kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
SERIKALI imetoa pole kwa familia za watu watatu waliouawa katika vurugu za kisiasa mkoani Arusha, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilipolazimisha kufanya maandamano bila kibali cha Polisi.
Pole hiyo imetolewa jana Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati alipofanya mazungumzo na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa.
Membe alisema Serikali inasikitishwa sana na tukio hilo na kutoa pole kwa familia za marehemu pamoja na wote walioguswa na msiba huo na kuwataka Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa na uvumilivu wakati Serikali ikijiandaa kutoa taarifa kwa undani juu ya
kilichotokea.
Pia Membe alizungumzia msimamo wa Tanzania kuhusu kura ya maoni Sudan ya Kusini, migogoro ya kisiasa nchini Cote d'lvoire, Madagascar na Zimbabwe pamoja na tatizo la uharamia katika pwani ya Afrika Mashariki.
Kuhusu kura ya maoni juu ya kujitenga ama kutojitenga kwa Sudan ya Kusini, alisema Tanzania inafuatilia kwa karibu mchakato wake na itaunga mkono matokeo ya kura hiyo.
Alieleza kufurahishwa kwake na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir, kwamba yeye kama kiongozi wa nchi hiyo ataheshimu uamuzi wa watu wa Sudan.
Kuhusu suala la Cote d' lvoire, alisema Tanzania inamuunga mkono Rais aliyeshinda uchaguzi nchini humo, Allassane Outtara na ushiriki wake katika mkutano ujao wa Umoja wa Afrika baadaye mwezi huu.
Membe alieleza kuunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kimataifa katika kutatua mgogoro wa Cote d' lvoire.
Alisema Tanzania inaunga mkono matumizi ya nguvu za kijeshi kumuondoa Rais anayengangania madaraka, Laurent Gbagbo kama juhudi zinazoendelea za kidiplomasia zitashindwa kuzaa matunda.
Kuhusu tatizo la uharamia katika pembe ya pwani ya Somalia na pwani ya Afrika Mashariki na hasa Tanzania, alisema Tanzania imejizatiti kuhakikisha maharamia wanatokomezwa kabisa katika pwani ya Afrika Mashariki.
Alisema mpaka sasa Tanzania imefanya marekebisho ya sheria zake ili kuruhusu maharamia wanaokamatwa katika high seas au Bahari Kuu kushitakiwa katika mahakama za hapa nchini.
Kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Madagascar, Membe alisema hali ya kisiasa ni tete nchini
humo hasa baada ya Katiba ya nchi hiyo kurekebishwa na kupunguza umri wa kugombea nafasi ya urais.
Lengo la mabadiliko hayo alisema ni kumwezesha kiongozi aliyeingia madarakani kinyume na matakwa ya Katiba, Andry Rajoelina kugombea urais.
Membe pia alisema kumezuka mvutano nchini Zimbabwe kati ya Chama tawala cha ZANU-PF na vyama vya upinzani, ikiwemo MDC kuhusu mchakato wa uchaguzi.
Chama tawala kinataka uchaguzi huo ufanyike mwanzoni mwa mwaka huu wakati vyama vya upinzani vikitaka wadau wote wahusike kupanga tarehe ya uchaguzi.
Membe aliomba Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Zimbabwe, ili ijikwamue katika matatizo ya kiuchumi na upatikanaji wa dawa mahospitalini.