Serikali ya Magufuli imepoteza TZS 1.5 trilioni mwaka 2016/17. Imetumia Mabilioni kinyume na Utaratibu, Imelipa Madeni Hewa

Mkuu wangu Chesty,, naomba unisamehe bure tu mdogo wangu, ni kughafirika tu kote huko! Naihurumia sana nchi yangu kuongozwa na likimbizi harafu kuna majitu kule Lumumba yanapiga vigelegele! Ndiyo maana nikatukana Matanzania yote maana tunaonekana kama hatuna akili vile,, yaaniamekosekana mkakamavu hata mmoja wa kudai vielelezo vya mtu huyu!! Hata mimi nilimkataa tangu siku anatangazwa pamoja na kujivika Usukuma lakini niligoma kula Haramu!!
Nimekuelewa ndugu yangu, itakuwa hasira zilizidi kuona tunafanyiwa mambo ya dharau na sie tumenyamaza tu kama misukule.
 
WanaJF, nashangaa kuna nini nyuma ya kulishikia bango suala 1.5 Try? Nauliza hivyo kwa kuzingatia Ripoti ya CAG ni ya hesabu ya 2016/17 ambai ni mwaka wa kwanza wa Serikali iliyoko madarakani. Ripoti hiyo inadhihirisha kwamba Serikali imerithi watendaji ambao ripoti imethibitisha kuwa bado kuna watumishi Serikalini na Taasisi zake waliokwishajenga tabia ya uzembe, utendaji kazi wa mazoea, usimamizi mbovu, ubadhirifu, na ufisadi wa mali na rasirimali za Taifa. Hivyo Rais Magufuli amekuwa sahihi kuteua na kutumbua aina hiyo ya watumishi.

Hivyo nina matumaini makubwa kuwa Serikali itatumia matokeo ya ripoti hiyo kuchukua hatua zaidi dhidi ya watumishi waliohusika na wa aina hiyo. Matokeo yake yataonekana kwenye Ripoti ya CAG ya 2019/20, mwaka wa mwisho wa Serikali yake
 
mzee wa trillion 1.5 vipi mbona hajaenda kuzindua zahanati, au ndio aibu ya kashfa ya ufisadi
 
SHILINGI TRILION 1.5 ZA KITANZANIA KAMA UKIWA NAZO

1. Kama una kasi ya kuhesabu shilingi milioni moja kwa dakika moja. Maana yake Shilingi trilioni 1.5 utazihesabu kwa dakika 1,500,000, sawa na masaa 25,000, sawa na siku 1042, sawa na miaka 2 na miezi kumi.

2. Noti moja ya Tsh. 10000 ina urefu wa Sentimita 15 na upana wa Sentimita 7.5. Ukitafuta eneo la mstatili wake ni sawa na Sentimita za eneo (mraba) 112.5 au (112Cm²).
Idadi ya noti za elfu 10 kwenye Tsh. Trilioni 1.5 ni noti 150,000,000. Ukizidisha na ile 112.5 ni sawa na eneo la Sentimita za mraba 16,875,000,000 au Mita za mraba 1,687,500. (1,687,500m²)
Uwanja mmoja wa mpira wa miguu wenye urefu wa mita 100 na upana wa mita 75 una eneo la 7500m²
Chukua (1,687,500 ÷ 7500) = 225
Maana yake, Tsh. Trilioni 1.5 unaweza kuzipanga zikafunika eneo sawa na viwanja 225 vya mpira wa miguu.

3. Kwa urefu wa Sentimita 15, kwa idadi ya hizo noti 150,000,000 ni sawa na umbali wa sentimita 2,250,000,000 sawa na kilometa 22,500.
Jumla ya umbali wa mipaka yote ya Tanzania bara pamoja na ufukwe wa bahari kutoka Tanga hadi Mtwara ni Km 4826.
Kwa hiyo ukizipanga kwa urefu pesa hizi, zinaweza kufanya mizunguko minne katika mipaka yote ya Tanzania bara (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Zambia, Malawi, Msumbiji na ufukwe wa bahari ya hindi kutoka Tanga hadi Mtwara) na bado zitabaki za kutosha umbali wa Km 3196.
Hizo zinazobaki unaweza kuzipanga mistari miwili kutoka ncha ya mbali kabisa ya kaskazini hadi ncha ya mbali ya kusini mwa Tanzania bara (Km 1223 X 2 = Km2446) Na bado zitabaki za Km 750. Ambazo zitapangika kutoka DSM had Tanga mara tatu na kubaki za Km 162. Hizo baki nazo mwenyewe.

4. Ikiwa Noti moja ya elfu 10 ina uzito wa gram 1, maana yake kwenye Trilioni 1.5 (noti milioni 150) zina uzito wa gram milioni 150 (150,000,000gm) au kilogram 150,000 sawa na uzito wa tani 150. Reli ya Standard Gauge inayojengwa inaweza kuhimili mzigo wa uzito wa Tani 35.

5. Zinatosha kujenga kilometa 500 za Reli ya STG kwa viwango vya ubora na gharama za sasa (kwa mfano wa hii iliyoanza kujengwa)

6. Ukipewa pesa hiyo na kuamua kutumia Tsh. Mil 10 kila siku. Zitaisha baada ya miaka 41.
[(1.5x10¹²) ÷ (10x10e8)]/365¼ = 41

7. Zinatosha kugawa TSh. 200 kwa kila Binadamu duniani, TSh 1000 kwa kila Mchina na TSh. 30,000 kwa kila Mtanzania.

8. Ukiweza kuzigawa pesa hizo 'kipedejee' kwa kuwarushia watu noti moja moja kila baada ya sekunde moja, bila kupumzika, itakubidi utumie miaka minne na miezi 9 ili ugawe zote.

9. Tsh. Trilioni 1.5 ni utajiri karibu sawa na utajiri wa Bilionea Mohammed Dewji. Ni zaidi ya fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa kiwanda cha Cement cha Dangote (1.3trilion). Ni nusu ya Utajiri wa Rais wa Marekani, Bilionea Donald Trump.

10. Pesa hiyo ni mara 25 ya pesa waliotumia Marekani katika kushambulia miji ya Homs na Damascus nchini Syria tarehe 14 Aprili 2018. Marekani walitumia Nyambizi inayotumia umeme wa nyuklia, ndege ya kijeshi aina ya B-1 bomber na meli moja ya kivita huku bajeti ikiwa dola Mil 26, sawa na Tshs bilion 60. Wamarekani wameandamana nchini kwao kupinga matumizi mabaya a ya kodi zao. Kwa hizi pesa zetu zisizoonekana wangeweza kufanya mashambulizi mengine 24 kama hayo.
 
Hakuna 1.5 t iliyopotea. Mnajipa midomo ya bure tu kulalama kwa kitu msichokijua. Hii ni serikali yetu, mtuache tufanye kazi sisi tulio wazalendo. Subirini 2025 mumchague mbowe na wakati huo atakuwa kigagula kweli kweli.
 
Ngoja tuone magazeti ya kesho yataandika nini
Hii serikali ilipashwa kufutwa watu wapelekwe mahakamani jeshi liongoze nchi kwa muda tuwekane sawa.

Wabunge wa ccm mkikosea hapa kuiwajibisha serikali basi mjue mahakama itawahusu
WaTz sio wajinga muelewe hivyo
Mje mkanushe na hesabu zenu za kuungaunga
Salute Zitto!
Umeongea nini sasa yaani wewe ni hayawani kweli kweli. Serikali imechaguliwa na wananchi na ipo kwa mujibu wa katiba. Nyie endelewni kupiga porojo. Huyu ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote. Sasa utasemaje Jeshi lichukue madaraka? Lichukue mara ngapi wakati yeye ndio analiongoza? Hovyoooooo?
 
Habari wakuu.

Tangu nimesikia na kusoma ripoti ya CAG na kung'amua hela za kitanzania kiasi cha Trillion 1.5 leo ndio nimepata nguvu ya kuandika hapa jukwaani.

Trillion 1.5 hazina maelezo zimetumikaje hadi wkt huu.

Hebu nikupe picha ya hizi hela.

Hizi hela ukiziweka ktk noti za elfu kumi kumi unapata jumla ya noti 150,000,000. Ikiwa kila noti ya shilingi elfu 10 ina urefu wa sentimita 14.
Kwa hesabu rahisi ni kwamba ukiamua kuzipanga hizo hela kwa kupanga noti za elfu kumi kumi unapata jumla ya kilomita 21,000.
Yani noti za elfu kumi kumi zinapangwa kwa kilomita ishirini na moja elfu (21,000km) ndo trillion 1.5 inamalizika.

Kama hujaelewa jaribu hii sasa.
Ukiamua kupanga noti za elfu kumi kumi kuanzia Dar es salaam hadi Mwanza kwa barabara kupitia Morogoro-Dodoma-Singida-Tabora-Shinyanga hadi Mwanza hali inakuwa hivi.
Ili kuzimaliza hizo trillion 1.5 utalazimika kuzipanga noti za elfu kumi kuanzia Ubungo (Dar) hadi Mwanza, utazipanga tena kutoka Mwanza kurudi hadi Dar, utazipanga tena kutoka Dar hadi Mwanza, ukifika Mwanza tena utazipanga hadi Dar, utarudi tena ukizipanga hadi Mwanza, halafu utarudia tena, na tena...hadi mara 18.

Kiufupi trillion 1.5 inapangwa kwa msururu wa noti za elfu 10 kutoka Dar hadi Mwanza mara 18 na safari ya kumi na tisa utaishia hapo Morogoro.

Vipimo vya umbali wa barabara ni kwa mujibu wa SUMATRA (Dar -Mwz 1,154km).

Kweli hela za noti za elfu zinazoweza kupangwa kutoka Dar hadi Mwanza zaidi ya mara 18 hazina maelezo zipo wapi?
Hela ambazo elfu kumi kumi zitapangwa msururu wa kilomita 21,000 hatujui zimetumikaje?
Hivi kilomita elfu 21 si unakaribia marekani kwa urefu au?


Wakuu Huku ni kulogwa au ujambazi?
 
Pole pole anajua zilipo na kafaidika. Na yule tumbili pia anajua zilipo zilitumika kumnunua.
Mtulia pia angekuwa havalishwi nepi angekuja kuzitetea kwa sababu na yeye kazifaidi.

Mkuu yeye kajichimbia anawacheki tu agu anasema hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Kwa sababu akitoka huko ni kama faru ndungai.

Kwanza atampoteza alhaji mtu Mungu CAG na baada ya hapo zitto afu atavunja baraza la mawaziri akiwatupia mzigo.. Na media zote zitakula za uso fasta fast blog zote zima kama watashindwa kulipia dola 900.
 
Back
Top Bottom