Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Mimi natoka Kyela na niko tired na hizi tuhuma za kila siku ambazo nyingi hazina maana kabisa.
Kwenye hili la maafa kuna watu wengi sana ambao wanasaidia, wengi wao hata hawahitaji kujitangaza. Kwa mfano hadi leo kuna kikosi cha JWTZ kiko kule kimejichimbia kikijenga madaraja na barabara ambayo imebomolewa. Sijasikia Mwamunyange akitamba sehemu jinsi alivyosaidia. Tunataka watu kama hao, chapa kazi, sifa itakuja baadaye.
Umesomeka MKUU....
Lakini jambo la msingi ni kwamba, mara nyingi tunakwamishwa na fikra hasi. Hata kama unafanya kazi na adui yako, ukiwa chanya, atakwama na kubadilika kuwa upande wako, lakini ukiwa hasi kwa kila mtu, hata rafikiyo atabadilika na kuwa adui yako, ama atakusaliti