Serikali ya Tanzania yasalimu amri kwa wafadhili

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Serikali ya Tanzania yasalimu amri kwa wafadhili

Source: Mwanahalisionline.

SERIKALI ya Tanzania inajiandaa kuwasilisha bungeni, muswada wa mabadiliko ya Sheria ya Takwimu, ili “kujiondoa” kwenye kibano cha kunyimwa fedha za miradi ya maendeleo na nchi wahisani.” Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).
Taarifa kutoka ndani ya serikali na mashirika ya fedha ya kimataifa – Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) – zinasema, serikali imelazimika kusalimu amri, kufuatia wafadhili hao, kuzuia mabilioni ya dola za Kimarekani kwa Tanzania.
Benki ya dunia imetenga takribani dola za Kimarekani 1.7 bilioni (karibu Sh. 4.1 trilioni), kwa ajili ya miradi mbalimbali nchini. Hata hivyo, sehemu kubwa ya fedha hizo, zimezuiwa kutokana na serikali kupitisha sheria mpya ya Takwimu.

Benki ya Dunia na IMF wanasema, sheria hiyo inakiuka haki za binadamu na kuminya uhuru wa wananchi wa kujieleza na ule wa kutoa maoni.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali imepanga kuwasilisha bungeni marekebisho ya vifungu kadhaa vinavyolalamikiwa na wahisani na wadau wengine, “ili kujinusuru na kibano hicho cha kunyimwa fedha.”

Muswaada wa mabadiliko ya sheria hiyo, unatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano huu wa Bunge la Bajeti unaoendelea mjini Dodoma.

Taarifa zinasema, muswada huo, utakuja bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza, mwezi Juni mwaka huu.
Bunge la Jamhuri, lilipitisha mabadiliko ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018, katika mkutano wa Bunge wa Septemba mwaka jana. Mabadiliko hayo yalikumbwa na upinzani mkali kutoka kwa makundi ya wanaharakati na wabunge wa upinzani.

Hata hivyo, muswada huo ulipitishwa kwa mbwembwe bungeni, baada ya serikali kuamua kutumia wingi na wabunge wa chama tawala – Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pamoja na mambo mengine, sheria mpya ya Takwimu inapiga marufuku uchakataji wa taarifa za tawimu na imeweka marufuku ya kusambaza taarifa zote za takwimu bila ruhusa ya serikali.

Aidha, sheria inaelekeza kuwa kila anayetoa taarifa za takwimu kuthibitishwa na serikali, na kwamba ni kosa la jinai kuchakata na kusambaza taarifa za takwimu bila ruhusa ya serikali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka jijini Dar es Salaam na makao makuu ya benki ya dunia nchini Marekani zinasema, benki imekasirishwa na hatua ya serikali kupitisha sheria hiyo na imeshinikiza kuondolewa mara moja, baadhi ya vifungu kandamizi vilivyomo kwenye sheria husika.

Mtoa taarifa wa MwanaHALISI Online ambaye ni mmoja wa maofisa wa ngazi ya juu wa IMF amesema, Benki ya Dunia imesisitiza, “haitarejesha hata dola moja ya fedha zake za maendeleo, kabla ya serikali kurekebisha sheria hiyo.”
Amesema, uamuzi wa benki hiyo, umetokana na “kujiridhisha kuwa sheria mpya ya Takwimu, “inaminya uhuru wa wananchi wa kupata taarifa na kinyume na Katiba ya Jamhuri na mikataba ya kimataifa.”

Vifungu ambavyo vipo kwenye Sheria ya Takwimu (2018) na ambavyo serikali imeahidi wahisani kuvifanyia marekebisho, ni pamoja na kifungu cha 24 (A) (2); 24 (B) (1) pamoja na 24 (B) (2).
Serikali imekubali kukiondoa pia kifungu kinachotoa adhabu kwa watu wanaopatikana na hatia ya kukiuka sheria hiyo.

Mtoa taarifa huyo anasema, kuwasilishwa kwa mabadiliko ya sheria ya Takwimu katika mkutano huu wa Bunge la Bajeti, ni sehemu ya makubaliano kati ya ujumbe wa serikali na maofisa wa ngazi ya juu wa benki ya dunia na IMF.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili, yaliyofanyika wiki mbili zilizopita, jijini Washington DC, nchini Marekani.
Anasema, katika mkutano huo, taarifa zinasema, ujumbe wa Tanzania uliweza kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa WB anayeshughulikia masuala ya Afrika, Hafez Ghanem na Mkurugenzi Mtendaji wa benki anayesimamia nchi za Afrika, Anne Kabagambe.
Fedha ambazo zimeondolewa na WB kutokana na kuwapo kwa sheria hiyo, ni pamoja na dola za Marekani 450 milioni, zilikuwa zimetengwa kwa ajili ya kusaidia miradi ya TASAF 111 na dola za Kimarekani 300 milioni, zilizokuwa zitolewe kwa ajili ya mradi wa maji safi vijijini na maji taka.

Mamilioni mengine yaliyozuiwa, ni dola za Marekani 400 milioni, zilizokuwa zimeombwa kwa ajili ya kuongeza ubora wa elimu ya sekondari.
Anasema, pamoja na kuwapo kwa sheria ya Takwimu, wahisani wamekasirishwa pia na hatua ya serikali ya kuweka zuio kwa wasichana waliopata mimba wakiwa shule za Sekondari kuendelea na mfumo rasmi wa elimu.
“Kule Marekani wakuwa hawa waliwaambia wazi wazi, maofisa wa Tanzania kuwa upatikanaji wa fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo inayo gharamiwa kwa mikopo nafuu ya Benki ya Dunia, haitatolewa iwapo serikali haitarekebisha kasoro hizo,” ameeleza afisa huyo wa WB.
Anasema, “serikali imekubali kufanyia marekebisho kasoro hizo, ikiwa ni pamoja na kuahidi kuwawezesha wasichana waliopata mimba shule za Sekondari kuendelea na masomo.”

Tangu kufanyika kwa mabadiliko kwenye sheria ya takwimu, watu kadhaa, wakiwamo wabunge na taasisi za kitafiti za ndani, zimeshindwa kuchambua na kuchapisha taarifa tofauti na zile za serikali hasa katika suala tata la ukuaji wa uchumi wa taifa.

Wakati serikali ikidai kuwa uchumi wake umezidi kuimarika, baadhi ya wabunge hasa wa upinzani, wamekuwa wakiituhumu serikali ya Rais John Pombe Magufuli, kudanganya kwenye taarifa zake za ukuaji wa uchumi.
Baadhi ya wakosoaji wa serikali kuhusu taarifa zake za ukuaji wa uchumi (GDP Growth Rate), wanadai kuwa wameshindwa kutoa taarifa mbadala kwa kuogopa mkono wa sheria, unaotokana na kuwapo kwa sheria hiyo.

Mpaka sasa, angalau Zitto Kabwe, mbunge kutoka chama cha ACT- Wazalendo, kutokea jimbo la Kigoma Mjini, mkoani Kigoma, Magharibi mwa Tanzania, ndiye anayeonekana kutumia kinga ya Bunge, kukosoa serikali kuhusu taarifa zake za ukuaji wa uchumi (GDP Growth Rate).
Zitto amekuwa akisema bungeni, kuwa uchumi wa nchi umedorora; kuna tofauti kubwa ya kipato kati ya matajiri na maskini.
 
Wabunge wetu hawaoni aibu kila uchwao wanadharirika wao. Hii inaashilia akili zao kuna mahali zimeshikwa

Haiwezekani wote wapitishe kitu ambacho hakikubaliki ndani na nje ya mipaka.

Alafu hapo hapo sheria haijadumu ata miaka 3.

Huu tunaita udhaifu. Kesho wakipelekewa kingine watapiga ndiyooooooooo alafu baada ya mwezi kinatenguliwa
 
Wapeleke police kama kawaida yao!! Kiburi kingi jukwaani wakitoka hapo wanaenda kujadiliana watapata vipi hizo hela?
 
nadhani waongeze mbinyo Zaidi.

Inatakiwa wasitoe hata shilingi mpaka hizo sheria kandamizi zibadilishwe, kuanzia sheria ya takwimu, sheria ya mitandao na sheria ya vyama vya siasa. Na baada ya hapo wafuatilie uchaguzi kama utakuwa huru na haki. Iwapo sheria zote kandamizi zitaondolewa na uchaguzi kuwa huru na haki hapo ndio watoe hela zao. Iwapo haitakuwa hivyo waweke hata vikwazo vya kuuza madini yetu nje mpaka wanyooke na huu uhuni unaofanywa na chama dola.
 
Wabunge wetu hawaoni aibu kila uchwao wanadharirika wao. Hii inaashilia akili zao kuna mahali zimeshikwa

Haiwezekani wote wapitishe kitu ambacho hakikubaliki ndani na nje ya mipaka.

Alafu hapo hapo sheria haijadumu ata miaka 3.

Huu tunaita udhaifu. Kesho wakipelekewa kingine watapiga ndiyooooooooo alafu baada ya mwezi kinatenguliwa
Kwenye bunge letu tuna wabunge wachache wa kuhesabu wenye uelewa mzuri, wanahesabika kwa majina. Lakini walio wengi ni mbumbumbu, wanafiki, waoga na wasio na uelewa wowote wa kulisaidia Taifa.

Hongera sana Zito, TL, Msigwa maana ninyi ni vinara katika kundi la wabunge wenye uelewa na wanaojitambua.
 
Kwa mfumo uliopo wa serikali, wa kuweka makada kama viongozi wa serikali za mikoa na wilaya, watu kama hao hawatakiwi awamu hii hasa kipindi cha pili. Nahisi ndo kutakuwa na maamuzi ya ajabu haijawahi kutokea sababu watakuwa hawana cha kupoteza.
 
Inatakiwa wasitoe hata shilingi mpaka hizo sheria kandamizi zibadilishwe, kuanzia sheria ya takwimu, sheria ya mitandao na sheria ya vyama vya siasa. Na baada ya hapo wafuatilie uchaguzi kama utakuwa huru na haki. Iwapo sheria zote kandamizi zitaondolewa na uchaguzi kuwa huru na haki hapo ndio watoe hela zao. Iwapo haitakuwa hivyo waweke hata vikwazo vya kuuza madini yetu nje mpaka wanyooke na huu uhuni unaofanywa na chama dola.
Tena kama ingekuwa inawezekana, baada ya kufanyia marekebisho hizo sheria gandamizi, walistahili kuapa kuwa hawataendelea kutunga sheria nyingine za kidikteta.
 
Halafu cha ajabu wale nyumbu fc, utawaona tena wanasifia hayo marekebisho!! Ohooo rais msikivu, bila kibano cha mabeberu ingekuwaje, mabeberu ni kama maji huwezi yakwepa kamweee!!! Yaani ukiwa na akili za kushikiwa, unapata tabu sana, kwani hujui huyo aliyekushikia kesho ataamua vipi!!! Yaani prof. Mzima anakubali akili zake zishikiliwe na std 7!!halafu hapo uniambie prof. Wa kizungu ni sawa na prof wa kibongo/afrika? Nakataaaa kamweee, prof anaendekeza njaaa kuliko hata mkulima?!!!
 
Wabunge wetu hawaoni aibu kila uchwao wanadharirika wao. Hii inaashilia akili zao kuna mahali zimeshikwa

Haiwezekani wote wapitishe kitu ambacho hakikubaliki ndani na nje ya mipaka.

Alafu hapo hapo sheria haijadumu ata miaka 3.

Huu tunaita udhaifu. Kesho wakipelekewa kingine watapiga ndiyooooooooo alafu baada ya mwezi kinatenguliwa
Ifikemahali wajiulize wanatumikia chama au wananchi nawaona waowakobze nalichama wawewanapiga kampeni kwenyechama wanakotumikia watuache wananchi wanatupenda wakati wakuomba kura tu wakipata wanatumikia lichama hovyo kabisa
 
Halafu cha ajabu wale nyumbu fc, utawaona tena wanasifia hayo marekebisho!! Ohooo rais msikivu, bila kibano cha mabeberu ingekuwaje, mabeberu ni kama maji huwezi yakwepa kamweee!!! Yaani ukiwa na akili za kushikiwa, unapata tabu sana, kwani hujui huyo aliyekushikia kesho ataamua vipi!!! Yaani prof. Mzima anakubali akili zake zishikiliwe na std 7!!halafu hapo uniambie prof. Wa kizungu ni sawa na prof wa kibongo/afrika? Nakataaaa kamweee, prof anaendekeza njaaa kuliko hata mkulima?!!!

Haiwezekani mkuu, usijaribu kufananisha kifo na usingizi.

Ma pro wa kizungu wako bize na tafiti za kitaalamu, wa kwetu wako wanapiga domo na kusifia ili wapate uteuzi.
 
Back
Top Bottom