Sh 11.6 trilioni zapotea kifisadi

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Na Mwandishi Wetu

TANZANIA imeshapoteza Sh11.6 trilioni, ikiwa ni wastani wa Sh289.3 bilioni kila mwaka kutokana na ufisadi, ukwepaji kodi na mzunguko wa fedha haramu, kwa mujibu wa matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi moja ya Marekani.Fedha hizo ni mara mbili ya fedha zilizoibwa kutoka kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika kipindi cha mwaka 2005/06.

Taarifa hiyo ya taasisi ya Global Financial Integrity yenye kichwa cha habari kisemacho:

"Illicity Financial Flows from Africa: Hidden Resources for Development (Mtiririko Haramu wa Kifedha Kutoka Afrika:Rasilimali za Maendeleo Zilizojificha)", imesema katika utafiti huo kuwa fedha hizo zimekuwa zikipotea kwa miongo minne na hivyo kufanya fedha zote zilizopotea katika kipindi hicho cha miaka 40 kufikia Sh11.6 trilioni, au kwa maneno mengine Sh11,000 bilioni.

Kwa mujibu wa utafiti huo ulioripotiwa na gazeti la The East African toleo namba 807 la Aprili 19 hadi 25 mwaka huu, utafiti huo ulifanywa na timu ya uangalizi wa fedha ya Marekani katika maeneo ya mzunguko wa fedha haramu, ukwepaji wa kodi, ufisadi serikalini na shughuili nyingine haramu.

Utafiti umeonyesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupoteza fedha katika maeneo hayo kwa nchi za Afrika Mashariki, ikifuatiwa na Kenya iliyopoteza dola 7.3 bilioni za Kimarekani(sawa na Sh9.5 trilioni za Kitanzania) na Uganda iliyopoteza dola 6.4bilioni za Kimare

kani ambazo ni sawa na Sh 8.32 trilioni.Mahesabu yaliyofanywa kulingana na matokeo ya utafiti huo yanaonyesha kuwa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki, zimepoteza dola za Marekani 22.6 bilioni, sawa na Sh29.4 trilioni katika kipindi hicho.

Utafiti huo umeeleza kuwa madhara ya kupotea fedha hizo, yanawaumiza wananchi wengi katika nchi hizo ambazo zote ni masikini.

Ripoti imeonyesha pia kuwa Tanzania inashika nafasi ya 13 kati ya nchi 15 zinazoongoza kwa matumizi haramu ya fedha baada ya Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Cameroon, Ivory Coast, Ethiopia, Gabon, Ghana, Madagascar, Msumbiji, Nigeria, Afrika Kusini na Sudan. Zambia na Zimbabwe zinashika nafasi ya 14 na 15.

Hata hivyo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo aliliambia gazeti hilo la The East African kuwa serikali imeanzisha kitengo cha intelijensia ya fedha kuongoza mapambano dhidi ya mzunguko wa fedha haramu nchini.

"Tatizo hili lipo, katika ngazi ya taifa na ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC), tumeliona hili tatizo kwa muda mrefu na tumeamua kuungana kupambana nalo," alisema Mkulo.

Msemaji wa Global Financial Integrity ameeleza kuwa kiasi cha fedha kilichopotezwa na nchi hizo tatu kinaweza kuwa zaidi ya mara mbili ya Sh29.4 trilioni kama njia nyingine haramu zingetajwa kwenye ripoti hiyo.

Utafiti huo unaonyesha kuwa rushwa na wizi unaohusisha wafanyakazi wa serikali unachangia asilimia tatu ya matumizi haramu ya fedha zinazovuka mipaka.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa nchi za Afrika pekee hupoteza dola 854 bilioni za Kimarekani kwa matumizi haramu, huku nchi tano zinazoongoza zikiwa ni Nigeria (dola 89.5 bilioni), Misri (dola 70.5 bilioni), Algeria (dola 25.7 bilioni), Morocco (dola 25 bilioni) na Afrika Kusini (dola 24.9 bilioni).

Source: Mwananchi
 
Matatizo ya upotevu wa fweza yataisha watanzania watakapoizika CCM.
 
Nawashauri CCJ waliangalie hili, watakapokuja madarakani wapitishe sheria ya kifo kwa watu hawa wanaoifukarisha nchi, ambayo idadi yao ni asilimia 0.000001 tu ya wananchi wote! Kuna watakaosikitika wakila shaba hawa!
 
Back
Top Bottom