Serikali yapiga marufuku kusambaza mafuta ya mashoga

Serikali imepiga marufuku miradi inayohusisha utoaji wa vilainishi kwa mashoga kama njia ya kukinga kundi hilo na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya kuzindua wodi ya wazazi, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema suala hilo halikubaliki na ni kukiuka miiko na maadili ya Watanzania.

Amesema mashirika yasiyo ya Kiserikali yanaweza kutumia njia nyingine mbadala za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na siyo kutoa vilainishi ambavyo kwa upande wa pili vinaweza kuwa vinachochea tatizo hilo.

Awali, akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, waziri huyo amesema kuwa Serikali iko mbioni kuandaa muswada wa sheria utakaowasilishwa bungeni ili kutunga sheria itakayomlazimisha kila mwananchi kuwa na bima ya afya.

Chanzo: Mwananchi

sasa siyo kupga vita matumizi ya mafua hayo, mi nahisi wapige vta itendo vya ushoga basi, kama HAYO MAFUTA YANAKINGA UKIMWI basi wayagawe kwa kila mmoja maana hili ni janga la TAIFA ,,,,
AU MIMI SIJAELEWA ?
AU ALIYELETA MADA KAIWEKA VIBAYA?
 
Serikali imepiga marufuku miradi inayohusisha utoaji wa vilainishi kwa mashoga kama njia ya kukinga kundi hilo na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya kuzindua wodi ya wazazi, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema suala hilo halikubaliki na ni kukiuka miiko na maadili ya Watanzania.

Amesema mashirika yasiyo ya Kiserikali yanaweza kutumia njia nyingine mbadala za kudhibiti maambukizi ya Ukimwi na siyo kutoa vilainishi ambavyo kwa upande wa pili vinaweza kuwa vinachochea tatizo hilo.

Awali, akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, waziri huyo amesema kuwa Serikali iko mbioni kuandaa muswada wa sheria utakaowasilishwa bungeni ili kutunga sheria itakayomlazimisha kila mwananchi kuwa na bima ya afya.

Chanzo: Mwananchi
Unafiki mkubwa kabisa huu si wawaambie hao wafadhili na kile kitengo pale Muhimbili kifungwe?
 
Sidhani kama anajua anachokiongea!! Walisaini mikataba wao, pesa wanapokea wao. Leo iweje mtu anaibuka na kusema hawataki vilainishi?? Hhahaahhaa tunaweka siasa kwenye maisha ya watu
 
yanageiwa wapi hayo mafuta nami nkachue maana ngono yoyote inasababsha michubuko si kwa mashoga tu!

BANGO
 
Sasa kama kuna vitu vizuri hiv vya kujikinga na ukimwi kwa nini wametuletea ma condom? Waachie wese hilo, wafungie condom zao kwanza hazina hata flavour. ..
 
Back
Top Bottom