Serikali walipeni "Mafao yao Wastaafu". Ni miezi 9 sasa toka wamestaafu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Wadau inasikitisha sana kusikia Wazee Wastaafu hawajalipwa Mafao yao toka walipostaafu Julai 2018.

Huu ni Mwezi wa 9 wamekuwa wanasotea Mafao yao lakini bado hawajalipwa, hebu tujiulize Wazee hawa wanaishije na Familia zao?

Ni vema Serikali ikawalipa Wazee Wastaafu Mafao yao pamoja na Pensheni zao za kila Mwezi kwani ndio kipato pekee walichonacho.
 
Hii serikali inayokopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii bila kurejesha huwa inajifikilia nini.

Mimi nadhani chama cha mawakili Tanganyika (TLS) kiwasaidie wazee hawa wafungue kesi mahakamani wawaburuze hawa mifuko mahakani wakaseme kwa nini hawalipi.

Wazee unganeni mkafungue kesi mahakamani maana wanataka mfe wagawane hizo fedha
 
Ni ujanja unafanyika kuwapunguza kwa kuwaua kwa stress.

Yaani mstaafu wa bongo anakuwa vonerted kiwa maskini wa kutupwa.

wasichojua hao watumishi wa pension ni kuwa na wao watastaafu siku moja
 
Ngojeeni tumalizie miradi yote
Ngoma hii mpaka 2040 ndy mtalipwa

Ova
 
Kama ni kweli basi hili jambo linailetea nchi laana kubwa sana.

Kifupi ardhi inalaaniwa. Miezi yote hiyo mnawazungusha? Yaani hata hao viongozi hawaoni kwamba ni uonevu kwa hawa wazee wetu?

Kwa kusikitika kwao tujue kabisa wanaachilia laana kwenye ardhi yetu. Inaumiza sana
 
Hi inchi ni mvurugano. We fikiria mtu kachota mahela kununulia korosho mpango usiyo kwenye budget , kwanini mambo mengine yasisimame
 
kweli wastaafu ktk nchi hii tuna hali ngumu sana, hatuna mtetezi labda tuseme aliyeshiba hajui mwenye njaa.
 
Bora hata wazee wastafu ni miezi 9 kuna wengine wanafuatilia MIRATHI toka 2017 mpaka sasa hawajalipwa, marehemu aliacha watoto wadogo wako shule za msingi na sekondari lakini serikali imeamua kufumba macho sasa sijui makato yake kwenye mshahara wake wameyapeleka wapi?
 
Dah...mshua anastaafu mwezi huu...hizi habari zinanitisha aisee japo atuitegemei hizo mambo namuonea huruma sana....anamipango yake mingi kinoma so ikichelewa kiasi hicho itamkwamisha sana..lets hope for the better.
 
Bora hata wazee wastafu ni miezi 9 kuna wengine wanafuatilia MIRATHI toka 2017 mpaka sasa hawajalipwa, marehemu aliacha watoto wadogo wako shule za msingi na sekondari lakini serikali imeamua kufumba macho sasa sijui makato yake kwenye mshahara wake wameyapeleka wapi?
Aiseee so sad
 
Kuna wazee Kenya walishawahi kuwafungulia kesi serikali ya uingereza nadhani kwa kuwatia ulemavu wakati wa ukoloni hukumu ilitoka na mahakama ilihukumu walipwe.

Ikiwa serikali haiwezi kuwapa haki yenu stahiki msikate tamaa na mawakili tunaomba muwape wazee hawa msaada wa kisheria haiwezekane leo wamewatumia watu hawa mpaka wamezeeka halafu leo na mafao yao wayale na matumbo yao yaliyojaa laana
 
Pole yao sana...

Jungu kuu halina ukoko...

Alafu ulipaji wa wastaafu haupo kwenye ilani ya chama kwa hiyo wasubiri kwanza...


Cc: mahondaw
 
Dah, jirani Yangu naye Julai hadi leo bilabila hd noma. Kachokaaa maskini Inatia huruma. Yaani km VILE Anasubiri fadhila Kumbe Ni haki yake
 
Kwa serikali zetu hizi ni vyema mtu ukaandaa uzee wako kwa njia tofauti na mafao na unatakiwa kuhesabia mafao kama umetoa sadaka fulani ili usijekuumia sana
 
Tuwe na subra wakuu. Tumenunua ndege 7 cash. Hao wazehee hawalijui hilo? Tunajenga reli ya umeme kwa pesa zetu wenyewe, hao wazehee hawaelewi?
Hao wazee hawategemei Standard Gauge kupata mlo wa siku.. wala Ndege kusomesha vijana wao.
 
Back
Top Bottom