Serikali yaifungia kuandikisha wanafunzi shule ya Al Muntazir kwa kupandisha ada na kutoza faini

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Serikali imeifungia kuandikisha wanafunzi kwa vidato vya kwanza na tano shule ya Al Muntazir iliyopo jijini Dar es salaam kwa kupandisha ada kinyume cha taratibu na Wizara ya elimu.

Pia shule hiyo imetuhumiwa kuwatoza faini wazazi wanaochelewa kulipa ada.

Ikumbukwe kuwa mwanzoni mwa mwaka huu serikali serikali ilipiga marufuku shule binafsi kupandisha ada kiholela na ikiwa shule inataka kufanya hivo ilitakiwa kuomba kibali kwa kamishna wa elimu.

image.jpeg

image.jpeg
 
Kuwatoza Faini walimu Wanaochelewa Kulipa Ada ... ???? Au Mm ndo sijaelewa
 
Mbona kuna shule zingine pia zimeongeza na hatujasikia kitu.. Au ndiyo wameanza na hawa?
 
Kweli serikal hii ipo kazini Hakuna kumuonea mtu aibu liwe jipu kubwa au dogo.. Ni kweli hio shule imepandisha ada na ni kila mwaka... Hapa kazi
 
Sijaelewa!

Ukilnganisha ada zinazotozwa Feza Schools na Almuntazir hawafikii kabisa, bado Almuntazir wana ada za chini kabisa, labda makosa yao kupandisha bila kufuata utaratibu, lakini ada za hii shule ni za chini ukilinganisha kwa mashule ya type hii!

Pili Serikali lazma akubali kuwa elimu yetu ilishuka sana sana saa mpaka watu kumimbilia shule hizi ambazo zinatoa elimu kwa kiwango! pia ikumbukwe walimu wa shule hizi hulipwa pesa nyingi kuendana na kiwango cha elimu wanayotoa, Pia shule kama hizi hutumia materials kwa ajili ya kufundisha watoto!

Mtoto wa darasa la kwanza anafundishwa jinsi ya kufanya Project! anafundishwa mambo mengi wanamjenga akili yake tokea chekechea! mtoto wa chekechea Kg2 anakuwa ameshaweza kusoma kabla hajamaliza Kg3 na anakuwa ana knowledge kubwa akifika darasa la kwanza anakuwa yupo mbali!

Mimi ni mzazi wa watoto wanaosoma shule hii! Nimeshuhudia mtoto ambae anasoma Degree IFM anacopy notes za mtoto alieko Form 2 ya Almuntazir!

NAdhani wafuate utaratibu halafu Serikali ikae na hizi shule ili wajifunze kutoka kwa hizi shule labda huenda elimu yetu itabadilika!
 
Mbona shule nyingi tu zimepandisha ada, wapite kwenye shule zote wataona

Ninanachojua mimi serikali haijakataza wamiliki wa shule binafsi kuongeza ada bali inatakiwa upandishe ada ukiwa na sababu za msingi. Na pia imekataza upandishaji ada kiholela, kabla ya kupandisha ada inatakiwa kupata kibali maalumu toka kwa kamishna wa elimu.
 
Back
Top Bottom