Serikali ya mseto huenda ikajadiliwa na kikao maalum

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Mwinyi%20makame%20Z%288%29.jpg

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame.



Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar yatakayoruhusu kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa yatalazimika kujadiliwa na kikao maalum cha dharura kutokana na Baraza la Wawakilishi kumaliza muda wake kabla ya kufanyika kura ya maoni, Julai 31 mwaka huu.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha bajeti kwa mwaka fedha 2010/11 mjini Zanzibar.
Alisema iwapo wananchi wa Zanzibar wataamua iwepo Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar, kikao cha dharura kitalazimika kuitishwa kwa kwa sababu Baraza linatakiwa kuvunjwa Julai 16 wakati kura ya maoni itafanyika Julai 31 mwaka huu
“Kama wananchi walio wengi wataunga mkono kuwepo kwa mabadiliko ya muundo wa Serikali, itabidi kuitishwa kikao cha dharura cha marekebisho ya katiba,” alisema katibu huyo.
Alisema Baraza la Wawakilishi baada ya kuvunjwa wajumbe wote watalazimika kurudi katika majimbo yao kujitayarisha na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
Tayari Tume ya Uchaguzi Zanzibara imeanza kutoa mafunzo kwa wadau wa uchaguzi kuhusu kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ama la.
Hata hivyo, wazo la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar linaonekana kuwagawa viongozi wa Serikali na CCM Zanzibar kwa madai kwamba suala hilo linakwenda kinyume na sera ya CCM na misingi ya Mapinduzi ya mwaka 1964
Kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2010/1011 Katibu wa Baraza hilo alisema inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Juni 9 mwaka huu.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom