Serikali yasaini mkataba wa dola bilioni 7

babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,221
3,167
Nimesoma kule kwa Ankal waziri wa nishati na madini William Ngeleja ametia saini mkataba na Kampuni ya Ophir wa utafutaji gasi na mafuta ambao utaligharimu dola bilioni 7.

Ophir Energy ambayo shareholder mkubwa ni Mittal, ilisajiliwa U.K 2004. Mwaka jana katika vitabu vyao vya mahesabu vilikuwa na cash 135milioni hakuna deni.

Dola bilioni 7 ni sawa na bajeti yetu 2010/2011.

Kuna mtu yeyote ambaye anaweza kuupata huo mkataba akatuwekea hapa? Tujue kama tumeuziwa mbuzi kwenye gunia kama mikataba mingine ya madini au ndiyo mambo yataanza kuwa tambarare.
 
na Chalila Kibuda na Marietha Mkoka

SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini jana imesaini mkataba na Kampuni ya Ophir na BG Group ya uchimbaji wa gesi mkoani Mtwara, utakaogharimu dola za Marekani bilioni saba, ambao utasaidia kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.

Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake mjini Dar es Salaam, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema uchimbaji wa gesi hiyo utasaidia kukuza uchumi kutokana na gesi nyingine kuuzwa nje ya nchi.

Alisema mradi huo ni mkubwa na wa kihistoria kwa taifa kutekelezwa, ambao utasaidia sehemu kubwa ya viwanda kutumia gesi ambayo itawapunguzia gharama kutoka katika matumizi ya umeme.

Alisema mradi huo utatekelezwa kwa miaka 25 na kampuni hiyo iliyoingia mkataba wa uchimbaji wa gesi hiyo na baadaye kubaki mikononi mwa serikali.

“Mradi huu ni wa kihistoria katika nchi kutekelezwa kwa kutumia fedha nyingi katika kuwekeza nchini Tanzania, kutokana na amani tuliyokuwanayo katika kujali wawekezaji,” alisema Ngeleja.

Alisema mradi huo utajali manufaa kwa wazalendo, kuanzia ajira, ambapo utatoa manung’uniko na kuonekana uwekezaji umeleta ukombozi ambao kila mwananchi atanufaika nao.

Source: Tanzania Daima.

*************************************************************************

mkataba wa utafutaji mafuta watiwa saini leo
Waziri wa Nishati na Madini mH. William Ngeleja (kulia) na Mwekezaji wa kampuni ya Ophir , ambae ni Technical Director bW. Jonathan Taylor wakiwekeana mkataba kwa ajili ya utafutaji wa gesi na mafuta baharini katika eneo la Kusini mwa Tanzania na litagharimu karibu shilingi zaidi ya trilioni 10 za madafu ama dola bilioni 7 za Kimarekani.

Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

source: Michuzi

Mtazamo:

Mkataba ulikuwa wa gesi au mafuta. Nimesikia mkataba ni 50/50 mgawanya kama ni hivyo JK nampa tano kwa hili maana atakuwa amecheza sana ataisaida nchi yetu kimaendeleo but mwenye mkataba atuonyeshe. Na kama niliwahi kusikia kuwa mafuta hamna tanzania au mambo yanaenda chini kwa chini?
 
hii ni good news kwakweli. pamoja na ile ya warusii usafishaji mafuta mkuranga sijui, nchi yetu niamwagiwa mvua ya baraka. LAKINI NAWEKA ANGALIZO, ISIJE KUWA WANAFANYA GELESHA ILI KUTOA ATTENTION KWA WANANCHI WAONE KAMA JK KAFANYA MAMBO MAKUBWA ILI WAMPE KURA KWENYE UCHAGUZI UFUATAO...WAKISHAONA AMEKAA KWENYE KITU TU, MAFAILI YOTE KWENYE JALALA.

pamoja na kwamba, nahisi kuwaamini kidogo kwasababu JK amekuwa anajiamini sana kuwa atapita, labda kweli katega mitego yake mingi anayojua hata wapinzani tutamuappreciate!

Nimefurahi kuwa hii kampuni mmoja wapo wa shareholders ni Mital, yule muhindi tajiri wa steel industries, Nafikiri kikwete angeongea na huyu jamaa aende kuchimba chuma kule liganga aweke steel industri hapa ili na sisi tuna export chuma cha pua...huyu jamaa nafikiri ndo anaongoza duniani kwa viwanda vya chuma cha pua kama sikosei....BADALA YAKE, WAMEMPA HII TENDA YA LIGANGA MHINDI WA KIBONGO SHUBAT PATEL....hivi huyu atafanya lolote litakalofaidisha taifa kweli?
 
ntwara oyeee

Ha ha haa...wamakonde hupenda ku replace m kwa n kama ntonto,nke,ntwara,nkwara,n'domo,nkono,n'guu.....lakini kuna maneno mwaili...yanawashinda amabvyo ni viungo vya binadamu,...siwezi kuiweka hapa kimaadili
 
Terms zitakuwa mbovu tu. Je, gesi na mafuta hayo ni kwa ajili ya ku-export au kwa matumizi ya mtanzania?
 
Nimeona hii na maoni yangu hapa ni kuwa kuna utata kwenye hii figure siamini kama hii kampuni ina ubavu wa kupata dola bilioni saba, na vilevile sijawahi kusikia kampuni yeyote ikitumia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya exploration (utafutaji) tofauti na development(kuendeleza). Ukweli ni kuwa kazi ya exploration ni kama kamari unaweza kupata au kukosa.

Sasa mi siamini hii figure kwa pointi zifuatazo;
  • Hii kampuni Ophir haina ubavu wa ku raise 7 billion for exploration.
  • Hakuna kampuni yeyote ya mafuta (including majors yaani BP, Exxonmobil etc) ambayo inatumia kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya utafutaji wa mafuta, kama ni development sawa hiyo ni issue nyingine.
  • Kwa vile East Africa ni new frontier, yaani ni eneo jipya la exploration kawaida ni kampuni ndogondogo ndio hufanya exploration kwa kati ya USD 10mil to Usd 60mil na sio hiyo figure.
Ophir wenyewe kama alivosema mdau mmoja hapo juu wana cash USD135m sasa vipi watumie dola bilioni 7 (zaidi ya mara 50!) kwa kamari, haiingii akilini.

Watanzania hesabu zinasumbua sana.

Ila ni muhimu kwa hizi kampuni kuendelea kufanya exploration kwa sababu sisi hatuna hizo hela na pili si vema tutumie hela za walipa kodi kuchezea kamari.
 
WaMzizima umekata issue vizuri mkuu. Hapa kwetu hii sekta ya mafuta watu hawaijui hata kidogo. Hata media yenyewe hawezi kuripoti kitu chenye mshiko. Absolutely, kwenye new frontier area, exploration stage expenditure inaenda step kwa step kidogo kidogo...sio kutumbikiza mihela halafu ukaambulia dry holes.....kwa hiyo 7 billion US$ sio realistic japo ni deepsea....lakini mmm!
 
Terms zitakuwa mbovu tu. Je, gesi na mafuta hayo ni kwa ajili ya ku-export au kwa matumizi ya mtanzania?

Wadanganyika mnasheherekea hata mkataba hamjauona!! Huko nyuma serikali ilisema hivyo hivyo walipotiliana saini na kampuni ya SONGAS, lakini toka kampuni hii ianze kuchimba gas huko kusini bei ya umeme haijapungua kama tulivyoahidiwa wala ile ya cement; ingawa kiwanda cha twiga cement kinatumia gas katika uzalishshaji. Katika mikataba hii mara nyingi tunaliwa kwasababu hao wanaotia saini hawasomo zile fine prints ambazo huwa zinakuwa na vipengele muhimu na hatari katika mikataba; kama mnavyojua viongozi wetu ni wavivu kusoma na ndio maana huwa wanapokea hata cheki zenye tarakimu tofauti na maandishi!! Hawataki kutuonyesha mikataba kwasababu wataumbuka na ufisadi wao kama si hivyo kwanini wafiche?.
 
Mungu asaidie tusidanganyike tena.
 
mmmh.. hivi ule mkataba wa IPTL haufanani na huu... ? Mbona tayari kuna makampuni mengine mengi tu ambayo yanatafuta gas na mafuta nchini? Kama serikali inaubia inaubia kupitia chombo gani, taasisi gani au kampuni gani? Maana nakumbuka hata kwenye Meremeta serikali ilikuwa na ubia kupitia Tangold ambayo warithi wake walikuwa ni familia za kina Chenge!
 
Shamba la bibi kila mtu atakuja ngoja tutaona watoto,wajukuu,na vitukuu watakavovishwa mizigo ya mikataba mibovu
 
Tanzania ni kati ya nchi zinazotenganisha majukumu kati ya mihimili mitatu ya dola:

Bunge - kutunga sheria na kusimamia serikali; Serikali (Rais/Kabineti) - kuleta mbele miswada na kutekeleza maamuzi ya sheria; na Mahakama – kuamua ni nini cha kufanya endapo kumekuwepo na opotovu wa sheria na maadili yake.

Hivi huyu Bwana Fez (kofia nyekundu) - m-Mbunge Mkono hachanganyi majukumu hayo?

SERIKALI: U-wakili wa serikali uko chini ya Wizara ya Sheria. Ni sehemu ya serikali. Hapo pichani, sijui Bwana Fez (m-Mbunge Mkono) nasimama upande upi? Mshauri/Wakili wa upande wa serikali au upande wa mwekezaji huyo wa nje?

MAHAKAMA: M-Bunge Mkono ni Mwanasheria/Wakili. Sawa. Lakini shughuli hizi za u-Wakili (mshitaki na mshitakiwa) huwa ni chini ya Mahakama.

Kama sikukosea, aliitetea Serikali (kesi ya maji).

Wakati Balali anakabiliwa na mashitaka huko BoT, m-Bunge Mkono alimtetea.

M-Bunge Mkono alikimbia kuonana na Balali wakati akitibiwa hospitalini huko Amerika. Mkono alikataa kutaja jina la hospitali kwa kisingizio kuwa yeye alipelekwa tu hapo hospitalini na jamaa ya karibu na Balali! Ajabu! Labda, hao jamaa wa karibu na Balali walimfunga macho asione au kuweza kusoma jina la hiyo hospitali!

Si hayo tu. Wakati wa kesi ya tuhuma ya kuua kwa kumpiga risasi dereva wa daladala iliyokuwa ikimkabili Ditto, m-Bunge Mkono alikimbia kutaka kumtetea huyo Ditto.

BUNGE: Wakati mwinginem-Bunge Mkono anafanya kazi yake ya u-Bunge. Kuna wkati alikwenda out of his limb na kutoka kikaoni kupinga nchi kuendelea kunyonywa na makampuni ya kigeni ya madini! Sawa.

Lakini hatukumwona Bwana Fez akitoka nje ya vikao ya Bunge vilivyohalalisha Benki ya Taifa ya Biashara kuuzwa kwa pesa za njugu.

Kwa nini? Alikuwa ndiye mpishi wa Benki hiyo kuuzwa (Balali na Anna Muganda na wengineo). Hapo baadaye alitamka (katika mazungumzo yake na Nyerere) kuwa alipata kazi, kama bingwa mshauri na kupewa kitita cha pesa.

Na wala hatumsikii akiwa mstari wa mbele wa kupambana na ufisadi! Kwa nini Benki yake (M Benki) ilianzishwa kwa ushirikiano na fisadi-tumiwa Jaeetu Patel, ambaye pia alimsaidia kujenga mashule huko kwao Uzanaki.
 
Kusaini mkataba si mbaya ila kubwa ni kama amepitia terms and conditions vizuri na kuona kama zitatufaidisha cc isijekuwa kapewa mkataba na kuusaini pasipo kuuchunguza kisheria, pili ni kuwa hata kama ni mzuri je utamfaidisha baada ya kumaterialize mtanzania wa kipato cha chini?
 
Nimeona hii na maoni yangu hapa ni kuwa kuna utata kwenye hii figure siamini kama hii kampuni ina ubavu wa kupata dola bilioni saba, na vilevile sijawahi kusikia kampuni yeyote ikitumia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya exploration (utafutaji) tofauti na development(kuendeleza). Ukweli ni kuwa kazi ya exploration ni kama kamari unaweza kupata au kukosa.

Sasa mi siamini hii figure kwa pointi zifuatazo;
  • Hii kampuni Ophir haina ubavu wa ku raise 7 billion for exploration.
  • Hakuna kampuni yeyote ya mafuta (including majors yaani BP, Exxonmobil etc) ambayo inatumia kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya utafutaji wa mafuta, kama ni development sawa hiyo ni issue nyingine.
  • Kwa vile East Africa ni new frontier, yaani ni eneo jipya la exploration kawaida ni kampuni ndogondogo ndio hufanya exploration kwa kati ya USD 10mil to Usd 60mil na sio hiyo figure.
Ophir wenyewe kama alivosema mdau mmoja hapo juu wana cash USD135m sasa vipi watumie dola bilioni 7 (zaidi ya mara 50!) kwa kamari, haiingii akilini.

Watanzania hesabu zinasumbua sana.

Ila ni muhimu kwa hizi kampuni kuendelea kufanya exploration kwa sababu sisi hatuna hizo hela na pili si vema tutumie hela za walipa kodi kuchezea kamari.

Sikuiona hii ndio maana niliziweka vile habari mbili tuzichambue maana kunaweza kuwapo usanii mwingi
 
mmmh.. hivi ule mkataba wa IPTL haufanani na huu... ? Mbona tayari kuna makampuni mengine mengi tu ambayo yanatafuta gas na mafuta nchini? Kama serikali inaubia inaubia kupitia chombo gani, taasisi gani au kampuni gani? Maana nakumbuka hata kwenye Meremeta serikali ilikuwa na ubia kupitia Tangold ambayo warithi wake walikuwa ni familia za kina Chenge!

Mzee wa kijijini mambo ya madini usifananishe na sekta ya mafuta na gesi. Sekta ya mafuta na gesi inasimamiwa na TPDC kwa niaba ya serikali. Kweli nakuhakikishia maslahi ya taifa yanazingatiwa sana. Production Sharing Agreement (PSA) ambazo TPDC huingia na makampuni ni nzuri na zinazingatia maslahi ya nchi ipasavyo. Tushukuru Mungu hii sekta Mkapa hakuitolea macho, tungekwisha. Angalia PSA model kwenye website ya TPDC, utagundua hawajamaa ni makini. In fact PSA tuingiazo ni standard worldwide. Bahati nzuri hizi sekta mbili, madini na mafuta & gesi nimekuwamo kwa miaka ya kutosha. Madini Mkapa alituliza, na sitamsamehe huyu mzee hata siku mmoja. Nashukuru hata kwenye kesi ya Mramba na YOna, anatajwa sasa; aliwazamisha hawa wazee.
 
mkuu hiyo dola bil.7 imewekwa ili tuliwe miaka hiyo 25 kwa sababu zile zile. oh hakuna kutoa kodi bado hatujarudisha pesa za uwekezaji. hiyo miaka 25 ikiisha mafuta nayo hakuna. hata uko iran na saudia visima vinaisha mafuta wanafungua vingine.
 
Back
Top Bottom