Serikali: Zaidi ya Wanafunzi 1,092,000 Kuanza Sekondari Januari 2024

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,774
Hayo yameelezwa na Waziri wa Tamisemi Hommed Mchengerwa wakati Akitoa taarifa ya Watoto Waliofaulu na kupangiwa shule za Sekondari mwaka 2024 tayari kuanza utekelezwaji wa Elimu Kwa mtaala Mpya.

===============

WANAFUNZI 1,092,984 ambao walifaulu mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2023 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2024 huku 1,410 wakipangwa kwenye baadhi ya Shule za Sekondari za mkondo wa Amali za kihandisi ikiwa ni kuanza utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu.

Akizungumza leo Desemba 17,2023 na waandishi wa habari jijini Mwanza, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema kati ya idadi hiyo wasichana ni 585,051 na wavulana 507,933 wamefaulu na kupangiwa katika Shule za Sekondari za Serikali ili waanze masomo ya Kidato cha Kwanza Januari, 2024.

Amesema idadi hiyo inajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 3,587 wakiwamo wasichana 1,590 na wavulana 1,997.

“Wanafunzi waliopangiwa katika shule 48 za bweni za Kitaifa ni 5,606 sawa na asilimia 0.5, katika Shule teule za mikoa ni 17,412 sawa na asilimia 1.6 na Shule 4,566 za Kutwa ni 1,069,966 sawa na asilimia 97.9,” amesema.

Amefafanua kuwa waliochaguliwa shule za wenye ufaulu wa alama za juu ni 942 na watakwenda Shule za sekondari saba ambazo ni Ilboru, Msalato, Kibaha, Kilakala, Mzumbe, Wavulana Tabora na Wasichana Tabora.

“Wanafunzi 1,410 wakiwemo wavulana 1,136 na wasichana 274 wamechaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari tisa za amali za Kihandisi ambazo ni Bwiru Boys, Ifunda, Mwadui, Iyunga, Moshi, Mtwara, Musoma, Tanga na Chato. Idadi hii ya wanafunzi inajumuisha wanafunzi wenye mahitaji maalum 274 wakiwemo wasichana 31 na wavulana 243,”amesema.

Mchengerwa amesema wanafunzi 3,254 wakiwamo wasichana 1,511 na wavulana 1,743 wamechaguliwa kujiunga katika Shule za Sekondari 32 za Bweni za Kitaifa za Kawaida. Idadi hii inajumuisha wanafunzi wenye Mahitaji Maalum 1,629 wakiwemo wasichana 836 na wavulana 793.

Amefafanua kuwa jumla ya Wanafunzi 17,412 wakiwemo Wasichana 7,816 na wavulana 9,596 wamechaguliwa kujiunga na shule za Bweni Teule na zile za wasichana za Mikoa. Shule za wasichana za mikoa saba zimepangiwa wanafunzi wasichana 897 wakijumuishwa wanafunzi wenye mahitaji maalum 116.

TAMISEMI
 
Hongera sana Serikali ya Mama.Miaka michache Iliyopita hao Watoto wangeingia shule Kwa mafungu Hadi mwezi April unakuta form 1 wanakuja 🤣🤣
 
Serikali imeendelea kuwanyanyapaa watoto waliofaulu vizuri zaidi toka English Medium schools..

Wamepelekwa shule za kata za hovyoo
Ulitaka wapelekwe wapi?

Mimi wakwangu mapacha wamemaliza msingi ya serikali na kurwa ana wastani wa A na amepangwa shule ya kutwa ya kata.
Na wapo hapo hapo wenye wastan wa B wamepelekwa bweni.nilishatoa mpaka uthibitisho hapa walikua wanabisha wakabaki midomo wazi baada ya kuona ushahidi.

Tunaishi nayo tu hii serikali lakin kuna mambo inaboronga sana.
 
Ulitaka wapelekwe wapi?

Mimi wakwangu mapacha wamemaliza msingi ya serikali na kurwa ana wastani wa A na amepangwa shule ya kutwa ya kata.
Na wapo hapo hapo wenye wastan wa B wamepelekwa bweni.nilishatoa mpaka uthibitisho hapa walikua wanabisha wakabaki midomo wazi baada ya kuona ushahidi.

Tunaishi nayo tu hii serikali lakin kuna mambo inaboronga sana.
Na amepata A ya hesabu,sayansi.
 
Nini hutokea hadi wengi wao wanashindwa maliza kidato cha nne?
 
Nini hutokea hadi wengi wao wanashindwa maliza kidato cha nne?
Jibu rahis sana,
wengi wanapewa nafasi hizo kwa njia za panya,hivyo kwasababu sio uwezo wao hatimae huishia njiani.
Yupo jamaa yangu miaka ya 99 alipangwa day school wazazi wake wakaja juu kwanin apangwe day ikiwa ana akili sana?wakati huo mimi nipo shule ya bweni ya serikali,wakaminyana wakampeleka bweni ya serikali,unajua kilichompata?mwaka 2003 tunapokea vyeti nikiwa na single digit jamaa alizungusha ziro safi.
Tangu hapo familia yake ilianza kua na heshima na mimi.sasa ivi yupo mjini anauza dagaa nikifika kazin kwake namuachia chenchi.
 
Na yupo mmoja alikua anadanganya watu eti shule za bweni za serikali zipo 38,
Sasa najua anasoma huu uzi naomba apewe hii listi ya shule za serikali za bweni kwa ajili ya kidato cha kwanza.
Screenshot_20240105-123407_Chrome.jpg
 
List moja ina shule 24,zidisha kwa tatu unapata shule 72 sasa yeye anadanganya watu eti shule zipo 38.
 
Back
Top Bottom