Serikali (TAKUKURU) yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar

Hujui biashara kaa kimya. Kama hujui kuadimika kwa bidhaa ni habari njema kwa mfanyabiashara aliye na hiyo bidhaa na lazima aitoe taratibu huku anasoma hali inaendaje asije akauza yote leo kwa elfu kumi alafu kesho akaja mteja anaitafta kwa laki moja (anaweza akajinyonga kwa ujinga huo)
TATIZO LA MSINGI HAPA NI UHABA WA SUKARI NDIO MAANA HATA MIMI NINGEKUWA NAYO NINGEITOA KWA VITUO SIO KAMA BIDHAA IKIWA YAPATIKANA.
Unaongelea kuhadimika kwa namna gani mkuu? Uhadimu huo wa sukari ni fake na nafurahia akichukuliwa hatua haiwezekani viwanda vifanye bidii ya kuzalisha afu watu wanaficha sukari na kuuza bei juu si bora hiyo bei wangepewa wakulima kuliko mnaojifanya wafanyabiashara
 
Hii movie imetengenezwa.Ngoja muone kama kutakuwa na serious case katika hili

Tamko limetoka asuhuhi,jioni watu wanakamatwa!Si bure hata kidogo.
jamaa had ametoa lile tamko means uchunguzi ulishafanyika na data zishakusanywa inamaana JPM tayari alkua na taarifa zote kuhusu hao watu,tatzo lilopo viwanda vinashindwa kusupply sukari hadi ipite kwa wafanyabiashara wakubwa ndo hao wanacontrol bei (wanauwezo wa kucreate scarcity ili wapandishe bei) ingawa kiukweli baada ya kuzuia sukari ya nje ya ndani isingetosha....sasa taarifa zao zipo viwandani kwamba wamechukua shehena kiasi gani,dola ilichofanya ni kutafuta data amechukua shehena kiasi gani kwa muda gani na amesupply kiasi gani,kwa sasa hali inavyoonekana mambo ni kukomoana kati ya wafanyabiashara wakubwa na rais baada ya njia zao za kiujanja kufungwa, na sio kwamba JPM ameamua kuwabana ila anafuata sheria iliokuwepo ya ulipaji kodi ila kwa kipindi cha JK haikua ikizingatiwa .... hiyo issue hipo wazi pia mjue yule mtu amekua akiyasoma matatizo ndani ya serikali kwa muda mrefu sana ndo maana anacheza nayo kwa haraka sana,Raisi anapiga kazi kubwa na nzuri lakini ameweza kutengeneza maadui ambao na wenyewe wanamuundia mikakati.
 
Wahujumu uchumi wasakwe popote walipo
wakamatwe,hivi ni kwa nini hili
la sukari watu wanatokwa na povu?

Mbona wakulima wanalima mahindi yao,kwa ghalama
wakiishavuna wakitaka kuuza nje wanazuiwa kwa kisingizio
kwamba nchi itaingia kwenye njaa tukiuza chakula ovyo.
hapo soko huria liko wapi? kwa nini mkulima akipangiwa
la kufanya kwenye bidhaa yake,tunaona ni sawa,
mfanya kazi akipangiwa la kufanya kwenye nguvu yake
anayouza kila mwezi tunaona ni sawatu.
Mfanya biashara akipangiwa la kufanya kwenye biashara yake
tunapiga kelele?

Hivi ni nani aliyeweka viwango hivi nchi hii kwamba kuna raia wanaoguswa tukaona ni sawatu na wengine hawatakiwi kuguswa kabisaaa!
vinginevyo watu watapiga kelele mpaka basi?

Sote ni watanzania wenye wajibu wa kulijenga taifa letu
bila kuangalia maslahi binafsi.Kama kuna mtu anadhani
anaweza kuchezea mamlaka na akawa salama,muda wake umepita.
wote tujifunze kutenda haki.Mfanya biashara ale jasho lake
kama wakulima na wafanya kazi walivyokuwa wakifanya
kwenye uongozi wa serikali iliyopita wakati wafanya biashara wakijiamlia
la kufanya.
Unajua wabongo tushajaa miemko ya kichama,baada ya kukikosa chama wanachokita ...... wamesahau huu sio muda wa kuangalia chama bali ni kuangalia mtu anayefaa kutuongoza.
 
Ninyi kurupukeni tu kwa maamuzi ya kutaka sifa laini, mwishowe mtajirishe watu kwa kuwalipa fidia.
JK wakati anafunga Bunge la 10, alisema kuwa issue sio kukamata na kuweka mtu ndani then akudai fidia ya mabilioni.
Hillary Rashid ni bonge la tajiri sasa kwa maamuzi ya kukurupuka ya awamu ya Ben, mwisho wakamlipa hela ndefu na wenzake.
Mlikurupuka kuzuia licha ya kuambiwa ya ndani haitoshi, sasa mnaacha kukiri kosa la kukurupuka na kuanza maigizo.

Ova
Kama ya ndani haitoshi ni sawa, lakini hii iliyopo kwenye maghala ilitoka wapi na kwa nini iwepo kwenye maghala wakati watu hawana sukari? Yatapita tu na utabiri wako utabaki kwenye kumbukumbu kama utabiri wa TB Joshua.
 
Mimi nilipenda sana bunge liwe na wabunge wengi wa upinzani kwa sababu ya kuisimamia serikali ya Rais Magufuli lakini ninachokiona kwa sasa ni vulugu tupu kwenye kambi ya upinzani.

Kuna mambo mengine kama una fikra pevu huwezi kupinga hata kama wewe ni mpinzani. Hata kukaa kimya kunasaidia sana katika ulingo wa kisiasa kwa sababu wananchi wengi wanaona na kufanya maamuzi.

Mbunge wa CHADEMA ambaye mpaka sasa amenivutia sana katika mitazamo yake ya kujenga taifa ni Mwanadada Esther Matiko.

Kwenye nchi za wenzetu, kuna masuala mengine utakuta vyama vyote vikubwa bungeni vinaungana katika kupigania maslahi ya wengi. Kwetu Itikadi za siasa zinawafanya hata wenye fikra pevu kuwa kama wajinga au wapumbavu.

Nchini Uingereza kwa sasa vyama vyote vikubwa vimeungana kuhakikisha nchi inabaki kwenye Jumuiya ya nchi za Ulaya.
mtazamo wangu kwa sasa nahisi ukawa wapo kwa maslahi ya chama na sio nchi kama walituonyesha kipindi cha JK na hadi kufikia hatua ya kutuvutia vijana wengi.
 
Nasikia kuna wafanyabiashara walioficha sukari ili kujipatia manufaa na wengine wameshaanza kukamatwa. Ushauri wangu sheria ichukue mkondo wake.

Kwa mfanya biashara kuficha sukari wakati katika jamii kuna uhaba wa sukari ni kosa la uhujumu uchumi linaloitwa Hoarding commodities.
Kwa mujibu wa sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 1984 inayojulikana kama Economic and Organized Crime Control Act, Cap 200 of 1984 inasema mtu aliye na leseni ama la atakayeficha bidhaa zinazozidi thamani ya milioni moja na wakati huo katika jamii kuna uhaba wa bidhaa husika atakuwa amefanya kosa la uhujumu uchumi lijulikanalo kama Hoarding commodities. Kosa hili linahusisha pia uuzaji wa bidhaa kwa bei ya juu zaidi hasa kwa bidhaa adimu kwa jamii rejea kifungu cha 57(1) cha sheria tajwa.
Mahakama yenye mamlaka ya kushughulikia makosa haya ni Mahakama Kuu na pia inaweza ikatoa amri ya kupokonywa bidhaa husika (forfeiture).
Hivi hukumu ikitolewa kabla mtuhumiwa hajakamatwa wala kesi haijafunguliwa huwa inakuwaje? Nimesikia hiyo sukari itataifishwa na mhusika hataruhusiwa kufanya biashara nchini milele
 
Hebu sheria tuweke kando, acha majaji na mahakimu nao wapumzike. Kesi zimekuwa nyingi sana. Hivi mtu akihukumiwa kabla ya kukamatwa na kesi haijafunguliwa hapo inakuwaje? Mie sielewi kama niko Tz nchi inayosifika kwa utawala bora
 
Rais Magufuli aache ubabe bhana biashara huria kwan lazma nitoe stock yangu yote? Aboreshe viwanda vya kuzalisha sukar iwe nyng sio kuingilia biashara za watu subir serikali italipa hili km mtataifisha hiyo sukar iwe km zile samak

Mbona mafuta waliweza? Yes biashara huria but goverment has the resposibilty to regulate "hands of, eyes on"
 
jamaa had ametoa lile tamko means uchunguzi ulishafanyika na data zishakusanywa inamaana JPM tayari alkua na taarifa zote kuhusu hao watu,tatzo lilopo viwanda vinashindwa kusupply sukari hadi ipite kwa wafanyabiashara wakubwa ndo hao wanacontrol bei (wanauwezo wa kucreate scarcity ili wapandishe bei) ingawa kiukweli baada ya kuzuia sukari ya nje ya ndani isingetosha....sasa taarifa zao zipo viwandani kwamba wamechukua shehena kiasi gani,dola ilichofanya ni kutafuta data amechukua shehena kiasi gani kwa muda gani na amesupply kiasi gani,kwa sasa hali inavyoonekana mambo ni kukomoana kati ya wafanyabiashara wakubwa na rais baada ya njia zao za kiujanja kufungwa, na sio kwamba JPM ameamua kuwabana ila anafuata sheria iliokuwepo ya ulipaji kodi ila kwa kipindi cha JK haikua ikizingatiwa .... hiyo issue hipo wazi pia mjue yule mtu amekua akiyasoma matatizo ndani ya serikali kwa muda mrefu sana ndo maana anacheza nayo kwa haraka sana,Raisi anapiga kazi kubwa na nzuri lakini ameweza kutengeneza maadui ambao na wenyewe wanamuundia mikakati.
Kadiri siku zinavyozidi kwenda mbele ndipo naanza kuona mapungufu makubwa kati yetu tuliokuwa tunasapoti UKAWA, mie sikuchangua mgombea yeyote toka CCM baada ya kuona nchi ishatekwa na matajiri kuanzia kupata haki hadi huduma za kijamii. Nikaomba mungu ampe nafasi Lowassa kwa maamuzi yake strong hasa yanayogusa jamii. Nilifanya hivyo kama shukrani kwa Lowassa kuwezesha upatikanaji wa maji mikoa ya kanda ya ziwa hususani Shinyanga (Kahama). Lakini nimekuja kugundua kuwa wengi tuliokuwa tunasapoti UKAWA tulikuwa na agenda binafsi mioyoni mwetu kupitia post zao hapa jamiiforum. Naomba sana mungu ampe afya njema Magufuli na kweli binadamu hana shukran hata kidogo. Mimi naona magufuri amevuka hadi malengo yangu ya raisi bora,imara na aliyetayari kujenga uadui hata na marafiki zake kwa ajili ya Watanzania walio wengi na waliokata tamaa.
 
... wananyang'anya mtu mali yake kwa mabavu eti unagawa bure? hii imepilitiza ...na Mungu anaona
Dawa yake huyo, alitegemea auze mara kumi ya bei aliyo nunulia. Halafu nyie ndio mtakao kuja kulalamika kuwa bei juu sana. Waacheni washikishwe adabu. Serikali inajua ni sukari kiasi gani inazalishwa na matumizi ni kiasi gani, msifikiri watu wamekurupuka tu kupambana na hili swala.
 
Tatizo bei elekezi. Tusubiri mengi maana wafanyabiashara watafilisika wote sijui tutarudi tena kuanza kulipa kodi ya kichwa maana selikali inatoa bei elekezi bila kujua bei ya kununulia na gharama.za biashara.
 
Back
Top Bottom