Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,814
- 11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 19 leo Mei 5, 2023.
Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia IGP imewataka ma RPC, OCD na wakuu wa vituo vya Polisi kukagua mara kwa mara mahubusu ili kuona watu waliopo ndani sababu gani zinafanya waendelee kukaa ndani ili waachiwe kama hakuna sababu za msingi za kuwashililia.
Aidha, Serikali imebaini pia kuwa baadhi ya watu wanaowekwa ndani hata ndugu zao hugoma kuwawekea dhamana sababu ya matukio ya kujiridua wanayofanya ambayo hufedhehesha jamii.
"Niwaombe pia ndugu wawe wepesi pia kuwadhamini kwa wale ambao dhamana zinakuwa wazi, lakini tumewasisitiza wakuu wa vituo, pale inapowezekana kwa makosa yanayodhaminiwa waweze kutoa dhamana" amesema Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini.
DKT. TULIA: MBEYA JIJI HAKUNA GARI LA ZIMA MOTO, PELEKENI GARI
Spika Dkt. Tulia Ackson amesema “Mbeya Jiji hakuna gari la Zimamoto na majanga ya moto yanatokea mara kwa mara, hivyo pelekeni gari.”
Awali, Mbunge Stella Simon Fiyao alisema ni Halmashauri 2 (Mbozi na Tunduma) kati ya 5 Mkoani Songwe hazina huduma ya magari ya Zimamoto, huku Halmashauri za Ileje, Momba na Songwe zikiwa hazina huduma na hata zile zenye huduma hizo zina magari madogo.
Akijibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema “Tunawasiliana na Mkuu wa Zimamoto ili kupata gari moja wakati mpango wa Serikali wa kununua magari ukiwa njiani, pia kwenye Wilaya ambazo hazina magari hakuna matukio ya majanga ya moto ya mara kwa mara."
BULAYA AHOJI KILICHOPO NYUMA YA PAZIA SAKATA LA TANGA CEMENT NA TWIGA CEMENT
Mbunge Ester Bulaya amehoji kinachokwamisha mchakato wa kibiashara unaoendelea kati ya Kampuni ya Twiga Cement na ile ya Tanga Cement, akitaka Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara kuelezea kwa undani kilichopo nyuma ya pazia na kuhusu maslahi ya Taifa katika skata hilo.
MBUNGE: KWA NINI WAKIMBIZA MWENGE WALIMWAGA POMBE ZA KIENYEJI MTWARA?
Mbunge wa Momba, Condester Michael Sichalwe amehoji sababu za mamlaka kuzuia uuzwaji wa Pombe za kienyeji Nchini na kudai unachangia kuminya ubunifu wa wazawa wakati vinywaji kutoka nje ya Nchi vinaruhusiwa kuingizwa na vinauzwa kwa bei kubwa.