Serikali (TAKUKURU) yakamata Tani 4,900 za Sukari iliyofichwa Mbagala na Tabata jijini Dar

Kwahiyo wewe unaona ni sawa mtu anunue sukari tani kwa tani then aweke store akiforecast kupanda kwa bei hapo mbeleni ndio auze?? Hii sukari tunayonunua elfu 3 sasa kwa kilo wewe unaona ni sawa tena usikute ulikuwa unaomba ifike mpaka elfu 10 ili ionekane serikali imeshindwa kufanya kazi...
 
Umeambiwa kama huiwezi hii kasi, uhame. Kumbe hujaondoka unaendelea kueneza chuki zako?

Rais katusikiliza na sasa imekubali ku import sukari bila ya masharti kama tulivyoshauri au hujaskia tangazo kama jana akiwa katesh! Wewe ndio ujiuluze kwa nini kawapuuza ushauri wenu wa kuto import
 
Sijakuuliza hayo uliyonijibu. Umekwepa swali langu ukatengeneza lako na ukalijibu. Soma swali langu unijibu, mbona simple tu!
Jifanye wewe ndio rais alafu solve hii problem na siyo kulalamika tu.

1. Viwanda Vya ndani vinazalisha sukari alafu haiuziki.

2. Wafanyabiashara wanaagiza sukari kiholela expired sukari kutoka nje.

3. Wafanyabiashara Wa ndani wanaamua kununua sukari yote kutoka viwandani alafu wanakaa nayo tu.

Wanaitunza Store.
 
Leo Takukuru wameanza kuweka wazi mambo wanayochunguza yakiwa katika hatua hii? Si ni Takukuru wenyewe walituambia sheria inawazuia kuweka wazi mambo yanapokuwa katika hatua ya uchunguzi? Ni mhemko au ni nini?
Mkuu huo ni mzuka tu pale wanapotaka kupata audiences. Wanajisahau kama walishatuambia sheria haziruhusu. Sas subri wakiwa wanamchunguza lugumi hutaskia lolote
 
Mkimaliza Sukari kavamieni Banks nao wanaficha Dola ili iadimike na kuuzwa kwa bei ya juu!
Uchumi ni Kanuni sio Amri, Kazi ya kusimamia uchumi inahitaji akili sio sio nyepesi kama kuwasha na kuzima Mwenge!
Mkuu umenena vyema.
 
Wanaofanya bei iwe 3000 ni pamoja na hao wanaoficha sukari ndani.. Au hata logic ndogo kama hii huelewi?
SIWEZI KUELEWA HIYO LOGIC YAKO NDOGO. Hata sukari isingefichwa bado isingeuzwa kwa hiyo bei elekezi ya 1800. Hivi kuna mfanyabiashara anayependa kupata hasara? Serikali imeshaagiza sukari na JPM amerudia hiyo kauli kuwa sukari italetwa ya kutosha na ya bei nafuu. Atakuwa mfanyabiashara asiye na akili anayeficha sukari wakati anajua sukari ikiingia itakuwa bei chini naye hatakuwa na pa kuuza kwa bei anayotaka yeye. Sasa hivi sukari kwa bei ya jumla inauzwa 55,000/- hadi 60,000/- kwa mfuko wa 25kg. Kwa maana hiyo kama sukari iliyoagizwa na serikali itaingia sokoni na bei elekezi ya 1800 mfuko huo wa 25kg utauzwa 40,000/- . Sasa huyo anayedaiwa anaficha sukari atakuwa na uji kichwani...!!
 
Kwanza huyo jamaa nilitegemea kafungwa au kunyongwa yaani sukari unanunua kwa bei ua chini afu unaiweka store uje uuze bei kubwa? Hana huruma kwa binadamu zaidi anawaza pesa kuliko uhai wa wenzake
 
Jifanye wewe ndio rais alafu solve hii problem na siyo kulalamika tu.

1. Viwanda Vya ndani vinazalisha sukari alafu haiuziki.

2. Wafanyabiashara wanaagiza sukari kiholela expired sukari kutoka nje.

3. Wafanyabiashara Wa ndani wanaamua kununua sukari yote kutoka viwandani alafu wanakaa nayo tu.

Wanaitunza Store.
Mwasita usinichoshe, hata ndoto tu ya kuwa raisi sijawahi kuota.
 
Mahitaji ya nchi ni tani laki tano kwa mwaka, uwezo wa viwanda vya ndani ni tani laki mbili kwa maana kwamba tani laki tatu inahitajika kuagizwa nje na wafanya biashara.
Swali nani alizuia wafanyabiashara kuagiza sukari nje na ni kwa ajili gani? kama ni kulinda viwanda vya ndani ili visiwe na ushindani je huyo mfanya biashara wa tani elfu nne kanunua kiwanda cha nje? kuna asuali mengi ya kuhoji hapa lanini niseme kosa la ukosefu wa sukari nchini na kuirudisha nchi enzi za ujima ni la Magufuli na sasa kwa sababu amezoea cheap politics anatafuta wa kumhamishia udhaifu huu na kwa sababu anatambua waTz ni kama manyumbu yatamwitikia tu kwa sauti kuu ndio mzee. Mwenye sukari hana kosa na hasa ukizihatia mtoa habari anakiri kuwa anatoa tani 250 kwa siku. Huo ni utaratibu wake toka awali na sii ameuanza mwaka huu.
Tunakoelekea kwa mtindo huu wa seikali ni kurudishwa kulipa kodi ya kichwa maana naona wawekezaji wakiipa kisogo Tanzania!
 
Baada ya muda mfupi wa rais kusema kuwa kuna wafanyabiashara wameficha Sukari, muda huu imeripotiwa kuwa huko Mbagala kuna Sukari ya zaidi ya tani 4,900 kwenye ghala la mfanyabiashara mmoja na imeelezwa zitachukuliwa hatua stahiki.

Chanzo: TBC, habari mpasuko.

Katika uchunguzi wake TAKUKURU pia imebaini kuwepo kwa mikakati ya dhati iliyokuwa ikifanywa na mfanyabiasha huyo kwa kununua sukari yote toka viwanda vya ndani na kisha kuihifadhi na kuuza bidhaa hiyo kidogo kidogo kwa wastani wa tani 250 kwa siku wakati alikuwa na uwezo wa kuuza zaidi jambo lililochangia uhaba wa sukari katika soko.

Kuficha bidhaa ni kosa la uhujumu uchumi na ni kinyume na Aya ya 3 Jedwali la kwanza Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 [Chapisho la Mwaka 2002]. Serikali haitavumilia hujuma za namna hii na itachukua hatua kali dhidi ya mfanyabiashara yeyote ataekwenda kinyume na sheria hii.

TAKUKURU imetoa wito kwa wafanyabiashara wote wa sukari kuacha vitendo vya kuficha sukari na vyombo vya uchunguzi vinafuatilia kote nchini na yeyote atakayebainika kufanya hujuma hizo atakabiliwa na mkondo wa Sheria.

Hapo kwenye Blue jamani huyu anauza tani 250 kwa siku ! na ati anaficha ! Tani 250 ni sawa na mifuko 5,000
kuuza kwa jumla kuna yafuatayo:
kuhakikisha vibaka hawaibi hivyo ulinzi wa ziada
kupokea oda na malipo
kupakia kwenye magari kutoka ndani ya ghala. Hapa kwa tunao jua kazi hizi lazima oda ziwe moja baada ya nyengine sio kujaza kila gari , hii nibiashara na majizi yapo katika kuitoa sukari ndani hivyo lazima extra caution.
sasa kila gari ikija kupakia mifuko kati ya 50 na 100 ni mgari mangapi yatakuja kuondoa hizo tani 250 ? wastani wa wanunuzi wa kitumbini na sehemu nyengine ni chini ya Tani Moja...sasa chukulia kila gari litaingia hapo na kuondoka na oda yake ya tani 5 ina maana tunazungumza magari 50 kwa siku ...
tuwe wakweli jamani magari 50 kwa siku nimengi mno
kila mtu anajua hizi canters zinabeba tani ngapi sana 5-7tns
sijaona ubaya wa huyu mfanya biashara ..fitina mbaya sana ..wala haimsaidii mtu yoyote ..kuhamisha matatizo kwa wengine
 
Mwasita usinichoshe, hata ndoto tu ya kuwa raisi sijawahi kuota.
Wambie na Chadema wenzako waache kulalamika tu bila kuleta solution.

Wanatakiwa waje na solution ili watanzania tuamini kuwa cdm ni mbadala Wa ccm.

Kulalamika tu haitufanye tuiamini chadema.
 
Huku mwanza siku ya tano hii sukari mtaani haipatikani...kuna baadhi ya maeneo huku kilo moja imefika elfu nne sasa..
 
Mkuu huo ni mzuka tu pale wanapotaka kupata audiences. Wanajisahau kama walishatuambia sheria haziruhusu. Sas subri wakiwa wanamchunguza lugumi hutaskia lolote
Mkuu mbona IGP ameshatolea ufafanuzi sikunyingi tu kuwa habari zilizoenea nchini kuhusu lugumi ni za uongo na za kupuuza...,i hali takukuru nao wanaendelea na uchunguzi , huku bunge likiwa limeshaunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza hilo sakata la lugumi.,,. Hapo tusitegemee chochote mkuu. Ni maigizo tu yanayoendelea nchini.
 
Wambie na Chadema wenzako waache kulalamika tu bila kuleta solution.

Wanatakiwa waje na solution ili watanzania tuamini kuwa cdm ni mbadala Wa ccm.

Kulalamika tu haitufanye tuiamini chadema.
Umenifanya nikujibu wakati nilishafunga mjadala na wewe. Sikiliza Mwasita tena nakueleza hili jambo kwa upole kabisa kutoka sakafuni mwa moyo wangu, ni makosa makubwa tena makubwa sana kudhani kila anayekosoa, anayehoji, anayepinga ni CHADEMA.
 
SIWEZI KUELEWA HIYO LOGIC YAKO NDOGO. Hata sukari isingefichwa bado isingeuzwa kwa hiyo bei elekezi ya 1800. Hivi kuna mfanyabiashara anayependa kupata hasara? Serikali imeshaagiza sukari na JPM amerudia hiyo kauli kuwa sukari italetwa ya kutosha na ya bei nafuu. Atakuwa mfanyabiashara asiye na akili anayeficha sukari wakati anajua sukari ikiingia itakuwa bei chini naye hatakuwa na pa kuuza kwa bei anayotaka yeye. Sasa hivi sukari kwa bei ya jumla inauzwa 55,000/- hadi 60,000/- kwa mfuko wa 25kg. Kwa maana hiyo kama sukari iliyoagizwa na serikali itaingia sokoni na bei elekezi ya 1800 mfuko huo wa 25kg utauzwa 40,000/- . Sasa huyo anayedaiwa anaficha sukari atakuwa na uji kichwani...!!

Kama uyu mfanya biashara ananunua sukar ya kieandani na kuificha atashindwa vipi kununu iyo sukari itakuyuingia kutoka nje na kuificha pia? Ndo mana lazima serikali ioneshe makali yake mapema ili kuzuia wajanja wachache kuchezea soko la sukari..!
 
Kwanza huyo jamaa nilitegemea kafungwa au kunyongwa yaani sukari unanunua kwa bei ua chini afu unaiweka store uje uuze bei kubwa? Hana huruma kwa binadamu zaidi anawaza pesa kuliko uhai wa wenzake
Hujui biashara kaa kimya. Kama hujui kuadimika kwa bidhaa ni habari njema kwa mfanyabiashara aliye na hiyo bidhaa na lazima aitoe taratibu huku anasoma hali inaendaje asije akauza yote leo kwa elfu kumi alafu kesho akaja mteja anaitafta kwa laki moja (anaweza akajinyonga kwa ujinga huo)
TATIZO LA MSINGI HAPA NI UHABA WA SUKARI NDIO MAANA HATA MIMI NINGEKUWA NAYO NINGEITOA KWA VITUO SIO KAMA BIDHAA IKIWA YAPATIKANA.
 
Kama uyu mfanya biashara ananunua sukar ya kieandani na kuificha atashindwa vipi kununu iyo sukari itakuyuingia kutoka nje na kuificha pia? Ndo mana lazima serikali ioneshe makali yake mapema ili kuzuia wajanja wachache kuchezea soko la sukari..!
Basi huyo mfanyabiashara anayeweza kufanya hayo yote na serrkili ipo, atakuwa bonge la kipanga na serikali yote ya JPM watakuwa bonge la vilaza.
 
Back
Top Bottom