Serikali ya Tanzania kuingiza nchini ndege 2 za kisasa kutoka Canada ndani ya siku 60

Hii Nchi ya vichekesho sana....
wanawapija vita CUF eti wanawataka kuwarejesha Waarabu huku upande mmoja wanawakumbatia...
Kwani unafikiri hawaujui ukweli? Si wanawapumbaza wanavijiji tu huko! Miji yote wanakosa kura
 
Ndiyo hivo tunaiga nyayo za KENYA jirani (mbinu za kibiashara) !!

Raundi hii naona kama mnaamka vile, Tanzania mlizoea sana kufanya biashara mkitegemea mambo ya undugu. Sasa mnaingia kwenye ubepari full time, hamna cha undugu ila maslahi. Hili mjifunze sana kutoka kwa Wakenya, linapokuja suala la biashara, hakuna kucheka cheka.

Nikiwa huko Tanzania, Wabongo walikua wanatushangaa sana jinsi Wakenya tunavyonuniana kwenye vikao vya biashara, lakini baadaye na baada ya kazi tunakunywa beer pamoja na kucheka kama mandugu, ila tukiwa kwenye majadiliano na mabishano na ushindani wa kibiashara kwenye vikao, inakua ni vijembe kwenda mbele.
 
Mmh dada mbona unajipa matumaini hewa? Sidhani kama watu wanamuogopa Magufuli kihivyo kwani wangekuwa na woga huo, waziri mkuu alisema mabasi yaendayo kasi yaanze kazi february 10, nipe mrejesho. Ile pump ya mafuta iliyokuwa na utata pale bandarini, hadi leo bado utata upo!! Katika mazingira haya ukiwa na imani kubwa kupita kiasi unaweza kufedheheka kupita kiasi iwapo mambo yataenda kinyume.
Kama hayakuanza February 10, kuna sabab za kimsingi ambazo hata Rais atakuwa amekubaliana nazo, Na mlisha sema si kila jambo mnataka picha na habari kwahiyo serikali itawatangazia tena tarehe ya kuanza hayo mabus, Ukisikia hizo bus zimeuzwa na hazitafanya kazi tenda ndio ukate tamaa na uongozi wa Magufuli. amini ndege zitafanya vizuri chini ya uongozi wake.
 
Huyo waziri mkuu wakati anatangaza zianze tarehe 10 hizo sababu za msingi hakuzijua ama hakuambiwa? Naona umeruka lile suala la pump ya mafuta bandarini, anyway maana sio mtihani tunafanya hapa hata usipotoa utetezi sio mbaya. Ila najaribu kukupa picha tu kwamba huku africa na tanzania haswa kusema ni jambo moja na kutekeleza ni jambo jingine. Ni vyema katika nchi yetu kuna nyie mnaomini kila mnachoambiwa na viongozi, na kuna akina sisi tunaoamini kama Tomaso. Tuna uzoefu na hizi hadithi, nia ni njema ila utekelezaji ni shida.
 
Kuhusu pump ya mafuta nadhani hata wewe huna uhakika kama agizo limedharauliwa ni hisia tu, ila tumuamini ndo jambo la msingi.
 
Raundi hii naona kama mnaamka vile, Tanzania mlizoea sana kufanya biashara mkitegemea mambo ya undugu. Sasa mnaingia kwenye ubepari full time, hamna cha undugu ila maslahi. Hili mjifunze sana kutoka kwa Wakenya, linapokuja suala la biashara, hakuna kucheka cheka.

Nikiwa huko Tanzania, Wabongo walikua wanatushangaa sana jinsi Wakenya tunavyonuniana kwenye vikao vya biashara, lakini baadaye na baada ya kazi tunakunywa beer pamoja na kucheka kama mandugu, ila tukiwa kwenye majadiliano na mabishano na ushindani wa kibiashara kwenye vikao, inakua ni vijembe kwenda mbele.

We jamaa huwa unaongea point sema Point zako huwa zinagusa kwenye vidonda tu na sio kwingineko.anyway katika hili uko sahihi kwa kuwa tokea tokea tumepata uhuru ndege pekee kuimiliki ni Bombardier DHC8-Q300 Dash 8, 5H-MWF ,kwa hiyo hizi habari za kununua ndege mbili kwa mpigo ni lazma zitusisimue.
 
Kuhusu pump ya mafuta nadhani hata wewe huna uhakika kama agizo limedharauliwa ni hisia tu, ila tumuamini ndo jambo la msingi.

Labda nikuambie kitu, hilo suala la pump naona wewe ndio huna taarifa za kutosha maana hata ni aibu kuliandika hapa, tunaogopa kuwakwaza nyie mnaomini kila mnachoambiwa na matamko toka serekalini. Ukipenda fuatilia ujue ukweli, lakini kama hutaki kuvunjika moyo na kupoteza imani ndani ya hizi siku 400+ ni bora ukabaki na imani yako kuliko kuujua ukweli ukavunjika moyo. Nisingependa kupunguza uzalendo wako kwenye mambo haya.

Tuachane na hayo hapo juu, ila hebu nipe taarifa maana kidogo wewe ni wa kileo, nasikia hapo bandarini meli zimepungua hivyo kuna uwezekano wa pato kushuka, je ni kweli ama uzushi wa wapinzani na waliotumbuliwa majipu?
 
Ninavyojua Canada hawatengenezi ndenge tunarudi kulekule kukodi makuukuu,#majanga!
Basi kuanzia leo ujue Canada wanatengeneza ndege BOMBADIER.

Bombardier Inc.
Company
bombardier.com
Bombardier Inc. is a Canadian multinational aerospace and transportation company, founded by Joseph-Armand Bombardier as L'Auto-Neige Bombardier Limitée on January 29, 1942, at Valcourt in the Eastern Townships, Quebec.Wikipedia
Stock price: BBD.B (TSE)CA$1.31-0.03 (-2.24%)
Mar 29, 4:15 PM EDT - Disclaimer
Headquarters: Montreal, Canada
CEO: Alain M. Bellemare
Founder: Joseph-Armand Bombardier
Founded: 1942, Valcourt, Canada
Subsidiaries: Bombardier Aerospace, Bombardier Transportation, Shor
 
ATCL ifumuliwe na kuundwa upya kwanza!
Very well said mkuu! Mm nashangaa tunavyolipokea hili suala kwa hisia, kwani ni nani aliesema tatizo la ATCL ni kutokua na ndege? Na ndio maana inashauriwa serikali isijiingize ktk biashara.
 
We jamaa huwa unaongea point sema Point zako huwa zinagusa kwenye vidonda tu na sio kwingineko.anyway katika hili uko sahihi kwa kuwa tokea tokea tumepata uhuru ndege pekee kuimiliki ni Bombardier DHC8-Q300 Dash 8, 5H-MWF ,kwa hiyo hizi habari za kununua ndege mbili kwa mpigo ni lazma zitusisimue.
Hapana kuna ndege tulirithi kutoka East African Airways mwaka 1977 na nyingine tulinunua mtumba kutoka kwa mtu akiitwa George Syporos kama sijakosea jina mwaka 1981 na ndege ile ilipotua tu JKNIA haikuruka tena
 
huo ni mwanzo mzuri wa biashara hiyo. nadhan kwa umakini wa serikali hii zitakuwa ni ndege zenye tija kwa taifa.
 
Back
Top Bottom