Serikali (NIDA) imefeli vibaya mno suala la vitambulisho vya taifa; kusubiri zaidi ya mwaka, vitambulisho vinapotea haviwafikii walengwa!

kwahiyo kuwa na namba ya kitambulisho tu inatosha bila kitambulisho chenyewe?Au nyienavutika tu kuifahamu hiyo namba
 
Kumba_fu sana NIDA, text imeingia like six in the morning nikatuma... Pesa wamekata hadi saivi nasubiri mrejesho.

Usile Mbegu.
 
website ya NIDA ambayo ni www.nida.go.tz haifunguki.
Na wanaoenda pale kutafuta huduma wanapata majibu ya njoo kesho au keshokutwa.

Tanzania tunarudi enzi ya ujima kwa matakwa ya watu wanaotaka kufaidika.
 
Hii ndiyo Tanzania ya kudanganywa na wenye shibe, vitambulisho vya uraia kutoka NIDA ni fupa gumu, limeshindikana, kila anaejaribu kulitafuna anaishia kulilamba lamba tu utamu ukiisha analitupa, mpaka mwishowe litajiozea lenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyakazi wengi wa NIDA wana kauli mbovu kwa watu wanaoenda kupata huduma ofisini kwao. Jana nimefika ofisi za NIDA manispaa ya Moshi mjini zilizopo KDC lengo likiwa kuuliza kuhusiana na kitambulisho baada ya kutumiwa Ujumbe kuwa tayari kitambulisho kishagaiwa na kupewa NIN, lakini zaidi ya hapo Ujumbe ulinieleza nifike ofisini kwao....
Niliamua kufika nikitegemea kupewa kitambulisho changu au kupata mwongozo wao. Nilifika pale ofisini kwao lakini ajabu ni kwamba takribani wafanyakazi wote walikuwa busy na simu zao huku wakitoa majibu ya hovyo kwa raia. Nlipofika niliwasalimia akaitikia mmoja tu wengine wananiangalia kwa dharau... Nkamwambia nimerudi hapa kufuatilia kitambulisho kwa mujibu wa Ujumbe nlotumiwa, yule jamaa akaniuliza jina nikamtajia alipocheki akanambia ondoka uje cku nyingine bado hakijatoka na akanambia Ujumbe nlotumiwa haukunambia niende ofisini... Nikataka kumweleza juu ya Ujumbe nlotumiwa akawa mkali kuwa cjaelewa Ujumbe nirudi nikausome vzuri... Nikakomaa nae nikamwonyesha Ujumbe kwenye simu na kumuonyesha kuwa nimeambiwa nifike ofisini kwao, baada ya kuusoma akabaki anababaika na ili kuniondoa... kwa walofika ofisi za NIDA Moshi huwa kuna Dada mmoja simfahamu jina lakini huwa anajibu watu vibaya sana akawaka na kusema "kwahyo unabishana na sisi au" nlichomjibu ni kwamba... Mimi nimetumiwa Ujumbe nifike hapa kuuliza na hata kama sikuuelewa bado unapaswa kunielewesha. Akabaki kimya, yule jamaa akanambia bado hakijatoka nikamuuliza lini kitakuwa tayari akanambia njoo mwezi wa tano.... Nikaondoka zangu wakiwa busy na simu zao.

Kuhitimisha, ni kwamba wafanyakazi wa NIDA na mamlaka nzima ni jipu lililoiva na linapaswa kutumbuliwa. Bila kuchukuliwa hatua mapema wataendelea kukwamisha nia njema ya serikali kuwahudumia wananchi wake. Pia nitoe rai kwa mamlaka husika hususan NIDA wilaya ya Moshi mjini waangaliwe kwa jicho la pekee maana wanafanya kazi kama hawataki na malalamiko ni mengi ya wanaoenda kupata Huduma pale. Kama pia wafanyakazi wa ofisi za. NIDA - Moshi wanaona Uzi huu nadhani pia ni nafasi yao kujirekebisha utendaji wao maana hawajui siku wala saa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kama una wasiwasi hivi Mkuu au Uraia wako una ulakini?
Nchi tunaelekea mfumo wa e~government, sasa huduma nyingine na habari si lazima kwenda maofisini na kupanga foleni za kupoteza siku nzima na fedha za nauli na mafuta halafu uambiwe njoo kesho.

Mbona LUKU ya TANESCO, maji ya DAWASA zimekuwa mafanikio?
NIDA kuna mtu anahitaji kutumbuliwa.
 
Mmekuwa mkituma msg kwa wananchi kupata taarifa za vitambulisho vyao vya Taifa binafsi nimetuma mara mbili, nilichoambulia nikukatwa salio tu na hamna taarifa yoyote niliyotumiwa.Hivi kwa staili hii mnavuna mamilioni mangapi ya dhuluma kwa wavuja jasho, machozi ya masikini ni mabaya mno mnaweza jikuta kwenye anguko la aibu kama watangulizi wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kumbe na eee umekumbana na utapeli wa taasisi hii ya serikali,

Hivi serikali hii itaacha lini dhuruma kwa wananchi?
 
Back
Top Bottom