Ni chombo gani kisheria kinachowasemea wazee wetu wastaafu katika masuala yao?

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasalimu.

Bila kupoteza Muda naomba nije kwenye MADA HUSIKA. NCHI hii ina sheria ya KUSTAAFU iliyopitishwa na BUNGE juu ya KUUSTAFU kwa WATUMISHI wa UMMA.

KUSTAAFU ktk NCHI kupo kwa Aina Mbili

1. Kuustaafu kwa HIARI (Miaka 55)
2.Kuustaafu kwa LAZIMA (Miaka 60).

WATUMISHI hawa WAKIISHASTAAFU hulipwa MAFAO na HAKI zao zote WANAZOSTAHIRI.
TATIZO lililopo kwa WAZEE hawa WASTAAFU Waliolitumikia TAIFA HILI kwa UAMINIFU MKUBWA mpaka WAKASTAAFU ni KULIPWA PENSHENI NDOGO SANA ya Kila MWEZI. .WAZEE hawa WASTAAFU karibu Asilimia 80 walikuwa WATUMISHI wa KAWAIDA hata MISHAHARA yao ilikuwa kidogo sana tofauti na KADA nyingine.

UDOGO wa PENSHENI ZAO za za MWEZI wengi wao HULIPWA Tsh 30000/= kwa Mwezi FEDHA ambayo haikidhi kununua Chochote.

Kutokana na hali hiyo WAZEE hawa WASTAAFU hawana CHOMBO chochote cha KISHERIA cha KUWASEMA MATATIZO yao kama Vile TUCTA TALGWU n.k.

WAZEE hawa WASTAAFU wamekuwa YATIMA hata WABUNGE hawawafikirii WAZEE hawa KUWASEA wakiwa ktk VIKAO vyao vya BUNGE KUWAONGEZEA Pensheni zao za kila MWEZI ili ziendane na hali HALISI ya KIUCHUMI ukizingatia hawana tena UWEZO wa kufanya SHUGHULI mbalimbali za kujiongezea KIPATO.

OMBI kwa SERIKALI
Tunaiomba SERIKALI iwape HESHIMA Kubwa WAZEE hawa kwa KUTAMBUA MICHANGO yao Wakati wa UTUMISHI wao kwa KUWAONGEZEA PENSHENI ZAO za kila MWEZI kwani WAMELITUMIKIA TAIFA hili kwa UAMINIFU na UADILIFU MKUBWA mpaka WAKASTAAFU bila KASHFA yoyote .
 
Wasemewe ili iweje, walipokuwa madarakani hawakutusikiliza wananchi walijiona Miungu watu. Wacha wataabike kama ni kweli. Na walioko madarakani wata-staafu na wao watapita humo humo. Tabu zao ni mafunzo kwa kizazi kijacho, wacha wapate tabu zaidi.
 
Back
Top Bottom