Serikali yavunja rekodi ya ukusanyaji mapato na akiba ya dola!

Mie huwa nasema watu humu JF sio great thinkers at all, ni Great Tanker. Kwa mujibu wa Takwimu za TRA mapato mengi hukusanywa mwezi March, June, Sept. na Dec. Hili linatokana na makampuni mengi kulipa zile ‘ Quarterly Provisional Tax’ kutokana na sheria ya kodi Income Tax Act No. 11 ya 2004. Kwa hiyo ni kweli kabisa hizo pesa zimekusanywa na mfanye tafiti sio kujibu humu kibubusa tu

Kama usemalo ni kweli mbona tunaelezwa mwezi january???? wewe ndiyo una matatizo Quarter ya kwanza umesema ni march je huu mwezi gani.Tunajadili makusanyo ya january mjomba.Fikiri kabla hujaandika
 
Yaweza kuwa kweli (i also doubt) ila kwa sasa CCM wanalipa madeni ya hela walizochukua kwa ajili ya kampeni.....mishahara itasubiri kidogo......:coffee:
 
Huo ni uongo mtupu HABARI LEO IMEJAA MAKANJANJA yanaandika kwa ajili ya njaa, hata arrears ya mishahara ya mwaka jana (nyongeza) maofisi kibao hayajalipwa sasa wanazusha eti wamevunja record uongo mtupu!!
 
Hizo hela zinaenda wapi? mbona hatuoni matunda yake.
Walishatuambia pia kuwa Inflation rate imeshuka sana hadi kufikia 5.5%, CPI pia iko chini wakati tumeshuhudia mfumuko wa bei wa kutisha mara tu baada ya kikwete kuapishwa.
Longolongo zao zinaipeleka nchi pabaya.
 
inflation mmeiangalia watanganyika?maana nnachokiona hapo ni mkwere kujicompare na mkapa kwenye makusanyo ya mapato,...mkwere figure zake zinaweza kuwa kubwa lakini in reality inflation ndio inakuza figure hiyo at the end of the day ni kama makusanyo zero..
 
Tatizo kwa mtazamo wangu, figure zile zimetolwa ili angalau kuziba midomo watu maana 575 bill ni kubwa kutamka lakini matumizi ya serikali kwa mwezi bado hawayasema ili tuweze kulingalinisha deficit ni kiasi gani. Ndiyo maana nasema jambo hili limekuja kisiasa zaidi.
 
Mie huwa nasema watu humu JF sio great thinkers at all, ni Great Tanker. Kwa mujibu wa Takwimu za TRA mapato mengi hukusanywa mwezi March, June, Sept. na Dec. Hili linatokana na makampuni mengi kulipa zile ‘ Quarterly Provisional Tax’ kutokana na sheria ya kodi Income Tax Act No. 11 ya 2004. Kwa hiyo ni kweli kabisa hizo pesa zimekusanywa na mfanye tafiti sio kujibu humu kibubusa tu

True genius!
 
Kama usemalo ni kweli mbona tunaelezwa mwezi january???? wewe ndiyo una matatizo Quarter ya kwanza umesema ni march je huu mwezi gani.Tunajadili makusanyo ya january mjomba.Fikiri kabla hujaandika

Makusanyo ya January hawawezi kuyatangaza leo, hayo subiri mwisho wa mwezi Feb! Kama wanaubuvu basi watutangazie kila mwezi na waseme wametumia kiasi gani na kwa ajiri gani
 
Uchumi wa nchi haukuzwi kwa kua na reserve au saving kubwa au ukusanyaji wa mapato kwa kiasi kikubwa!!!
ILA....
Kwa kufanya allocation ya saving kwenda kwenye investment ambazo ni productive na sustainable.....Kuwa na saving kubwa kuna madhara mengi kwenye uchumi kama vile kufa kwa demand of goods and services maana watu wanakua hawa consume due to lack of purchasing power....and later viwanda vitazidi kufa maana vitashindwa kujiendesha kwa faida.

Pia ukusanyaji wa kodi kwa kiasi kikubwa bila kuzingatia maadhara yake kwenye ukuaji wa uchumi mchanga kama tanzania ni hatari kubwa maana badae small industries zitashindwa kujiendesha then miaka ijayo mtakosa vyanzo vya mapato.

Hatuhitaji kusikia ukusanyaji au uwepo wa reserve kubwa ya foreign currency......lah!! ila tunataka kuona ni jinsi gani serikali inatengeneza fursa kwa wananchi wake waweze ku invest na kukuza uchumi...kama vile uwepo wa nishati ya uhakika na uboreshaji wa miundo mbinu.

SASA WAMETUTANGAZIA HAYO ILI KINA NANII WAKAKWAPUE KAMA ZILE ZA EPA AU????
 
Wana JF kuna habari katika gazeti la habari leo linalosema kuwa serikali ya JK imevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato mwezi Dec, 2010 kwa kukusanya 587bill kati ya malengo ya 570bill na huku ikionyesha kuwa saizi serikali ina akiba ya dola 3.8bill, kiwango hiki ni kikubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa sasa.
Hoja yangu iko hapa, kama ni kweli basi serikali ya JK inahitaji pongezi kwa kazi nzuri iliyofanya lakini inahitaji kuthamini hasa mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na kushuka kwa thamani ya Tshs ambayo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kuwa ghali zaidi hususani mafuta ambayo yanamekuwa yakipanda kila kukicha.
Athari ya kupanda kwa mafuta kutokana na kushuka kwa Tshs kuna dirct impact kwenye ongezeko la bei ambalo ndilo kilio cha wananchi wengi kwa sasa.
Hakuna haja ya kujisifu kwenye makaratasi wakati hali halisi ni mbaya.
Source: HabariLeo | BoT yavunja rekodi akiba ya dola na HabariLeo | TRA yavunja rekodi,yakusanya bil. 580/-.
Nawakilisha kwa mjadala zaidi.

Rula its Possible labda kwa hii mbinu ya kuunda noti mpya, lakini ki-uchumi ni ndoto kutoka wapi wewe unaishi wapi Rula maana kila kitu kipo wazi na kinaonekana huwezi kuongeza mapata bila kuongezeka kwa "Economic activities" kama "Business Activities" na Investments hasa kwenye land wewe umeona wapi ongezeko la Investments na activities au upo vitani Afganstan???!!!
 
Wana JF kuna habari katika gazeti la habari leo linalosema kuwa serikali ya JK imevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato mwezi Dec, 2010 kwa kukusanya 587bill kati ya malengo ya 570bill na huku ikionyesha kuwa saizi serikali ina akiba ya dola 3.8bill, kiwango hiki ni kikubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa sasa.
Hoja yangu iko hapa, kama ni kweli basi serikali ya JK inahitaji pongezi kwa kazi nzuri iliyofanya lakini inahitaji kuthamini hasa mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na kushuka kwa thamani ya Tshs ambayo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kuwa ghali zaidi hususani mafuta ambayo yanamekuwa yakipanda kila kukicha.
Athari ya kupanda kwa mafuta kutokana na kushuka kwa Tshs kuna dirct impact kwenye ongezeko la bei ambalo ndilo kilio cha wananchi wengi kwa sasa.
Hakuna haja ya kujisifu kwenye makaratasi wakati hali halisi ni mbaya.
Source: HabariLeo | BoT yavunja rekodi akiba ya dola na HabariLeo | TRA yavunja rekodi,yakusanya bil. 580/-.
Nawakilisha kwa mjadala zaidi.

Hiyo wamdanganye Matonya si Kingwipa1,
Inawezekanaje ujisifu kuongeza kukusanya mapato wakati hujatueleza source ngapi za mapato umeziongeza?
Kupandisha bei bidhaa mbali mbali kumeongeza kodi na hivyo hakuna chanzo kipya cha mapato ama kuongezeka kwa nguvu ya kukusanya kodi bali ujambazi wa kumkamua mtumiaji wa bidhaa. Ona mafuta, umeme juuu, na kila bidhaa imekwenda juu juuu zaidi tangu kuapishwa kwa JK 2010.
 
Nchi inaongozwa kisaniisanii tu. Kama kuna akiba ya dola kwa nini wasitatue tatizo la umeme nchini? umeme ni nguzo mhimu katika kuimarisha uchumi ndio maana tunaona vitu vimepanda bei baada ya mgawo wa umeme kuongezeka.
 
Sina hakika kama hiyo taarifa ina ukweli wowote, kama kunakuwa na salio kama hilo kwa nini wanazidisha mabakuli kwa wahisani? Inatakiwa kuwepo Independent Institution ambayo inaweza ku-verify hizo info na si kuwaadaha watanzania kwa manufaa ya kisiasa.
 
Wana JF kuna habari katika gazeti la habari leo linalosema kuwa serikali ya JK imevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato mwezi Dec, 2010 kwa kukusanya 587bill kati ya malengo ya 570bill na huku ikionyesha kuwa saizi serikali ina akiba ya dola 3.8bill, kiwango hiki ni kikubwa kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kwa sasa.
Hoja yangu iko hapa, kama ni kweli basi serikali ya JK inahitaji pongezi kwa kazi nzuri iliyofanya lakini inahitaji kuthamini hasa mfumuko wa bei ambao kwa kiasi kikubwa umesababishwa na kushuka kwa thamani ya Tshs ambayo imesababisha uagizaji wa bidhaa kutoka nje kuwa ghali zaidi hususani mafuta ambayo yanamekuwa yakipanda kila kukicha.
Athari ya kupanda kwa mafuta kutokana na kushuka kwa Tshs kuna dirct impact kwenye ongezeko la bei ambalo ndilo kilio cha wananchi wengi kwa sasa.
Hakuna haja ya kujisifu kwenye makaratasi wakati hali halisi ni mbaya.
Source: HabariLeo | BoT yavunja rekodi akiba ya dola na HabariLeo | TRA yavunja rekodi,yakusanya bil. 580/-.
Nawakilisha kwa mjadala zaidi.

Kama hii ni kweli na ipungue basi bei ya mafuta ili viwanda vyetu viongeze uzalishaji na vipunguze bei ya bidhaa inayosababishwa na ongezeko la mafuta na ishindane na bidhaa za kutoka nje, ipungue basi bei ya gesi ya kupikia ili tusiendelee kukata miti kwa matumizi ya kuni na mkaa, yaboreshwe basi mafao ya watumishi katika nyanja zote. ikiwa hivyo hio hadithi nitaiona ya kweli.
 
ukiona habari imetolewa na HABARI LEO pekee basi jua kuna jambo

BTW, ukiangalia na exchange rate baada ya kushuka thamani ya shili unapata how much in terms of dollars?

Naskia hazina imekauka
 
Kuna haja ya BUNGE kutunga sheria ambayo itailazimisha Serikali kila mwezi kutoa taarifa sahihi za mapato na matumizi in detail. Na pia hizo figures ziwe zinahakikiwa independently kama mchangiaji mmoja alivyopendekeza hapa.
 
Ni aibu kujisifia kwa makusanyo hayo wakati nchi inayumba kiasi hiki na hatuna ubora wowote ule tunaoweza kujivunia na kutembea kifua mbele.
 
Hayo madola yasije kuishia kuilipaaDowans na safari za muheshimiwa kwani watanzania wa kawaida maisha bado magumu tu
 
Back
Top Bottom