Serikali yatoa pole kwa waliouawa Arusha

Kuhusu hilo mbona lipo wazi kabisa kwamba polisi ndio chanzo cha mauaji? Na jumuiya za kimataifa zinatakiwa zitambue kwamba mambo sio shwari kama wanavyoambiwa.

kinachonipa raha kwenye hii serikali ni kila mtu kukurupuka na kauli zake. Atakuja makamba na bintiye Chatanda wataongea lao, Nahodha ataongea lake, Tendwa lake. But napenda nisummarise kwaajili yao, ARUSHA MMEFANYA USANII KWENYE UCHAGUZI WA MEYA
 
....membe hana lolote aafikiri anaweza kuwa rais wa nchi hii ...kaama alifanya kikao na mabalozi alikuwa na haja gani za kutupatia taarifa za ndani za yaliyojadiliwa ......si angeenda kuripoti kwa bosi wake ...anatafuta sifa tu ...
 
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Jeshi la Polisi lilikiuka maadili ya kazi yao, lilipokuwa likikabiliana na raia waliokuwa wakiandamana kupinga suala la uteuzi wa meya wa Arusha.Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na vurugu zilizozuka baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanaandamana jijini Arusha wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwa risasi za moto.

“Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya kazi kwa mipaka ili kuhakikisha kuwa linadumisha amani nchini,” alisema Membe akielezea kuwa ni maoni yake binafsi kuhusiana na tukio hilo linaloelekea kuliwekea doa Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani.

Vurugu hizo zilitokana na Chadema kuamua kuandamana kwa amani licha ya kuwepo na amri ya polisi iliyokuwa inawazuia wakishinikiza uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha urudiwe kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu zilizomsimika Gaudence Lyimo wa CCM kwenye madaraka hayo. Membe alisema kuwa mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini walimbana wakitaka Serikali iweke wazi suala la mauaji hayo ili dunia ifahamu ukweli badala ya tetesi.

“( Wamenibana (mabalozi) kweli kweli ili Serikali itoe tamko rasmi… Nimewajibu kwamba ndani ya wiki hii Serikali itatoa tamko kwa kuwa nayo haijafurahia mauaji hayo,” alisema Membe. Aliongeza kuwa waliokufa katika tukio hilo ni Watanzania hivyo bila kujali itikadi ya chama, msiba huo ni wa kitaifa.

“Natoa pole kwa wafiwa wote ambao wamepoteza ndugu na rafiki kutokana na tukio lile, pia na wale waliolazwa hospitali, nawatakia kila la kheri wapone na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Membe.

Membe alisema kuwa jana alikutana na mabalozi hao kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu tukio hilo la mauaji yaliyofanywa na polisi kwenye maandamano hayo ya wafuasi wa Chadema, Januari 5, mwaka huu. Habari za ndani ya kikao hicho ambazo gazeti hili lilizipata zilieleza kwamba mabalozi hao walilituhumu Jeshi la Polisi wakisema kuwa halikutenda haki kwa sababu waandamanaji hawakuwa na silaha na walikuwa wakiandamana kwa amani.

Walipendekeza pia kuwa ni vyema jeshi hilo likapatiwa mafunzo ya kukabili maandamano ili kujua ni wakati gani wa kutumia silaha za moto, mabomu ya machozi au vifaa vingine vya kutuliza ghasia.

Chanzo hicho kilieleza kwamba kauli za mabalozi hao kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwa zimechangiwa na msimamo wa CCM na Chadema. Makatibu wa vyama vyote wamesikika wakikebehi kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha ya kusema tatizo hilo la Arusha ni la kisiasa hivyo linapaswa kutatuliwa kisiasa kwa vyama vyote viwili kukutana na kumaliza tofauti zao.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa alisema hawawezi kukaa na CCM kwa kuwa chama hicho na Serikali yake ni katili na ya kihuni. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akasema hawezi kukutana na Chadema kwa sababu suala la meya wa Arusha liko nje ya uwezo wa vyama hivyo viwili.

Makmba alisema kwamba uchaguzi wa meya ulisimamiwa na Serikali na kwamba wao CCM kama ilivyo Chadema, walichofanya ni kupeleka jina la mtu wanayeona anafaa. Makamba alifafanua zaidi kuwa kulingana na taratibu, meya huyo wa CCM alichaguliwa kihalali na kwamba kama kuna aliye na malalamiko anapaswa kufungua kesi mahakamani.

Wakati mabalozi wakitoa maoni yao tayari maaskofu wa makanisa ya Kikristo mkoani Arusha wameshatangaza kutomtambua meya huyo wa CCM na kwamba hawatampa ushirikiano.
Kutokana na mazingira hayo ya kuwepo kwa watu waliopoteza maisha na hata shutuma hizo za viongozi wa dini, aliyechaguliwa Naibu Meya, Michael Kivuyo wa TLP, alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati sakata hilo kwa kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na Nahodha. Vilevile, Pinda anatarajiwa kukutana na viongozi wa Chadema.
 
Habari kutoka katika vyanzo vya kuaminika zinasema Membe anataka kugombea Uraisi 2011. Kauli zake zina political motive!
 
Kauli ya Membe kuhusu mauaji yaliyofanywa na polisi Arusha.., nini kinaendelea ndani ya serikali., ni sahihi kwa Mwema na Nahodha kuendelea kung'ang'ania madaraka..?

Habari kamili..,

Na Hussein Issa (Mwananchi 12/01/2011)
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amesema Jeshi la Polisi lilikiuka maadili ya kazi yao, lilipokuwa likikabiliana na raia waliokuwa wakiandamana kupinga suala la uteuzi wa meya wa Arusha.Waziri Membe aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na vurugu zilizozuka baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanaandamana jijini Arusha wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa kwa risasi za moto.

“Jeshi la Polisi linatakiwa kufanya kazi kwa mipaka ili kuhakikisha kuwa linadumisha amani nchini,” alisema Membe akielezea kuwa ni maoni yake binafsi kuhusiana na tukio hilo linaloelekea kuliwekea doa Tanzania ambayo inajulikana kuwa ni kisiwa cha amani.

Vurugu hizo zilitokana na Chadema kuamua kuandamana kwa amani licha ya kuwepo na amri ya polisi iliyokuwa inawazuia wakishinikiza uchaguzi wa Meya wa jiji la Arusha urudiwe kwa sababu kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu zilizomsimika Gaudence Lyimo wa CCM kwenye madaraka hayo. Membe alisema kuwa mabalozi wa nchi mbalimbali hapa nchini walimbana wakitaka Serikali iweke wazi suala la mauaji hayo ili dunia ifahamu ukweli badala ya tetesi.

“( Wamenibana (mabalozi) kweli kweli ili Serikali itoe tamko rasmi… Nimewajibu kwamba ndani ya wiki hii Serikali itatoa tamko kwa kuwa nayo haijafurahia mauaji hayo,” alisema Membe. Aliongeza kuwa waliokufa katika tukio hilo ni Watanzania hivyo bila kujali itikadi ya chama, msiba huo ni wa kitaifa.

“Natoa pole kwa wafiwa wote ambao wamepoteza ndugu na rafiki kutokana na tukio lile, pia na wale waliolazwa hospitali, nawatakia kila la kheri wapone na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Membe.

Membe alisema kuwa jana alikutana na mabalozi hao kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine walijadili kuhusu tukio hilo la mauaji yaliyofanywa na polisi kwenye maandamano hayo ya wafuasi wa Chadema, Januari 5, mwaka huu. Habari za ndani ya kikao hicho ambazo gazeti hili lilizipata zilieleza kwamba mabalozi hao walilituhumu Jeshi la Polisi wakisema kuwa halikutenda haki kwa sababu waandamanaji hawakuwa na silaha na walikuwa wakiandamana kwa amani.

Walipendekeza pia kuwa ni vyema jeshi hilo likapatiwa mafunzo ya kukabili maandamano ili kujua ni wakati gani wa kutumia silaha za moto, mabomu ya machozi au vifaa vingine vya kutuliza ghasia.

Chanzo hicho kilieleza kwamba kauli za mabalozi hao kwa kiasi kikubwa zinaweza kuwa zimechangiwa na msimamo wa CCM na Chadema. Makatibu wa vyama vyote wamesikika wakikebehi kauli iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsa Vuai Nahodha ya kusema tatizo hilo la Arusha ni la kisiasa hivyo linapaswa kutatuliwa kisiasa kwa vyama vyote viwili kukutana na kumaliza tofauti zao.

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa alisema hawawezi kukaa na CCM kwa kuwa chama hicho na Serikali yake ni katili na ya kihuni. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akasema hawezi kukutana na Chadema kwa sababu suala la meya wa Arusha liko nje ya uwezo wa vyama hivyo viwili.

Makmba alisema kwamba uchaguzi wa meya ulisimamiwa na Serikali na kwamba wao CCM kama ilivyo Chadema, walichofanya ni kupeleka jina la mtu wanayeona anafaa. Makamba alifafanua zaidi kuwa kulingana na taratibu, meya huyo wa CCM alichaguliwa kihalali na kwamba kama kuna aliye na malalamiko anapaswa kufungua kesi mahakamani.

Wakati mabalozi wakitoa maoni yao tayari maaskofu wa makanisa ya Kikristo mkoani Arusha wameshatangaza kutomtambua meya huyo wa CCM na kwamba hawatampa ushirikiano.
Kutokana na mazingira hayo ya kuwepo kwa watu waliopoteza maisha na hata shutuma hizo za viongozi wa dini, aliyechaguliwa Naibu Meya, Michael Kivuyo wa TLP, alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati sakata hilo kwa kukutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema na Nahodha. Vilevile, Pinda anatarajiwa kukutana na viongozi wa Chadema

inasikitisha bira mabalozi kukubana isingetolewakauli?
 
Hii serikali imekaa kimtindo mtindo kweli. Kila mtu anasema jambo lake as if hayuko serikalini. Kwa bahati mbaya polisi wetu naona hawajajifunza kuyapima kwa weredi maneno na amri za kisiasa. Sasa hivi kama mambo yataenda vibaya basi huu mzigo wote ataubeba RPC wa Arusha. Ndio maana namuheshimu sana yule RPC waliyemtoa Arusha baada ya uchaguzi. He has his head intact. Kichwa chake hakijachakachuliwa.
 
....membe hana lolote aafikiri anaweza kuwa rais wa nchi hii ...kaama alifanya kikao na mabalozi alikuwa na haja gani za kutupatia taarifa za ndani za yaliyojadiliwa ......si angeenda kuripoti kwa bosi wake ...anatafuta sifa tu ...

PM, kwa hali ya mambo ilivyo sasa, who can stop him? Mbona mambo yamekaa bila mipangilio?
 
Hii serikali imekaa kimtindo mtindo kweli. Kila mtu anasema jambo lake as if hayuko serikalini. Kwa bahati mbaya polisi wetu naona hawajajifunza kuyapima kwa weredi maneno na amri za kisiasa. Sasa hivi kama mambo yataenda vibaya basi huu mzigo wote ataubeba RPC wa Arusha. Ndio maana namuheshimu sana yule RPC waliyemtoa Arusha baada ya uchaguzi. He has his head intact. Kichwa chake hakijachakachuliwa.

Mkuu Membe amekiuka maadili ya utawala. Haiingii akilini kusema kuwa ni kosa la polisi, Membe akiwa waziri ni sehemu ya government establishment, hatakiwi kuji-exclude kutoka kwa polisi. Alitakiwa kusema "tumefanya makosa", sio wamefanya makosa. Otherwise atwambie kuwa pilisi wetu ni incompetent au atuambie kama wanapokea order kutoka nje ya serikali.

Anatia aibu na ni kauli isiyo na busara kutoka kwa waziri mwandamizi na inaonesha kuwa serikali si kitu kimoja. Polisi watajiona kuwa wanatolewa kafara kutokana na makosa ya wanasiasa. Polisi kama wakitumia profession yao wanaweza kuwa professional, lakini kama wanatekeleza politicized order wanakuwa political pia. Bado lawama zinatakiwa ziende kwa political leaders.

Huwezi kuwatupia mpira kwa kuwalaumu kwa kutekeleza order za wanasiasa. Polisi wetu si independent. Najua kuwa Bernard Membe can not fool diplomats too.
 
Ni aibu sana ni karibu wiki zima lapita kikwete anafanya tu tafrija ikulu na kwingineko wakati wajeruhi wamejaa arusha, na hata hatoi pole na wala neno lo lote, aibu sana.

Siku moja tu woman-congress wa marekani baada ya kujeruhiwa na wengine sita kuuawa na risasi Obama yuko njiani kwenda kushiriki maombolezo kwa waliouawa, kuwapa pole majeruhi, lakini Mkwere wetu anafanya tu tafrija maana yake anafurahia damu aliyoimwaga Arusha.

"Mwivi haji ila kwa kuchinja na kuharibu"
 
Sidhani kama hiyo kauli ameitoa huku akipenda ni kama vile amelazimishwa aseme tu
 
Viongozi wetu jinsi wanavyoonesha dharau na ushenzi kwa wananchi bila aibu:

-- Tamko linatolewa mbele ya mabalozi
-- Tamko linatolewa baada ya kulazimishwa
-- Tamko linatolewa baada ya wiki kupita
-- Muda wote huu mkuu wa nchi yuko kimyaaa!

Officially uchunguzi wa tukio umefanyika lini na ni nani aliongoza uchunguzi huo? Tamko la waziri wa mambo ya ndani na la mkuu wa jeshi la polisi linaendana na tamko la waziri wa mambo ya nje? Tamko la Rais litaoana na matamko mengine na ni nani atajiuzulu kwa tukio kubwa kama hili la ukiukaji maadali nchini mwetu??!
 
Tamko 'binafsi' la Membe linapingana na msimamo wa wawakilishi wa "System at work JF", Zomba na Dar-es-salaam!!
 
Polisi wa Tanzania hawajui kuwa kutumia akili ya ushawishi is part of their work. Hili suala inabidi lijadiliwe vizuri na lichukuliwe very serious na Serikali. Amani inakuja tu pale wale watunza amani kama wanawajua vizuri wale watunzwao kwa hiyo amani. Amani si lazima ije kwaa risasi au virungu; vile vile inaweza kuja baada ya polisi kujaribu kuongea na wadau wao wa amani ambao ni wananchi. Polisi lazima vile vile wajifunze somo la ushawishi na upendo.

Polisi ya Tanzania haifanyi kazi kwa ajili ya wadau wake (wananchi) bali kwa ajili ya kutunza CCM.
Good point, naamini polisi ni binadamu wangeongea kwa busara na wanaowalinda isingekuwa taabu
 
Ukatili wa polisi ni kitu kimechukuliwa kama kawaida na serikali ya Tanzania na wanancho kwa ujumla. Mauaji mengi yamefanywa na polisi na kwa kumbukumbu zangu ni taarifa ya uchunguzi moja tuu ndiyo iliyofanyiwa kazi na serikali ya Tanzania. Hii ilikuwa ni ile iliyomhusu Zombe.Tanzania ni cnhi ambayo mwenye nguvu anaweza kulipa polisi ukabambikiwa kesi na kuteswa ama kufa au kupoteza viuong bila mtu kufanywa lolote. Kwa wenzetu Kenya ukatili wa polisi ulikuwa ni mojawapo ya mambo yaliyosukuma wananchi kudai Katiba mpya na kuwa na jeshi jipya la polisi. Hivyo polisi, viongozi/wanasiasa na wananchi wa Tanzania wote tumekuwa tunalitumia jeshi la polisi vibaya. Nakumbuka mwaka 2006 nilipoteza jamaa aliyeuawa na polisi kwa madai walikuwa kundi la majambazi. Hadithi ni nyingi lakini kunahisisa kuwa hata kama walikuwa majambazi waliuawa kwasababu hawakutoa mgao kwa polisi. Siukubali ujambazi hata kidogo lakini ni nane aliyempa polisi mamlaka kuua? Kwanini hawa mabwana wasipelekwe mahakamani?

Hili swala la police brutality/ukatili wa polisi linatakiwa lifanyiwe kazi ya kina na independent commission of inuiry ikiwezekana jopo litakalo jumlisha wastu wa ndani na nje. Policy reforms inatakiwa ipewe kipaumbale ndani ya katiba mpya. Katika Katiba mpya viongozi wa polisi wawajibishwe kama watu binafsai kunapokuwa na mauaji. Kenya, Bwana Ali aliyekuwa mkuu wa polisi wakati wa vurugu baada ya uchaguzi 2007, amejumlishwa katika orodha ya Ocampo kutokana na makosa ya ama kutekeleza amri ya juu bila kuzingatia haki za binaadamu/maadili ya kazi, ama katika kujipendekeza kwa wateule alitoa amri zilizopita kipimo. Ingawa sina ushahidi, katika nchi ambayo wakubwa wanamamlka makubwa kupita kipimo, wateule wanajitahidi kujipendekeza kupita kipimo. Tanzania maisha ya mteule yanastawi pale anpokuwa na mbinu kubwa za kujipendekeza hata ikibidi apote utu wake. Sintashangaa mkuu wa polisi wa Arusha aliamuru hayo yafanyike ili kumthibitishia mteule wake kwamba yeye yuko kwa ajili yake. Katika Katiba mpya tunayoizungumzia kama Taifa, ni muhimu kwa Tanzania kuwa na jeshi la polisi linaloheshimu haki za binaadamu na ustawi/maendeleo ya watu. Haki ya kuishi haitolewi na polisi, wanasiasa wala viongozi wa nchi, bali mtu anaipata kwa kuzaliwa. Yeyote anayetoa uhai wa mtu mwingine amevunja haki ya kuishi ya mtu na hawezi kutetewa kwasababu yeyote ile.

Katiba mpya ijenge utaratibu mpya wa viongozi kuwajibika kwa maendeleo, ustawi wa watu/wananchi na siyo mabalozi;wateule ama chama. Viongozi wetu wajifunze kuheshimu na kuthamini uhai na kujutia kupoteza hata roho/uhai mmoja. Kwa kifupi viongozi na watendaji wa serikali yetu hawathamini uhai wa waTanzania mpaka pale inapowahusu wao moja kwa moja. Watu 5 waliouwawa na polisi Arusha ni pigo kubwa sana kwa nchi yetu, si chama, sipolisi wala rais anaweza kuumba uhai ama kuurudisha ukitolewa. Tumekuwa tunaangalia umuhimu wa watu kutokana na wanafanya/ama watafanya nini. Hii ni dhana mbovu, uhai wa mtu ni haki yake ya kuzaliwa na hauwezi kuchukuliwa na mtu/taasisi yeyote. Viongozi ikijumlisha polisi wanawajibu kulinda na kustawisha uhai na siyo kuuotoa. Hakuna samahani yeyote inaweza rudisha roho/uhai hata mmoja kati ya ule uliopotezwa Arusha.

Kawaida mpya tunayoitaka Tanzania, ni ile ambayo waziri wa mambo ya ndani, mkuu wa wa jeshi la polisi, mkuu wa mkoa wa polisi na polisi waliohusika na mauaji hayo kupelekwa mbele ya vyombo vya sheria na kuwajibishwa kwa kupoteza uhai huo. Kawaida mpya tunayoitka ni ile ambayo wahusika wote haya wataachia ngazi zao pale watakaposhtakiwa ili kuiachia sheria ichukue mkondo wake. Bahati mbaya haya hawezi kutokea ndani ya Katiba ya sasa kwasababu aliyewateuwa haya anaweza asione sababu.

Mungu ibariki Tanzania na uisadie ipate Katiba Mpya ambayo ni endelevu na itaheshimu na kulinda uhai wa Mtanzania na haki za binaadamu kwa ujumla.
 
Alisema katika uchaguzi uliofanyika IVORY COST, Rais anayeng,ang,ania madaraka hakushinda, hiyo hawamtambui, bali wanamtambua huyu mwingine aliyenyang,anywa ushindi.

Boss wake JK mwenyewe kachakachua matokeo, na hakuna mtu yoyote serikalini aliye toa tamko kuwa matokeo ya urais hayakuwa sahihi.
lakini yanapotokea nchi nyingine, basi wanajitokeza na kudai mabadiliko.
 
Tambwe Hiza anaongea uchafu huu,na Membe anaongea uchafu mwingine,Michanganyoooo tuuuuu hatuelewi ni nani anae maanisha kilicho sahihi.Embu Dr.Slaa Rais wangu wakeli kanyaga twende hawa naona wanaleta gozigozi...Huyu Mende...ooossooory Membe amaebanwa a wakuu wa huko anakotakiwa kwenda kutembelea kuomba nga wa watoto(Thithiemu ombaomba)sasa asipoongea vizuri atakosa wa kumkaribisha na thithiemu watakosa misaada maana wanategemea misaada kwa 99.999%.she...e..nzi.!!
 
Ndiyo utekelezaji wa sera za CCM (Chama Cha Mafisadi), mmoja akikosea mwingine anajifanya anapoza issue, bado hatujamuuliza mgoshi Makamba ana weza kusema hata Membe hana akili kama Lowassa aliyependekeza maridhiano. Hawa viongozi wetu nafikiri jioni ikifika huwa kunakukusanya kwa Mkwere kwamba nani kafanya nini leo, ndiyo maana wakikosa cha kusema kwenye wizara zao wanadandia za wengine. Yawezekana Membe (Mende) ameongelea mauaji ya A town kwa vile ni mpakani na nchi nyingine ha ha ha ha haaaaaaa!!!!!!
 
Back
Top Bottom