Serikali sasa taabani, wanafunzi vyuo vikuu kutolipwa pesa zao.

don-oba

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
1,387
677
Ikiwa imepita takribani wiki moja, tangu nimeripoti hazina ya taifa kukauka kupelekea kukatwa pensheni za wastaafu serikali, sasa imegeukia wanafunzi vyuo vikuu nchini.

Akiongea na wanafunzi CHUO KIKUU CHA MT AUGUSTINE-, makamu mkuu wa chuo Rev Dr Charles H. Kitima amesema kwamba serikali kupitia bodi ya mikopo imesema haina pesa za kuwalipa wanafunzi wa chuo icho walioanza semister ya pili tangu february 13 mwaka huu.

Aidha ametishia kutowapokea wanafunzi walio chini ya udhamini wa serikali ktk mwaka wasomo unaokuja. Aliendelea kusema bodi yamikopo hutoa 'meals and accomodation' na kuwacheleweshea 'tuition fee' ambapo chuo hushindwa kujiendesha chenyewe. 'SAUT' ni chuo pekee nchini ambacho tuition fee yake ni ndogo.

Inavyosemeka serikali ina haha kutafuta pesa kuwalipa wanafunzi vyuo vikuu. Cha kushangaza hapa, ni kwamba bajeti ilishapita na fungu kutengwa, je sirikali ilimega?. Takribani wiki mbili sasa wanafunzi wa SAUT hawajapewa fedha zao hali inayowaathiri kimasomo.
 
Hii habari ni ya kweli kabisa. Muda mfupitu uliopita nilipigiwa simu na Binti yangu aliyeko hapo SAUT akinijulisha kuwa wameambiwa hadi mid- March ndipo watakapopewa hela zao za kijikimu. Ni aibu na masoneneko, na ni hatari pia kwa vijana wetu. Kama mzazi/mlezi hana jinsi nyingine ya kusaidia, vijana hawa wataangukia kubaya.
 
Hii haina cha kushangaza kwani ikumbukwe Mh. zitto alishasema kutokana na inflation plus financial crisis iliyojitokeza ni lazima budget yetu kushake tena alitoa mpaka makadirio ya zaidi ya shs 780 bil kuwa inakadiriwa kujitokeza kama deficit kwa kushuka kwa thamani ya shs kwa kuzingatia budget yetu ya 2011/2012, soma www.zittoworldpress.com cha msingi na kwa ushauri wa bure ni serikali kuchukua juhudi za makusudi kufunga mkanda na kuachana na matumizi ya siyo na ulazima hususan luxurius na badala kuhimiza zaidi uzalishaji wa ndani kama kilimo, ufugaji, na si kwa maneno kama ilivyo sasa kilimo kwanza na mbegu fake, mbolea kukosekana, ruzuku za kisiasa, na kuweka matrecta showroom kama pale dodoma, mbeya nk. nainaamini tunaweza lakini si kwa kuthubutu bali kwa kuchukua hatua za zati za kuwawezesha watu wetu kutokana na uhitaji wao na kwa wakati.
 
Wako wapi wale wapenzi na watetezi wa magamba waliotoa povu kupinga kuwa serikali imeishiwa? Waje tena hapa wabishe (ukichukulia kuwa serikali yenyewe imeshakiri)!
 
Tatizo serikali yetu haikubali kabisa mawazo ya upinzani,zitto kawahasa jinsi ya kufanya lkn hawakumsikiliza ona sasa wanaumbuka,bora jk alivyoenda uk kuongea na cameroon.
 
Bajeti ilishatengwa, imekuaje wamemega hilo fungu?. Inavyosemekana wali-double budget.
 
hatuna serikali tanzania tuna genge la mafisadi ambao wamepeana uongozi ili mwenye kusafiri kila siku asafiri na mwenye kula pesa za wananchi ale tu.kiukweli zamani nilikua nasikia fahari sana kua mtanzania ila sasa hivi hali ni tofauti kabisa
 
Take total Government/GDP for 2009,2010 and 2011; if the ratio is increasing there is a crisis if it is stagnant or decreasing there is no any financial crisis
 
Hapa kuna bomu zito linakuja, watanzania tukaemkao wa kusubiri tu maana hawa jamaa wa UDSM wapo njiani next week na mziki wao si mdogo. Tutegemee mihula ya masomo vyuoni kusogezwa mbele. Wakuu wa vyuo nao waache kuwa politician waikomalie serikali iwape wanafunzi wao pesa za kujikimu la sivyo wawaamuru warudi majumbani mwao kuliko kuwaacha bila suluhisho.
 
JK wewe si ni mchumi?, ongezea akili nyingine ku-stablelize hii hali.
 
Ngoja udsm tufungue hyo j3 afu tujibiwe ****** ka huo waliojibiwa wana saut tuone kama patakalika hapo magogoni!!
 
Naona wameamua kuifumua bajeti ya kila kitu na kuhaha kusaka ela.
Naona tusahau bajeti iliyopita maana haipo tena kilichobaki sasa ni kukabana koo na trafic pamoja na TRA na vyanzo vingine vya mapato ili kipataikanacho ndo kitumike
 
jamaan huku saut hali ishakua mbaya, dada zetu washaanza kujipiga mnada yaani hadi buku mbili..baba mwanaasha tusaidie bwana watu tunashindia mlo mmoja kwa siku tenaa chai
 
Bajeti ilishatengwa, imekuaje wamemega hilo fungu?. Inavyosemekana wali-double budget.

fanyeni kitu wanaSAUT! kitakacho wakumbusha hao MAGAMBA! sisi tutawaunga mkono wiki ijayo! subiri tufungue tukinukishe! nahuu uchaguzi wa ARUMERU ndopesa zinaisha kabisa!
 
jamaan huku saut hali ishakua mbaya, dada zetu washaanza kujipiga mnada yaani hadi buku mbili..baba mwanaasha tusaidie bwana watu tunashindia mlo mmoja kwa siku tenaa chai[/QU
WACHA UJINGA WEWE INA MAANA MKOPO UMEWAATHIRI ZAIDI WATOTO WA KIKE MPAKA WAJIPIGE MNADA?KAMA WAO WANAFANYA HIVYO WEWE UNAFANYA NINI?ACHA TABIA YA KUDHALILISHA WANAWAKE!JENGA HOJA NA UTASIKIKA SI KUONGEA ******!TENA UKAE UKIJUA WAKATI WEWE UMEKAUKIWA MTOTO WA KIKE HUWA NA AKIBA!
 
Back
Top Bottom