Shafii Dauda na Dahuu wateuliwa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Dar es Salaam

Ila hata Kama CCM imechoka itamteua Lucas Mwashamba kwenye kitengo gani?. Lazima tuwe wa kweli. Labda ateuliwe kwenye kitengo Cha kuosha na kutunza mbwa wa mawaziri.
Ila huyu Mwashambwa kawa mwiba mkali kwa CHADEMA tawi la JF.
 
Hebu angalia mchango wa hawa halafu fananisha na kipara kipya au Kamanda Asiyechoka

View attachment 2846603

Hawa eti wameteuliwa kwenye Jumuiya ya Wazazi , huku Magonjwa Mtambuka na Lucas mwashambwa wametoswa !

Hata hivyo sisi wengine tulishaonya mapema sana kwamba CCM ina wenyewe, lakini hatukueleweka.

========

Shafii Dauda ateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo, utamaduni na Mazingira ya Jumuiya ya wazazi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo Baraza la wazazi mkoa laridhia uteuzi wa wa mjumbe huyo, baraza liliofanyika chini ya Mwenyekiti ced Khadija Ally Said katika ukumbi wa Iddi Nyundo manispaa ya Temeke na Mgeni Rasmi akiwa Prof Adolf Mkenda Waziri Wa Elimu Sayansi na Teknolojia.

Pia baraza limemteua Husna Abdul maarufu kama Dahuu kuwa mjumbe wa kamati ya habari na mawasiliano ya Jumuiya ya wazazi mkoa wa DSM.
Tunakushukuru sana kwa kuendelea kutupatia taarifa za mambo mazuri yanayoendelea kwenye chama pendwa CCM. Hakika unakitendea haki chama chako cha watoa taarifa. Endelea na moyo huohuo wa kutuhabarisha kuhusu CCM.
 
Back
Top Bottom