EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Bunge limeidhinisha Sh. milioni 300 kwa ajili ya kununua magari mawili ya serikali. Uidhinishwaji huo umefanywa muda mfupi baada ya serikali kudai kuwa imesitisha kununua magari ya starehe na gharama kubwa ili kupunguza matumizi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina Kombani, amesema kuwa fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kununua magari mawili kwa sababu kuna uhaba wa magari.
Hata hivyo, Bunge limeishinisha fedha hizo bila kuhoji madai ya serikali kupunguza matumizi ya anasa. Juhudi za wabunge wa upinzani kupinga matumizi hayo ziligonga mwamba kutokana wingi wa wabunge wa chama tawala walioidhinisha matumizi ya fedha hizo.
Inadaiwa kuwa Sh. milioni 300 zilizoidhinishwa na Bunge kununulia magari hayo mawili zinaweza kununua matrekta sita kwa ajili ya kuwasaidia wakulima na pia kujenga madarasa matano ya shule za msingi.