Shaffih Dauda na Wachambuzi wengi wamejipatia fedha nyingi kwa utapeli wa uchambuzi

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe, tusichoshane!.

Miaka ya nyuma hawa watu walioitwa wachambuzi wa kandanda akiwemo Shaffih Dauda na wenzie wametupiga sana ndoige kuhusu Kandanda na historia yake ni kwasababu miaka hiyo watanzania wengi walikuwa wavivu kusoma na kutafuta maarifa zaidi yanayohusu soka, kitu kingine pia ilikuwa ni ufinyu wa teknolojia ikiwemo ukosefu wa luninga,ukosefu wa simu janja pamoja na ukosefu wa kimtandao(Internet).


Watanzania wa leo si wa miaka 15 iliyopita kwasababu sasa hivi kuna kila aina ya miundombinu(Facilities)za kupata taarifa kwa urahisi na kurahisisha usomaji.

Sasa wachambuzi wengi wanadhani watanzania wa leo ni mazumbukuku kama wa miaka 15 - 20 iliyopita.

Hii imepelekea wachambuzi wengi wa kandanda walio sahihi na wasio sahihi kupewa jina linalosadifu uhalisia wao "WACHAMBUZI WA MICHONGO".


Kitendo cha Shaffih Dauda kusema ya kwamba "Emiliano Martinez ndiye goli kipa wa kwanza kutoka America kusini kushinda tuzo ya goli kipa bora wa kombe la dunia" kimenisikitisha sana na kuwaza mambo mengi sana kuhusu huyu jamaa na wachambuzi wengine niliyowaamini na bila shaka watanzania wengi wapenda soka watakuwa walishangaa sana na kutoamini kama kweli ni yeye ndiye aliyetoa ile posti.

Shaffih Dauda kama mchambuzi nguli wa kabumbu hapa nchini alijizolea umaarufu hadi kuaminiwa na makampuni makubwa na kuwa balozi wao,ukiachana na mambo ya ubalozi pia aliweza kuwashawishi wadau mbalimbali kudhamini michuano ya ndondo cup ambako huko amejipatia mipesa ya kutosha.

Sasa nilichogundua ni kwamba,hawa wachambuzi wa miaka hiyo akiwemo Shaffih Dauda mwenyewe, walitudanganya sana kwasababu watanzania wengi tulikuwa si wafuatilia mambo na kujikuta tunavutiwa nao tukiamini wanalifahamu soka kumbe ilikuwa sivyo!.

Kitendo cha Shaffih Dauda kukosolewa hadharani na mpigania haki Malisa kinaonyesha namna ambavyo jamaa halijui soka bali ni kanjanja,hivi ni kweli kabisa Shaffih hili halikuwa halifahamu mpaka kufahamishwa na mtu ambaye uchambuzi wa soka si kazi yake?,hivi kweli kwa teknolojia ya leo alishindwa hata ku-google ili kuhalalisha uchambuzi wake?,au ni mapenzi na mahaba ya Emiliano Martnez ndiyo yalifanya aposti ule ujinga.

Hiki kitendo kimefichua mambo mengi sana kwa jamaa na tafsiri yake ni kwamba,hata hapo Clouds ashukuru miaka hiyo anapata ajira bado wabongo wengi walikuwa vilaza kwenye masuala ya soka, kupitia uongo wake jamaa leo amejipatia maisha mazuri sana.

Kibaya zaidi bado anataka kuendeleza uongo kwenye dunia ambayo imejaa wasomi,wafuatilia mambo na watu makini katika soka,akiendelea na ujinga huu katika dunia ya watu wanaojua zaidi yake ataumbuka kwa ukanjanja wake.


Ni hayo tu.
 
Kama unamfatilia vizuri Shafii Dauda utagundua hiyo sio taarifa yake ya kwanza kukosea

Huwa najiuliza hizi takwimu huwa anazitoa kichwani mwake kupitia kumbukumbu au huwa anazipitia kuhakiki katika site za mitandao ambayo imekuwa maalumu kwa ajili ya data hizo?
 
Kama unamfatilia vizuri Shafii Dauda utagundua hiyo sio taarifa yake ya kwanza kukosea

Huwa najiuliza hizi takwimu huwa anazitoa kichwani mwake kupitia kumbukumbu au huwa anazipitia kuhakiki katika site za mitandao ambayo imekuwa maalumu kwa ajili ya data hizo?
Sipingi kwamba hawezi kosea,Ila nahisi shafi hiyo page Kuna vijana kawaajiri
 
Wachambuzi wengi aiseee ni hamna kitu ukitaka kujua hilo angalia ligi mabingwa africa ? Wachambuzi wanaenda kugoogle timu inayocheza na simba au yanga then wanakuja na maelezo yao basi wabongo tunawaona wako vizur sana kisa wanaongezea maneno kama double pivot, 4,4,2 diamond,

Kiufupi hakuna wachambuzi tz yan hapo wasafi ndio hamna kitu lakin ndio mtu ana acha mise zake anasikiliza sports arena.
 
Hahaa...ukishaangalia Sky Sports inatosha..
Labda kama unataka kusikiliza Bongo hapa..angalia Mpira pita hivi..achana na uchambuzi huu wa kuunga unga.
 
Kati ya Maulid kitenge au yeye mwenyewe Shafii Dauda aliwahi kukutana na msala wa kusambaza taarifa ya uongo, utetezi wake ulikuwa sio yeye bali ni vijana waliokuwa wana monitor hiyo page..
Ni kweli,hao jamaa wapo bize
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom