Serikali tusaidieni kuondoa Magogo mabuchani

Mel James

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
344
241
Habari za mda huu

Naenda moja kwa moja kwenye mada. Serikali tumekuwa tukikatiwa nyama kwenye magogo toka enzi za uhuru. Bucha nyingi hasa mikoani ni magogo.

Binafsi sijaona madhara au kusikia madhara ila ukweli ni kwamba kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kasi dunian kote na pia hulka ya binadamu, kila mtu anapenda kitu kizuri.

Tunaomba mtutolee haya magogo buchani kama mliweza mifuko ya Rambo hili sidhani kama kwenu ni shida. Tunaomba msamini pia kipato chetu tunapata kwa shida sana bado kodi kama zote basi tunaomba na sisi tupate anagalau kitu bora, isue ya mizani buchani hiyo imewashinda kucheki kama inapima sawa au sio sawa, ila hilo la magogo lipo ndani ya uwezo wenu.

Kuna kipindi nilisikia mnataka kutoa magogo badae ikawa kimya. Ila hongeren sana kuweza kusimamia ili la usafi jumamosi za mwisho wa mwezi hapa mkoani kwangu panarizisha sana.

Asanteni
 
Sure asee hii tabia ya kucharanga nyama kwa shoka kwenye magogo ni ya enzi za ujima. Ukinunua nyama inakiwa na vimifupa vidogo vidogo ukipika chakula unaweza kuvunjika jino wakati wa kula.

Watumie mashine za kukatia nyama zinakata mpaka mfupa vizuri tu. Hii ya kucharanga inakera sana. Inaharibu nyama.
 
Watetezi wa matumizi ya magogo wao ututaka kujiuliza kwa nini visu vya mashine ya kukatia nyama uisha na kutakiwa kubadilisha na kuweka kisu kipya. Wakimaanisha nyama iliyokatwa kwa kisu cha mashine ubaki na chembechembe za chuma kilichotumika kutengenzea kisu ambazo tunazila kupitia nyama hizo na mwisho wa siku tunapata madhara ya kiafya.
 
Naunga mkono hoja.. Huu usasa unatuletea madhara na maradhi mengi bila kujua
 
Mifuko ya rambo ina mbadala, magogo hayana mbadala japo wengi wanadhani msumeno wa umeme ndio mbadala, hapana. Kuna mabucha yaliweka msumeno wa umeme wakajikuta umeme ukikatika hawawezi kuuza nyama na huenda siku nzima au wiki kama uwajuavyo Tanesco.

Dar kuna maeneo ambayo kila siku umeme hukatika kwa siku nzima, fikiria watauzaje nyama bila uwepo wa gogo, pia gharama za umeme ni kubwa hivyo itabidi wapandishe bei.
 
Hongereni sana Dodoma, Iringa na Mbeya bucha karibu zote ni magogo.
Yale magogo hatari kiafya damu ya miaka nenda rudi huozeana kwenye gogo hivyo huwemo wadudu usioona kwa macho.

Dawa wananchi tuanze kususa kununua nyama yenye gogo na tuwaambie kabisa wenye hizo bucha
Serikali izifunge tu hizo bucha zenye magogo
 
Kwani hayaoshwi? Kwani hiyo nyama unakula mbichi?
 
Gogo unaoshaje likatakata linakuwa na vishimoshimo pia damu Inaingia kwenye vishimo na ndani ya gogo lenyewe sababu linafyonza damu linafyonza unaoshaje?
 
Kwa taarifa yako gogo linaoshwa na bucha lote pia.. Usipofanya hivyo nyama ya the next day haitauzika au haitalika kwa harufu..damu iliyooza ina harufu kali na mbaya
Damu iliyokauka kwenye gogo au chembechembe za gogo havina athari kama chembechembw za chuma toka kwenye msumeno wa umeme
 
Mapaka na mende husaidia sana kuyasafisha kwa kulamba na kula mabaki yaliyo ndani ya vishimo, sawa na vibao vya kwenye majiko ya baa ndiyo maana paka na mende wa sehemu hizo ni watani.
 
Watetezi wa matumizi ya magogo wao ututaka kujiuliza kwa nini visu vya mashine ya kukatia nyama uisha na kutakiwa kubadilisha na kuweka kisu kipya. Wakimaanisha nyama iliyokatwa kwa kisu cha mashine ubaki na chembechembe za chuma kilichotumika kutengenzea kisu ambazo tunazila kupitia nyama hizo na mwisho wa siku tunapata madhara ya kiafya.
Me siamini kabisa, chuma ipo ila kiasi kidogo sana hata kisu cha jikoni kinaisha. Visu vyenyewe vya buchani vinaisha. Sufuria zenyewe zinaisha na kutoboka.
 
Sure asee hii tabia ya kucharanga nyama kwa shoka kwenye magogo ni ya enzi za ujima. Ukinunua nyama inakiwa na vimifupa vidogo vidogo ukipika chakula unaweza kuvunjika jino wakati wa kula.

Watumie mashine za kukatia nyama zinakata mpaka mfupa vizuri tu. Hii ya kucharanga inakera sana. Inaharibu nyama.
Sema ni umaskini, nyama haitakiwi kuuzwa na mifupa. Unakuta mfupa upo tu, hata uboho wake haiwezekaniki kuutoa.
 
Watetezi wa matumizi ya magogo wao ututaka kujiuliza kwa nini visu vya mashine ya kukatia nyama uisha na kutakiwa kubadilisha na kuweka kisu kipya. Wakimaanisha nyama iliyokatwa kwa kisu cha mashine ubaki na chembechembe za chuma kilichotumika kutengenzea kisu ambazo tunazila kupitia nyama hizo na mwisho wa siku tunapata madhara ya kiafya.
Mbona hata hayo mashoka na visu wanavyocharangia nyama baada ya muda hunolewa, makali yanapoteaje kama sio chuma kinabaki kwenye nyama
 
Kwa taarifa yako gogo linaoshwa na bucha lote pia.. Usipofanya hivyo nyama ya the next day haitauzika au haitalika kwa harufu..damu iliyooza ina harufu kali na mbaya
Damu iliyokauka kwenye gogo au chembechembe za gogo havina athari kama chembechembw za chuma toka kwenye msumeno wa umeme
Chuma ni madini na mwili wa binadamu huhitaji madini.
 
Mifuko ya rambo ina mbadala, magogo hayana mbadala japo wengi wanadhani msumeno wa umeme ndio mbadala, hapana. Kuna mabucha yaliweka msumeno wa umeme wakajikuta umeme ukikatika hawawezi kuuza nyama na huenda siku nzima au wiki kama uwajuavyo Tanesco. Dar kuna maeneo ambayo kila siku umeme hukatika kwa siku nzima, fikiria watauzaje nyama bila uwepo wa gogo, pia gharama za umeme ni kubwa hivyo itabidi wapandishe bei.
Si kweli mtaani kwetu mabucha mengi vigogo tumesahau kabisa. Vile vigogo kwa kuwa hawavisafishi vizuri kwa maji ya moto kabisa vina uchafu mwingi sanaa...
 
Back
Top Bottom