki zake lakini alisema hayuko tayari kutoa maelezo yake polisi na kudai atayatoa mahakamani,” alidai Mrakibu wa Polisi Kitundu.

Alidai walimuomba taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwapatia. Kuhusu upelelezi wa tuhuma hizo, shahidi huyo alidai aliongoza upelelezi wa tukio hilo kwa kupitia hotuba ya Zitto ambayo mmoja wa maofisa wa polisi aliichukua kwenye mkutano wake ambako walikuta maneno ya kichochezi yalikuwa yanatakiwa kutolewa ufafanuzi na mshitakiwa huyo.

Alidai maneno yaliyotakiwa kutolewa ufafanuzi ni kwamba “polisi limeuwa wananchi wapatao 100 na waliokwenda kutibiwa katika Zahanati ya Nguruka, polisi walichukua majeruhi na kuwaua.”

Chanzo: Habari leo
 
Pelekeni tume huru ikawaulize wale Wasukuma ni kitu gani walifanyiwa.
 
Kwa hiyo mbilikimo hawana akili?

Sidhani kama maana ilikuwa mbilikimo hawana akili. Nafikiri anamaanisha akili 'fupi' kama mbilikimo.
Lakini hata hivyo mimi binafsi sioni kama ni sawa kutumia msemo kama huu kwani unaweza kupotosha maana na kuwaudhi watu.
 
Sidhani kama maana ilikuwa mbilikimo hawana akili. Nafikiri anamaanisha akili 'fupi' kama mbilikimo.
Lakini hata hivyo mimi binafsi sioni kama ni sawa kutumia msemo kama huu kwani unaweza kupotosha maana na kuwaudhi watu.

Alipaswa kusema akili mbilikimo, na sio huo upuuzi aliposema huyo dogo, kwamba uwe akili kama mbilikimo.
 
Mithili ya Kigogo!!

Ndugu Zitto Kabwe alipotakiwa kutoa maelezo ya Ushahidi wa uwepo wa mauaji ya watu yaliyofanywa huko Kigoma alishindwa au kugoma.

CC : Mwanasheria Mwandishi Pascal Mayalla

SOURCE: MAGAZETI YA JANA
Chanzo: Habari leo
Asante kwa taarifa,
Usikute mimi pia ni miongoni mwa waliomponza Zitto, maana niliwahi kushauri hivi

P
 
Asante kwa taarifa,
Usikute mimi pia ni miongoni mwa waliomponza Zitto, maana niliwahi kushauri hivi

P
Kuhusu wewe mbona yamesemwa mengi mkuu Pascal!!! Eti pia yule ripota wa The Economist wewe ndio ulimuunguza kwenye mamlaka
 
Zitto ana alili sana ila jeshi lilishavuliwa nguo and likagoma kuchutama... japo sheria ipo wazi kuwa ukimuua polosi umetangaza vita hivyo jeshi lina haki yake kulipa kisasi vitani
 
Back
Top Bottom