Serikali ya CCM yachanganyikiwa na yaitumia polisi kuzima moto wa Chadema, kulikoni ?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Kwa kutambua mapema kuwa mkutano wa CCM ungedorora, jeshi la polisi linatumiwa kuficha aibu hiyo kwa kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa wilayani Tarime. Chadema yadaiwa imenyimwa kibali cha mkutano na maandamano kwa kisingizio cha kulinda usalama - Swali ni usalama wa nani ? Wananchi Tarime wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi lakini mbona Chadema wamefanya mikutano mingi na maandamano bila uvunjaji wowote wa amani ?

Je, ni amani ya CCM na viongozi wake ndio unalindwa ili wasipokee kisago kutoka kwa wananchi waliowachoka kama kilichompata mbunge wa Tarime au katibu wa CCM wa Arusha ? Itakuaje hao hao polisi wanaotakiwa kuwalinda wananchi wanakuwa wepesi kutumia silaha, zinazonunuliwa kwa kodi zao, kuwauwa kama mbwa ? Hiyo amani inakuwa hatarini tu pale wananchi wanapoikataa CCM na serikali yake ya kifisadi au hawa polisi tuwaeleweje ? endelea kusoma;

Tarime hali tete, polisi wamwagwa kila kona
Na George Marato, NIPASHE.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime na Rorya limetangaza kuzuia maandamano, mikutano na mikusanyiko yoyote ya kisiasa kwa kipindi hiki kwa maelezo kuwa hali ya usalama wilayani Tarime si ya kuridhisha kwa sasa.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishina Msadidizi, Constantine Massawe, aliliambia NIPASHE jana asubuhi mjini Tarime kuwa hatua hiyo imechukuliwa na Jeshi hilo kuanzia juzi Mei 18 mwaka huu kutokana na vurugu zinazotokana na kuuawa kwa watu watano kwa kupigwa risasi na polisi katika mgodi wa North Mara wilayani humo.

Alisema Chama cha Mapinduzi CCM, ambacho kiliomba kufanya mkutano wa hadhara mjini Tarime juzi ambao ulipangwa kuhutubiwa na Katibu Mkuu wake, Wilson Mukama ulizuiwa kutokana na sababu hizo za ki usalama.

Aidha, Kamanda huyo alisema licha ya CCM kuzuiwa kufanya mikutano wilayani Tarime pia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ambacho kiliomba kufanya mikutano katika mji wa Nyamongo na Tarime mjini pia kilizuiawa kufanya hivyo kwa sababu hizo.

"Hali ya usalama katika wilaya ya Tarime kwa sasa si ya kuridhisha hivyo tumezuia mikutano na maandamano yoyote ya kisiasa kwa wakati huu hadi hali itakapokuwa shwari,"alisema Masawe.

Katika hatua nyingine, Jeshi Polisi nchini limeanua kugharamia mazishi ya watu watano waliouawa na polisi katika wilaya ya Tarime kufuatia vurugu za uvamizi wa mgodi wa dhahabu huko Nyamongo wa North Mara.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Oparesheni Jeshi la Polisi nchini, Paulo Chagonja, wakati alipokuwa akizungumza na ndugu wa marehemu waliokuwa katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.

Chagonja aliwataka ndugu hao kuzika marehemu hao kwa kile alichodai kuwa kama ni kufa tayari watu walishakufa na hata kama wasipozikwa hawawezi kupata uhai.

Aidha, alisema kuwa serikali iko tayari kusaidia gharama za mazishi pamoja na kutoa ubani kwa ndugu wa marehemu ikiwa kama njia mojawapo ya pole. Alisema kuwa watu hao waliuawa kwa bahati mbaya kwani haikuwa nia ya askari hao kuua na kwamba waliouawa ni wavamizi na si majambazi kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali.

Aliwataka ndugu wa marehemu kuungana pamoja ili miili ya marehemu ifanyiwe uchunguzi na kisha ikazikwe lakini ndugu wa marehemu waligoma kwenda kufanya uchunguzi kwa kile walichodai kuwa hawana utaalamu wa kufanya uchunguzi huo.

Hata hivyo, alisema kuwa baada ya mazishi serikali itaunda tume kutoka makao makuu itakayoshirikiana na ndugu wa marehemu ili kutafuta chanzo cha mauaji hayo,na kwamba atakae bainika kuhusika kwa namna moja ama nyingine serikali haitasita kumchukulia hatua hata kama ni kiongozi wa serikali.

Ndugu wa marehemu hao waliendelea kusema kuwa ni jambo la ajabu serikali tena Jeshi kugharamia mazishi ya watu waliowaua kwa madai kuwa ni majambazi.

"Jamani iweje, jambazi likazikwa na serikali? Na kama ni jambazi iweje polisi mseme mtatoa ubani? Hatuziki mpaka kieleweke ili iwe fundisho kwa Jeshi kuua watu ovyo,"walisema ndugu wa marehemu.

Naungana na Polisi kuzuia mikutano yeyote ya kisiasa katika kipindi hiki!
its not about right, its not about politics, its not about politicians, its not about biasness and its not about brutality! Rather its about console and stability!
 
mfa maji haichi kutapatapa, wanadhani wameiza cdm kumbe ndo kwanza wanajimaliza. Chadema ni tumaini jipya la watanzania
 
Hata wakati wa kudai Uhuru Tanganyika,zilitungwa sheria kibao za kuzuia vyama vya siasa vya waafrika,mikutano ya Tanu ilizuiliwa,Tanu ikahujumiwa lakini mwisho wa siku waafrika walishinda na Tanu ikapeta...the same to CDM,this time tomorrow CDM will be the ruling party in Tz
 
Naungana na Polisi kuzuia mikutano yeyote ya kisiasa katika kipindi hiki!
its not about right, its not about politics, its not about politicians, its not about biasness and its not about brutality! Rather its about console and stability!
yaani wewe kweli ni papa D, na muda si mrefu utakuwa papa K
 
sasa mbona huyo Chagonja maelezo yake yamepishana na bosi wake kagasheki?juzi kagasheki alisisitiza kuwa wale walikuwa ni wahalifu sasa leo hii chagonja atubadilishie jina na kuwaita wavamizi?daaa kweli gamba si mchezo kudadadeki,hatuziki mtu hadi kielewekeeeeeeeee safari hii.
 
Huwezi kulinganisha Tanu na Chadema .hii ni sawa na kulinganisha Nyerere na Mutei au ugali na Mavi.
 
Naungana na Polisi kuzuia mikutano yeyote ya kisiasa katika kipindi hiki!
its not about right, its not about politics, its not about politicians, its not about biasness and its not about brutality! Rather its about console and stability!

Na polisi wangeruhusu basi ningefikiri kwamba hawa watu wana matatizo ya akili kama wale wanaofikiria kufanya maandamano katika hali ambayo usalama ni tete na watu wamefariki. Hivi hakuna kazi nyingine kwa chama hiki isipokuwa ni maandamano na hotuba hata misibani. Hakika siasa hizi za kichochezi hazipaswi kupewa nafasi na ndiyo mwanzo wa kuvurugika kwa amani. Leo ukiona mtu anasifia kiongozi kutaka kuuawa basi ujue huyu ana upofu wa fikra! Mkutano huo haustahili kufanyika na waking'ang'ania basi wana lao jambo na mkono wa chuma uwafikie!
 
Naungana na Polisi kuzuia mikutano yeyote ya kisiasa katika kipindi hiki!
Rather its about console and stability!

Hapo kwenye red, I wish I knew what you are trying to convey, unaweza kueleza kwa kiswahili ? Polisi waue wanaodai kuwa ni majambazi, hao hao polisi wawape pole wafiwa kwa kutoa rambirambi halafu hao hao polisi wazuie wengine kuwapa pole kwa kudai wanalinda usalama wao ! Hapana, huku ni kuingilia haki ya msingi ya mwananchi na kujaribu kukwepa ukweli kuwa wana Tarime hawana tatizo na Chadema, kama ni hasira itakuwa ni kwa hao wauaji na wavua magamba.
 
Tumaini jipya wakati mnachochoe fujo.Hii yote ni kwa ajili ya kushindwa kuingia Ikulu kwa njia ya kidemokrasia.Sasa mnatumia njia ya black market.Hakika itawtokea puani si siku nyingi.Kamwe hamwezi kuingia ikulu labda chama ambacho bado kuzaliwa.
 
naungana na polisi kuzuia mikutano yeyote ya kisiasa katika kipindi hiki!
Its not about right, its not about politics, its not about politicians, its not about biasness and its not about brutality! rather its about console and stability!
si lazima kuchangia wote kama point less tulia tu
 
Tumaini jipya wakati mnachochoe fujo.Hii yote ni kwa ajili ya kushindwa kuingia Ikulu kwa njia ya kidemokrasia.Sasa mnatumia njia ya black market.Hakika itawtokea puani si siku nyingi.Kamwe hamwezi kuingia ikulu labda chama ambacho bado kuzaliwa.

Hizi juvenile politics haziwezi kuwafikisha popote. Ukiuliza mikakati ya 2015 na kujaribu kuwa na level playing field huwezi kupata majibu. Wana mawazo ya kudhani maandamano yanaweza kuiondoa serikali ya watu! Baadae wadai wameibiwa kura, kwa sababu tu watu wanawashangilia katika mikusanyiko yao. Hawajui kwamba kwa sasa hiyo ndiyo outing ya watu.
 
Kama hiyo ndio "outing" ya watu, what does it tell you? Even to a dumb, it means watu wanaokwenda kwenye maandamano na mikutano ka outing basi HAWANA UWEZO WA KWENDA OUTING AMBAYO NI MORE ENTERTAINING!!!!
 
Na polisi wangeruhusu basi ningefikiri kwamba hawa watu wana matatizo ya akili kama wale wanaofikiria kufanya maandamano katika hali ambayo usalama ni tete na watu wamefariki. Hivi hakuna kazi nyingine kwa chama hiki isipokuwa ni maandamano na hotuba hata misibani. Hakika siasa hizi za kichochezi hazipaswi kupewa nafasi na ndiyo mwanzo wa kuvurugika kwa amani. Leo ukiona mtu anasifia kiongozi kutaka kuuawa basi ujue huyu ana upofu wa fikra! Mkutano huo haustahili kufanyika na waking'ang'ania basi wana lao jambo na mkono wa chuma uwafikie!

Hata huyo JK wenu alishasema (akiongea na UWT) kuwa anaekudhulumu hatakupatia haki bila kuishughulikia! Hata JK Nyerere aliitwa mchochezi, cha ajabu leo ni kipi?

Waambie waliokutumeni hivi: Watanzania wa leo si wajinga tena!
 
Very true, except you!
 
Kwa kutambua mapema kuwa mkutano wa CCM ungedorora, jeshi la polisi linatumiwa kuficha aibu hiyo kwa kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa wilayani Tarime. Chadema yadaiwa imenyimwa kibali cha mkutano na maandamano kwa kisingizio cha kulinda usalama - Swali ni usalama wa nani ? Wananchi Tarime wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi lakini mbona Chadema wamefanya mikutano mingi na maandamano bila uvunjaji wowote wa amani ?

Je, ni amani ya CCM na viongozi wake ndio unalindwa ili wasipokee kisago kutoka kwa wananchi waliowachoka kama kilichompata mbunge wa Tarime au katibu wa CCM wa Arusha ? Itakuaje hao hao polisi wanaotakiwa kuwalinda wananchi wanakuwa wepesi kutumia silaha, zinazonunuliwa kwa kodi zao, kuwauwa kama mbwa ? Hiyo amani inakuwa hatarini tu pale wananchi wanapoikataa CCM na serikali yake ya kifisadi au hawa polisi tuwaeleweje ? endelea kusoma;

[/LEFT]

Safi kabisa wtz tunaomboleza vifo vilivyotokea nyie wanasiasa mnataka kunufaika kisiasa aibu gani hii nyie cdm muda si mrefu mtapoteza mvuto
 
Wakimaliza Watutajie Majina ya Hao Askari Waliowanyofoa uhai Ndugu Zetu... Tuwaweke Kwenye List of Shame in Tanzania!!
 
Back
Top Bottom